Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Ndani ya kipindi cha wiki tatu tu Tanzania tumeshuhudia vifo vya viongozi wawili wa kitaifa wakifariki wakati wakitibiwa kisiri huko India kinaashiria bado huduma zetu za kiafya hapa Tanzania ni duni, mbovu au haziaminiki na watanzania walio wengi wakiwemo viongozi wakubwa wa kitaifa.
Taifa lilipokea kwa mshtuko taarifa za kifo cha Laurence Mafuru na leo hii limepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Ndugulile ambaye alikuwa mbunge wa Kigamboni, na mkuu mteule wa shirika la afya duniani (WHO) ukanda wa Afrika.
Katika hali ya kawaida, kwa nafasi walizokuwa nazo wahusika maana yake serikali ilikuwa ikigharamia matibabu yao kwa kipindi chote cha ugonjwa, kifo na kurejeshwa nchini miili yao kwa taratibu za maziko. Na kwa misingi hiyo, serikali ilitoa kibali cha wao kwenda India kutibiwa kwa kuwa huduma za kiafya hapa nchini hazikuwa zinakidhi viwango vya wahusika kupona au kupata nafuu.
Ikiwa, mbunge mwandamizi wa CCM, naibu waziri wa afya mstaafu, mkuu mteule wa kitengo cha afya cha umoja wa mataifa (WHO) ukanda wa Afrika, anaweza kuugua na kukimbilia India kutibiwa huku akikacha kutibiwa kwenye hospitali ya Muhimbili, Bugando, KCMC, Benjamin Mkapa, Aga Khan nk, hiyo inatoa taswira kamili kuwa kwenye ubora wa utoaji wa huduma za Afya Tanzania bado sana.
Siku ukiona viongozi wetu hawaendi tena India kutibiwa, na wanaugua mpaka kupona au kufariki hapa hapa Tanzania hapo ndipo tutatambua ubora wa huduma za afya zitolewazo hapa nchini.