ha ha ha! kipato huleta majivuno! huu msemo anaupenda sana Msemaji wa Makolo FC!
Feisaaaaaaaaalll!! anachanja mbuga ndugu msikilizaji , anaachia kombora kali, la la la la, Goooooooooooal!
Mnyama anachinjwa na kisu kikali ndugu msikilizaji!! CCM Kirumba kumekucha!! Yanga moja Simba sifuri na sidhani kama watarudisha bao hili la karne, bao la kideoni!! Ama kwa hakika timu ya Mikia ni mbovu kabisa!!Onyango wa Makolo FC anaanguka ovyo!!
Goli moja la Fei Toto aka "Zanzibar finest" limeipasua Makolo FC vipande vipande na kuisambaratisha kabisa na kuleta utani unaokera sana na kuumiza sana mioyo ya wanasimba!
Yanga ni BRAND KUBWA Ili kuacha kutembeza bakuli forever, Yanga, kupitia GSM au mkopo wa benki ijenge Petrol stations nchi nzima zenye nembo ya Yanga , inunue mabasi ya kwenda mikoani yenye rangi na nembo ya Yanga au itengeneze vinywaji baridi kama juice na maji na labda pia viwanda vya unga wa ngano na sembe na vyote viwe na Lebo ya Yanga na picha za Mayele , Manara na Feisal , mashabiki wa Yanga ni mamilioni dunia nzima watakunywa , watanunua , watalipia na kula bidhaa zenye brand ya Yanga tu hasa siku tunazoifunga Simba na hivyo kujaza pesa mfuko wa Yanga , "mwananchi" gani hatapenda kupiga picha au selfie akiwa amekamata "juice" yenye picha ya Feisaaaaaaaaalll!!
sisi wabongo ni wagumu sana kuchangia timu bila return yaani kulipia kitu bila kupata kitu . Yanga wasinisahau kwa wazo hili just 1% share of profit please !