Kitendo cha wachezaji wa yanga kumpiga refa hakikubaliki

Kitendo cha wachezaji wa yanga kumpiga refa hakikubaliki

Acha habari za kusikia na kuzi'publish with confidence "eti walimpiga mtoto hadi akafariki" mtoto wa nani mkeo? ukiitwa leo Polisi ukasaidie Polisi katika hilo suala utaenda? jamani Watanzania tusiwe tunapenda kuropokaropoka bila mpangilio maalum,tutaumia!

huo ulikua ni uongo mkubwa hamna k2 kama hicho
 
Mkuu Yanga bado wana nafasi, Yanga wamesajili wachezaji zaidi ya 25, hivyo kufungiwa hao watano pamoja na kwamba ni wa kikosi cha kwanza lakini bado waliopo wanaweza kuonyesha upinzani na hadi kuchukua ubingwa.
Tusubiri tuone, but naona Tegete na canavaro ni tegemeo kubwa sana kwa yanga. kukosekana kwao lazima kutakuwa na madhara kwenye timu
 
Mkuu ufanisi mbovu wa Takukuru mbadala wake sio wachezaji kumpiga refa, hiyo mimi napinga hata kama ingekuwa ni timu yangu ya Simba ndo wamefanya huo upuuzi bado ningepinga na ningeunga mkono adhabu ambayo wangepata, Tanzania kila taasisi inalalamikiwa kwa hiyo badala yake iwe ni kutwangana tu; jamani acheni kuwatetea wachezaji waliofanya hivyo vitendo, wamevuna walichopanda.

Naona kama umeamua kutoelewa hoja yangu kwa makusudi. Tangu awali nimepinga kitendo cha wachezaji kujichukulia sheria mikononi.
Nilipoizungumzia takukuru nilikuwa najibu hoja yako ya kutaka wapelekewe ushahidi wakati ukijua hawana ufanisi wowote.
Hapa nilitaka tutafakari njia nyengine za kukabiliana na tuhuma za rushwa katika ligi zetu.
 
Kuna mkono wa aliyepakatwa hapo, itakuwaje refa aachwe? Yeye ndo chanzo,we big match kama ile unampa kadi nyekundu mchezaji ambaye ni injini ya mchezo,tena dakika za awali, huyu refa tena wacha niongekee kikurya ,"alikuwa anabhikiri bhizuri mura?'
 
Tusubiri tuone, but naona Tegete na canavaro ni tegemeo kubwa sana kwa yanga. kukosekana kwao lazima kutakuwa na madhara kwenye timu

hapana wachezaj wa muhimu pale ni kanavaro na nurdin bakari.TEGETE MSIMU HANA NAMBA,MWASKA YUPO OSCAR JOSHUA,OMEGA SEME HANA NAMBA
 
Pamoja na kwamba siungi mkono kitendo cha wachezaji kumshambulia mwamuzi lakini kadi nyekundu aliyopewa niyonzima haikustahili, mwamuzi angeweza kumuonya kwa mdomo tu na yakaisha, ....
Nadhani suala la msingi hapo ni je kuna kosa lilitendeka kwa mujibu wa sheria/kanuni za soka...kama jibu ni ndiyo....je sheria zinasemaje juu ya kosa hilo? Mimi sikuangalia mechi hiyo...hebu niambie Niyonzima alifanya nini mpaka astahili kuonywa na kwa kanuni ipi? Sasa kama kanuni zinataka kuonya na referee akatoa redcard hapo ni sawa mwamuzi amekosea na adhabu yake naamini inaainishwa na kanuni na taratibu na siyo wachezaji kumshambulia (angalau tunakubaliana katika hili la kumshambulia mwamuzi kukosa uhalali wowote!)

Tukifika mahali tunataka refa asikilize maneno ya mitaani na kufanya maamuzi uwanjani kwa kuzingatia maneno ya mitaani, then hakuna maana ya kuwa na sheria/kanuni. Hata hao TFF kama tunategemea wafanye maamuzi kwa kusikiliza uvumi (bila kuwepo ushahidi angalau hata wa kimazingira) wanaweza kujikuta wanashindwa kuweka mwamuzi atakayekubalika na pande zote maana kila atakayewekwa mtu/timu yoyote kwa maslahi yake anaweza kuzusha lolote kuhusu refa huyo!

Obviously, maamuzi ya refa hayawezi kuzipendeza pande zote kwa wakati mmoja na kila wakati...mara nyingi kunakuwa na grivances...sasa hatua gani mchezaji/timu inachukuwa kama haikubaliani na maamuzi ya refa hapo ndio suala la professionalism linaingia.
 
