Kitendo cha wachezaji wa yanga kumpiga refa hakikubaliki

Kitendo cha wachezaji wa yanga kumpiga refa hakikubaliki

Kwa nini Mwasika wamemfungia mwaka 1 af Cannavaro mechi 6?! Kwani aliyempiga refa alikuwa nani?
 
ni kweli sometimes marefa wanachangia kwa kiasi kikubwa iwe makusudi/kupanga au kutokusudia kuamsha hasira za wachezaji kutokana na maamuzi mabovu au yenye utata ila kwa wachezaji wa ligi kuu kwa hapa bongo kwa level yao hawakustahili kufanya walichokifanya ni aibu kwao,klabu na taifa kwa ujumla baadhi yao ndo tunategeme wajekua profesional kweli,haya sasa wameshaicost team inayowalipa mishahara and benefits
 
Sababu ya kufungiwa ni nn? Then kumfungia mtu mwaka mzima ni kuuwa kiwango au kurekebisha?

kama hujui kilichotokea inaelekea wewe siyo mfatiliaji wa soka la bongo...kifupi ni kwamba wachezaji wa yanga walimtwanga mwamzi aliechezesha pambano lao kati ya yanga na azam wakipinga niyonzima kupewa kadi mbili za njano ikifatiwa na nyekudu wakidai ameonewa hivyo kuamua kurushia mknd yaliopta ipatavyo
 
Hio adhabu mbona wametoa kubwa hivo?

ungeona refa walivyo mtwanga makonde wala usingesema unacho kisema kwanza mimi nashanga wamepewa adhabu ndogo sana labda ni mmoja tu ndiyo katendewa haki ambae ni mwasika...
 
TFF imemfungia mwaka 1 mchezaji wa yanga stephano mwasika,pia mechi sita kwa canavaro,na Tegete,pia mechi 3 kwa nurdin bakari,na omega seme na YANGA kupigwa faini ya milioni 4.5 kutokana na vurugu kati ya mechi ya yanga na Azam

Refa je aliye sababisha vurugu hizo kapewa adhabu gani?
 
Kwa kitendo walichofanya, nadhani adhabu hiyo ni ndogo, viwanja vya mpira sio sehemu ya masumbwi-kama ni masumbwi ni bora wakajiunge na kina Matumla

pamoja sana mkuu mimi nilitegemea adhabu ndogo kabisa ingekuwa miezi 3 matokeo yake eti mechi tatu sijui sita tff wameonyesha kuwaonea huruma yanga lakini na kuhakiiikm angekuwa w chezaji wasimba mbaya zaidi iwe haruna moshi angefungiwa hata maisha...
 
Na-support adhabu hiyo. Kwa karne hii, nilisikitishwa na kitendo cha wachezaji wa Yanga kumpiga refa. Kama refa alikosea ilifaa walalamike TFF, sio kuchukua sheria mkononi
 
TFF sijui wametumia vigezo gani kuwafungia mechi 3 na mechi 6 watu waliorusha makonde kwa mwamuzi...
 
yanga2.jpg
Isreal Mujuni Nkongo akipata 'kipigo' toka kwa wachezaji/mchezaji wa Yanga
 
Na-support adhabu hiyo. Kwa karne hii, nilisikitishwa na kitendo cha wachezaji wa Yanga kumpiga refa. Kama refa alikosea ilifaa walalamike TFF, sio kuchukua sheria mkononi
Huoni kama ni ndogo sana hasa kwa wazezaji waliofungiwa mechi 3 na 6.....
 
Dah wachezaji wamenisikitisha sana hawa. Adhabu iendane na kosa wasilete usimba
 
Nidhamu ni kitu muhimu sana ambacho waafrika wengi tunakichukulia kirahisi rahisi. Kuanzia kwenye mambo yetu wenyewe na yale ya kijamii, tukikosa nidhamu hakuna lolote tutakalofaanikiwa.
 
Back
Top Bottom