naungana na wewe! vipindi vingi sasa hivi vya TV vimeanza kukosa maadili, kama mamlaka husika haitochukua hatua zitasababisha mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa! jana nilijiuliza maswali mengi sana
1. Je kama mtu unaangalia kile kipindi na familia yako halafu mtoto mdogo akauliza kibamia ni nini? au kwanini wamevaa bamia?
2. Pili najiuliza tu je Kuwa na maumbile madogo ni hali ambayo mtu anajitakia au ni sababu za kimaumbile tu? kimtizamo wangu hii hali inatokana na maumbile ya mtu, na haipaswi kuchukuliwa kimzaa hivi! kama ni ugonjwa basi ni ugonjwa kama mwingine hauhitaji fufanyiwa mzaha kiasi hiki!
3. je hivi vituo vya luninga wanafanya uhakiki wa vipindi kabla havijarushwa hewani?