Kuna mkono wa aliyepakatwa hapo, itakuwaje refa aachwe? Yeye ndo chanzo,we big match kama ile unampa kadi nyekundu mchezaji ambaye ni injini ya mchezo,tena dakika za awali, huyu refa tena wacha niongekee kikurya ,"alikuwa anabhikiri bhizuri mura?'

alichofanya refa nikuwanyongonyeza key players wa yanga kama haruna tena dk za mwanzo
 
Tusubiri tuone, but naona Tegete na canavaro ni tegemeo kubwa sana kwa yanga. kukosekana kwao lazima kutakuwa na madhara kwenye timu
Labda Canavaro lakini Tegete kwa msimu huu sio tegemeo sana.
 
Wangefungiwa maisha, iwe fundisho kwa wengine, hii adhabu ni ndogo sana, ndio maana hatuendelei kimichezo kwa sababu nidhamu hatuna.

Kakate rufaa TFF sasa kama haujaridhika na hukumu yao!Muone kwanza ulivyofanana na mwenyekiti wenu yule msomali poli!!Yanga next level,tuacheni na yanga yetu jamani!!
 
Hii yanga kazi kututia aibu 2 kama taifa,wawaache azam msimu ujao wa2wakilishe 2.kila cku kuishia round ya kwnza ndo nini..
 
Hakuna mchezaji aliyeongezewa adhabu, ukweli ni kwamba adhabu ya Tegete ni miezi 6 tangu awali, hakuna kikao kingine kilichokaa kuhusu swala lile, hili ndio tatizo la waandishi makanjanja wa Tanzania badala ya kudeal na ofisa habari wa TFF wao wanaokoteza habari barabarani hili waonekane wako up to date kumbe makanjanja watupu, pumbavu kabisa.
Labda nikupe changamoto wewe mdau uliyeleta habari hii unaweza kutupa reliable source of news!!??
 
Kama ushahidi upo kwamba alipokea hela lazima naye atapata kipande chake, lakini kama ni tetesi tu zitabakia kuwa tetesi tu mpaka zitakapothibitishwa, jamani twende mbele turudi nyuma; kabla ya mechi ya jmosi Azam alishawafunga Yanga mechi tatu hizo nazo walitoa hela? Lawama zipelekeni kwa viongozi na wachezaji kwa kulishana sumu na kufanya matendo yasio kuwa ya kianamichezo, mie nlikuwepo uwanjani kadi zote hizo Niyonzima alistahili, nakumbuka kuna mechi ya Simba na Yanga Mrwanda alipata red mazingira kama yale ya aliyopata red Niyonzima, kwa hiyo mimi nasema bado Niyonzima alistahili alichopata ndo maana kwa kutambua hivyo kawaomba radhi wanachama, washabiki wa Yanga na wapenzi wa mpira kwa ujumla na kama ameonewa kwa nini aombe radhi?
Kweli nawe unauonyesha ukilaza wako,kwa hyo Niyonzima kuomba msamaha kwako unadhani alifanya kosa? tulia wanaojua taratibu wachangie
 
Hii yanga kazi kututia aibu 2 kama taifa,wawaache azam msimu ujao wa2wakilishe 2.kila cku kuishia round ya kwnza ndo nini..
Off course mimi ni Yanga moderate fan, naunga mkono hoja yako kwa 100%
 
Kwa hiyo wakati Yanga wanawafunga Azam nao walikuwa wanatoa hela, hapo ni wakati wa Manji, kibao kimegeuka mkajua mpango ni ule ule.

Na kuhusu Niyonzima kama kaonewa kwa nini aombe radhi, anajikosha tu anajua alichofanya ni kosa, gesture yoyote ni yellow kadi.

Kuhusu nidhamu naunga mkono, nidhamu ni kitu cha maana sana kwa wanadamu, kwenye nidhamu kuna ustaarabu na kuheshimiana. Lakini mambo ya Ndondi na soka wapi na wapi?

hapanà, mbona azam wamewafunga yanga mara 3 mwaka huu,mbona hii game ya 4 ndo wame mind? Azam walimpa pesa refa OVER
 
hivi kwa kosa hili kwa nini wasiifute yanga kwenye ligi kabisa ili iwe fundisho kwa timu zingine zenye tabia kama hii ya yanga
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mkuu hata habari zingezagaa kwamba wachezaji wa Yanga wamempiga refa bila kuwa na ushahidi wowote wasingepewa adhabu, kwa hiyo wewe unayetaka tuamini hizo tetesi zako peleka hizo taarifa Takukuru maana hiyo ni rushwa na naamini watazifanyia kazi na sio kulalama tu mbona refa hajaadhibiwa, aadhibiwe kwa kosa gani alilofanya?

kuwa nyong'onyeza yanga kwa kuwapa red card key players ulikua ni mchongo
 
Back
Top Bottom