Kitendo cha Museveni na Kagame kutokuja kumuaga hayati Rais Magufuli kinaashiria nini?

Hii stori yake naweza ipata wapi au unaweza nipa angalau kidogo
 
Tuwape Muda yawezekana watakuwepo tarehe 26/03/2021 kwenye safari ya mwisho ya kumpuzisha hayati Rais John Pombe Joseph Magufuli. Kwa mtazamo wangu kama wataenda chato itakuwa sawa kwa sababu Mkuu wetu wa nchi atakuwepo pia Chato ni sehemu ya Tanzania.
 
tusihukumu mazishi bado hayajafanyika...........huenda wamepanga kuja siku ya mazishi Chato.
 
Acha kihelehele ,ukihisi kuwashwa jikune kidogo.Msiba bado haujaisha na bado tuna siku 21 mbele wanaweza kuja siku yeyote hata baada ya kuzika huo ndio utamaduni wetu wa Afrika😂😂😂😂
 

Ni kitu gani kinakufanya udhani Rais Samia hakuwa MATAGA wakati yeye alikuwa no.2.
 
Sasa kama ni hivyo, si wangeweza kuja lakini wakakaa mbali wasisogelee karibu au wanasubiri azikwe ndipo waje? Hii sio sawa hata kidogo na sio afya kwa mustakabali wa EAC.
Mnazungumza as if Rwanda na Uganda hakuna COVID-19!!

M7 na PK wanajuwa vizuri jinsi ya kujikinga na maambukizi, binafsi naona kuto udhulia kwao msiba bila shaka walishauriana kwa kina na kufikia uhamuzi wa kutoshiriki kwenye msiba, tukiwekea maanani jinsi PK na M7 walivyo kuwa karibu sana na JPM lazima tutabaki tunajiuliza maswali mengi upande wetu labda kuna kitu hakikukaa sawa.
 
Kwani Magufuli amekwenda hata msiba mmoja wa viongozi wa nchi za Africa? Kama yeye aliona sawa kumpeleka Samia amwakilishe ni swa pia kwa Museveni na Kagame kutuma wawakilishi. Shida iko wapi?
 
Hii stori yake naweza ipata wapi au unaweza nipa angalau kidogo
911sep11 kaandika hivi "nine one one( emergence call)
Sep(september) eleven(siku ya shambulio) 911sep11"
Kwa maono yangu hapo kamaliza.

Kama unataka kujua historia ya shambulio la kigaidi lililotokea Marekani sep 11, google tu utapata historia yote. 911 ni namba ya simu ya Emergency, ukiwa marekani na kupatwa na janga la haraka (ugonjwa, moto au ugaidi) unapiga na wao hujua wakusaidie vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…