Alipewa hela baada ya mchezo (baada ya 'kupendelea') au kabla ya mchezo (ili apendelee)? Anyway, hilo la kupewa pesa tuliweke kando (nikiamini huna ushahidi wowote).
Labda katika hili la kupendelea Azam (ambalo kwa hoja yako pengine linatokaba na kupewa hela), ni maamuzi gani aliyafanya ambayo unadhani aliwapendelea Azam to the detriment of Yanga? Bila kuwa specific inakuwa ngumu sana kwa 'sweeping allegations' kama hizi kukubaliwa na watu wasioegamia upande wowote. Nilimsikia jana kiongozi wa yanga akisema wamekata rufaa kuhusu mchezo wao na Azam lakini alipoulizwa basis ya rufaa yao akakataa kusema! Sasa kuwa na viongozi kama hawa katika vilabu vya soka ni tatizo!