Mdau wa JamiiForums anaomba kufahamu kama kitendo cha mwanamke kujisaia wakati wa kujifungua huhusishwa na kushiriki tendo la ndoa kinyume cha maumbile.
Ameuliza swali hii baada ya kuwepo wa sintohamu kubwa miongoni mwa watu ambapo baadhi husema ni jambo la kawaida huku wengine wakipinga.
Ukweli wa jambo hili upoje?
Ameuliza swali hii baada ya kuwepo wa sintohamu kubwa miongoni mwa watu ambapo baadhi husema ni jambo la kawaida huku wengine wakipinga.
Ukweli wa jambo hili upoje?
- Tunachokijua
- Tangu kutungwa kwake, ujauzito wa kawaida hudumu kwa wastani wa siku 280, yaani wiki 40, hadi mwanamkr aweze kujifungua.
Kipindi hiki hutawaliwa na mabadiliko mengi ya kimwili na kihisia ambayo kwa pamoja hulenga kusaidia ukuaji mzuri wa mtoto tumboni pamoja na kudumisha afya njema ya mama.
Hata hivyo, kama inavyofahamika kwa watu wote, mwanamke hupaswa kupata uchungu wa uzazi ili kuihitimisha safari hii, tendo ambalo humtenganisha mama na mtoto ili aanze kujitegemea mwenyewe, kisha safari ya ukuaji wa mtoto nje ya mwili wa mama huendelea.
Kutoa haja kubwa wakati wa kujifungua
Hatua hili muhimu kwenye kuleta uhai mpya duniani hutawaliwa na misemo, nadharia na aina nyingi za uvumi zinazopaswa kujadiliwa kisahansi.
Mathalani ni ile nadharia inayosema kuwa mwanamke hapaswi kujisaidia haja kubwa wakati wa kujifungua, na akifanya hivyo humaanisha alishiriki tendo la ndoa kinyume cha maumbile.
Nadharia hii haina ukweli, ni imani potofu inayotweza utu wa mwanamke.
Uchungu wa kuzaa huambatana na hatua kuu tatu anazopitia mwanamke ambazo ni-
- Kufunguka na kupanuka kwa mlango wa kizazi
- Kutoka nje kwa mtoto
- Kusinyaa kwa mji wa uzazi na kutolewa nje kwa kondo la uzazi
Sio choo pekee, mwanamke anaweza pia kutoa haja ndogo pamoja na majimaji mengine yoyote yale yanayozalishwa mwilini mwake. Vyote hivi huwa havina ishara mbaya kwake.
Mgandamizo unaoongeza mijongeo ya misuli ya tumbo kuelekea sehemu ya chini ya nyonga inaweza pia kuchangiwa na mabadiliko ya homoni za mwili yanayotokea wakati wa uchungu pamoja na mkao wa mtoto tumboni.
Aidha, ni muhimu kufahamu kuwa misuli inayodhibiti mfumo wa chakula pamoja na ule wa uzazi hufanana hivyo ni ngumu kuzuia isiende sambamba
Ili kupunguza nafasi ya kutokea kwa hali hii, wanawake hushauriwa kunywa maji mengi kwenye hatua za mwisho wa ujauzito pamoja na kutumia vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi ili kurahisisha choo, tendo ambalo husaidia kusafisha utumbo mkubwa na kufanya usitunze choo kwa muda mrefu.
Ifahamike kuwa kitu pekee ambacho hukatazwa ni kitendo cha mwanamke kujisaidia kwenye tundu la choo kwa kuwa mtoto anaweza kudondokea humo na kupoteza maisha au kupata madhara makubwa kwenye afya yake.