Kitendo cha Manara kumpiga madongo ya wazi Barbara ni ukatili, binti wa watu almanusura azimie

Kitendo cha Manara kumpiga madongo ya wazi Barbara ni ukatili, binti wa watu almanusura azimie

Kabla ya kubishana na mtu uwe unaangalia jina lake la bandia kwanza.!
Angalia huo mjadala mm na yeye tulianza wapi usisome post za mwisho anzia tokea mwanzo halafu uje kunipa jibu nani alianza kukosea
 
...Manara amekua home akiona Yellow and Green tu Simba alikuja kusalimia na kupiga hela na kuchota siri zenu tu na sasa unaona matunda yake pale Yanga! Mganga gani wa Simba asiemjua? Njia gani ya kupita kuipasua Simba asiyoijua?
Kwa ufupi tu unatuambia kwamba mafanikio haya ya Yanga yameletwa na Manara. Maneno mengine umeongezea nyama tu
 
Huu ni udhalilishaji

Kwa kweli kitendo cha Manara kumtupia madongo huyu binti ilikuwa ni ukatili, yani Barbara alikuwa anaombea tu muda uende haraka Manara amalize maana si kwa makombora ya madongo haya Manara aliyokuwa akimfyatulia binti, Manara ana mdomo mchafu aiee.

Ilibidi binti wa watu aangalie pembeni na aikaze sana mikono na meno ili kujizuia asitetemeke na kuzuia machozi

View attachment 2248585

Manara kaona haitoshi bado anapasha kiporo kaweka hii video insta, huu sio ukatili kweli?

View attachment 2248544
Dah! Wanaume tuko tofauti!!
Kaongea Barbara, Senzo, Ahmed wote wamekwenda kwenye point hakuna mpasho, matusi wala majigambo ila Haji pekee ndo kaleta fyoko zake. Ivi umeshindwa kuona tofauti ya hao watatu na huyo unaemsifu?!
Mwanaume unasifia mipasho kutoka kwa mwanaume mwenzio kwenda kwa mwanamke!!!
Dunia inaelekea ukingoni.
 
Dr. Haji Manara amwita Ahmed Ally Dogo
 

Attachments

  • hajismanara~tv~CeXumKVIS1V~1.mp4
    3.7 MB
ha ha ha! kipato huleta majivuno! huu msemo anaupenda sana Msemaji wa Makolo FC!

Feisaaaaaaaaalll!! anachanja mbuga ndugu msikilizaji , anaachia kombora kali, la la la la, Goooooooooooal!
Mnyama anachinjwa na kisu kikali ndugu msikilizaji!! CCM Kirumba kumekucha!! Yanga moja Simba sifuri na sidhani kama watarudisha bao hili la karne, bao la kideoni!! Ama kwa hakika timu ya Mikia ni mbovu kabisa!!Onyango wa Makolo FC anaanguka ovyo!!

Goli moja la Fei Toto aka "Zanzibar finest" limeipasua Makolo FC vipande vipande na kuisambaratisha kabisa na kuleta utani unaokera sana na kuumiza sana mioyo ya wanasimba!

Yanga ni BRAND KUBWA Ili kuacha kutembeza bakuli forever, Yanga, kupitia GSM au mkopo wa benki ijenge Petrol stations nchi nzima zenye nembo ya Yanga , inunue mabasi ya kwenda mikoani yenye rangi na nembo ya Yanga au itengeneze vinywaji baridi kama juice na maji na labda pia viwanda vya unga wa ngano na sembe na vyote viwe na Lebo ya Yanga na picha za Mayele , Manara na Feisal , mashabiki wa Yanga ni mamilioni dunia nzima watakunywa , watanunua , watalipia na kula bidhaa zenye brand ya Yanga tu hasa siku tunazoifunga Simba na hivyo kujaza pesa mfuko wa Yanga , "mwananchi" gani hatapenda kupiga picha au selfie akiwa amekamata "juice" yenye picha ya Feisaaaaaaaaalll!!

sisi wabongo ni wagumu sana kuchangia timu bila return yaani kulipia kitu bila kupata kitu . Yanga wasinisahau kwa wazo hili just 1% share of profit please !
Ubunifu poa kabisa, lakini kwa maoni yangu mimi wasinunue mabasi ya kusafirishia abiria, very risk kama yakipata ajari hata mawili ujue biashara hapo itakuwa imekufa na simba watapata jambo la kuwapiga nalo Yanga
 
Back
Top Bottom