Hivi karibuni Benjamin Netanyahu alisikika akisema anataka jeshi lake liingie Rafah na kufanikisha mpango wake wa kuwamaliza Hamas kabla mwezi mktukufu wa Ramadhani haujaingia hapo Machi 10.
Baada ya kitisho hicho Misri imekuwa ikitishia kuvunja mkataba wa camp david baina yake na Israel.Hata hivyo kitendo cha kupeleka jeshi kujenga ukuta mwengine ndani ya upande wake pembezoni mwa jangwa la Sinai kunaweza kukazusha wasi wasi juu ya nia yake hasa.
Jee ujenzi huo ni kambi nyengine kwa ajili ya watu wa Gaza au ni kwa ajili ya kambi ya jeshi lake kulinda mpaka huo.
Na jee kitendo cha Israel kusitisha kwa muda zoezi la kuingia Gaza kwa kutumia vikosi vya ardhini wamesikia nasaha za walimwengu kwamba kutasababisha madhara makubwa bila kutoa tija au ni kusubiri ujenzi huo unaofanywa na Misri ukamilike.
Wasi wasi huo umekuja baada ya picha za satelite kuona ukuta mkubwa ukijengwa takriban maili mbili upande wa Misri kutoka ukuta mwengine iliyojenga hapo awali wenye seng'enge juu yake.
Gaza si eneo la Israel na linakaliwa na watu wenye uhusiano mkubwa na Misri.Kilichotarajiwa kufanywa na Misri ili kuwalinda na kuwasaidia watu wa Gaza na kuingiza jeshi lake upande wa pili ndani ya Gaza ili kuzuia israel isifike hapo katika kuwawinda kwao Hamas.
Alwaz: Kuna maswali ambayo ni muhimu kuyajibu, hasa watu kama wewe uliyeamua kuwa Pro Hamas bila kuchambua zipi ni pumba, na upi ni mchele!
- Egypt ilifunga mpaka wake na Gaza toka 2005, Rafah crossing kwa Mpalestina inataka vibali maalumu! Mpalestina hawezi kuingia Egypt, labda awe na dual Citizenship, na maybe anapita on transit. Kwa lugha nyepesi Wapelestina hawatakiwi Egypt.
- Israel inalaumiwa imeifanya Gaza Open air prison, Watu hawajuilizi kama Gaza iko kifungoni, walioifungia ni Israel na Egypt kwa pamoja! Israel imefunga upande wake! Wapelestina wanaingia kwa vibali! Kufanya kazi, kutibiwa, na nimesikia hata kutoa mimba! Mwanamke hawezi kutoa mimba Gaza! Uwe umebakwa, umepata mimba nje ya ndoa lazima uende Israel! Baniani mbaya kiatu chake dawa!
Na Egypt ina sababu tosha kabisa, hiyo Itikadi ya Hamas ni sumu kali! Wamejifunza adha za Moslem Brotherhood, na madhara ya kuwakaribisha Wapelestina nchini kwako, wakiangalia nini kilifanyika Jordan, na Lebanon iliyokuwa nchi ya mafanikio huko nyuma, leo Lebanon is totaly failed state! Hizbollah imeiweka kifungoni serikali na wananchi wa Lebanon!
Israel inalaumiwa ni Apartheid State, kwa nini Egypty hailaumiwi? Unaona wazi double standard ! Egypt imeikalia Gaza miaka mingi tu, iliporudishiwa Sinai peninsula 1982 ikagoma kabisa kuichukua Gaza, ambayo toka mgao wa awali wa UN, Gaza ilikuwa upande wa Waarabu ( Angalia UN Partion 1947 map) ( Baadaye wakaibali jina na kujiita Wapelestina) Egypt hailamumiwi kabisa! Waarabu hawalioni hili, Inashangaza sana!
Sasa hivi ia ya Israel kuipiga Rafah ( ambayo ndio imebakia stronghold ya Hamas) Egypt imekwenda kabisa kuweka mpaka kama wa chuma! Haitaki kabisa kusikia Mpalestina anakimbilia huko! Husikii kabisa hizo kelele za "Humanitarians" Wala lawama kutoa kwa Waarabu wenzao!
In short Israel, kama mambo hayabadiliki Rafah inavamiwa, Israel hamsikilizi Mwamerika, wala mpatanishi Qatar!
Kwa kifupi vita hii imeweka wazi interests za Waarabu......Mpalestina ni ndugu wao wa kambo....sana sana wana share Uislamu! Hakuna jingine! Nakubaliana kabisa na Zuheir Mohsen, kiongozi mwandamizi wa PLO, aliposema maneno haya:
- The Palestinian people do not exist. There are no differences between Jordanians, Palestinians, Syrians and Lebanese. We are part of one people, the Arab nation. Lo and behold, I have relatives with Palestinian, Lebanese, Jordanian and Syrian citizenship. We are one people. It is only for political reasons that we carefully endorse our Palestinian identity. Indeed, it is of national interest for the Arabs to encourage the existence of the Palestinians in the face of Zionism. Yes, the existence of a separate Palestinian identity is only for tactical reasons. The establishment of a Palestinian state is a new means to continue the struggle against Israel and for Arab unity.
Wapalestina ni kiungo tu cha kuwaunganisha Waarabu kupingana au kuipinga Israel! Ni chambo tu! Hayo mambo ya haki za kuwepo kwao, sio la msingi kwa mataifa ya kiarabu!