Mbona Rais anapopeleka maendeleo sehemu mbalimbali huwa wanamsifia? amejenga zahanati, barabara, madarasa, sifa zote kwake..
Tena Ole Sendeka ndio huwa kinara wa kutoa hizo sifa.
Kwanini basi hizo pesa Rais anazopeleka kwenye hayo maendeleo zikipigwa asihusishwe? badala yake lawama waangushiwe watendaji tena kwa kunukuu ibara ya Katiba?!
Basi kama ndio hivyo, kuanzia leo wanapojenga barabara, shule, zahanati.. pongezi wapelekewe hao watendaji.
Lakini tofauti na hapo, Rais anahusika kwa yote hayo, Mwigulu yupo sahihi, ndio maana Rais amekuwa mpole kwa wapigaji, anawabembeleza waondoke wenyewe ofisini.