Uchaguzi 2020 Kitendo cha Tundu Lissu kukubalika Kanda ya Ziwa kwa kiwango hiki inaashiria nini?

Hata Buchosa ukiacha Shigongo kunyoa o hana hoja yoyote
 
kuna mtu kinamuuma sana!! yeye na watu wake hakutegema kabisa uchaguzi huu kuwa hivi.
 
Umesahau mafuriko ya lowasa au umekuwa janaa
 
Utasubiri sana mkuu labda 2035
 
Watasema wameibiwa kura baada ya kupigwa kipingo cha mbwa kokoko
 
Kawaida yenu kujitekenya na kucheka
 
Mnafeli hapo tu! Kumuita mtu au mtu kukusikiliza unacho muomba haimanishi kukubalia, muamuzi sanduku la kura
 

Kwa kuiba sawa na mmeshaonywa. Hebu jiulize unadhani amerejea nchini kifara?
 

Bora upinzani kuliko anaetaka kujiongezea utawala kwa kuvunja katiba.
Kiufupi ccm wengi hawamuungi jiwe na hao ndio watakao mpindua.

Unakumbuka kinana alivyosema wakati amealikwa aseme kwenye mkutano mkuu?
Alisema uchaguzi huu sio wa kubeza na hili ndilo kinalotokea.
Alafu CD ya kumpamba mzee imeshachujuka yaani
 
Hivi jamani na nyie mnafikiri geita kabisa geita wampigie Kura Tundu lissu half wamwache magu
Mbona kikwete mkazii wa ursino kinondoni alipata Kura 20 kwenye Jimbo la kawe 2015

Pale lugalo JWTz alipata % 30 ya kura za wajeda
 
Mkuu Ruttashobolwa , asante sana kwa kuwaeleza watu humu ukweli huu, japo watu humu watakubeza, lakini ukweli siku zote, una tabia moja, husimama mpaka mwisho.
Maadam tarehe 28 inakuja, tusiendelee kuandikia mate wakati wino upo!.

Ila pia kuna kitu umewasaidia hawa waota ndoto mchana bila wao kujijua, umewaokoa na kupata ugonjwa wa depression kutokana na too great expectations, kuwa mtu wao atashinda, hivyo ukweli kama huu unawasaidia kuwaandaa kisaikolojia kupokea kipigo cha mwaka, hivyo watakaposhindwa, wataishia kuumia tuu lakini hawata athirika kisaikolojia, na namna pekee ya kujifariji itakuwa ni kulia sana kwa kupiga makelele ili kuondoa machungu.

p
 
Huko Kanda ya ziwa si ndiko waliozulumiwa nyavu zao, watu wamelipishwa faini Hadi milioni 4 kwa kukutwa na vipande vya samaki, walikuwa wakiwategemea wacongo kuja kununua dagaa na samaki baada ya kuwashughulikia wafanyabiashara uchumi wa watu wa ziwani ukafa kibudu hivyo Wana hasira ya kumsomesha namba mtu October.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…