Mimi ni shabiki mkubwa sana wa Yanga.....Pamoja na kuwa shabiki mkubwa wa Yanga sikupendezwa(hata kidogo) na hatua iliyochukuliwa na wachezaji wakubwa na wenye heshima katika soka la nchi hii kama Nadir Haroub, Nurudin Bakari, Jerry Tegete na Stephano Mwasyika cha kumpiga muamuzi Israel NKONGO...Hii ni aibu na fedheha kubwa sana kwa Yanga, TFF na Taifa kwa ujumla.....Katika hili naulalamikia zaidi uongozi wa Yanga kwa kuwaaminisha(tangu siku moja kabla ya mechi) wachezaji kwamba Azam wamemhonga muamuzi hivyo wategemee kushindwa katika mechi hiyo,hali hii iliwafanya wachezaji wa Yanga waingie uwanjani wakijua kwamba panga pangua siku hiyo lazima muamuzi awamalize kwa kuwapendelea Azam,na hili ndilo lilipelekea Haruna Niyonzima(mara kwa mara) kumlalamikia Refa kwa kumfokea kila wakati alipoonekana akifanya maamuzi ya kuikandamiza Yanga......Ningekuwa na uwezo ningewawajibisha viongozi hawa kwa kuanzia na Mwenyekiti Nchunga, Katibu Mwesigwa na Afisa Habari Sendeu kwani kauli zao ndizo zilipelekea mechi hiyo kuharibika kwani ziliwasukuma wachezaji kumpiga muamuzi.....
Lawama zangu pia namtupia muamuzi Israel NKONGO......Kwa hali ilivyokuwa kutokana na 'tension' ya mchezo na hali ya kisaikolojia ya wachezaji wa Yanga ambao tangu wakati wa 'pre match meeting' viongozi wao walionekana kutokuwa na imani na muamuzi huyo,alipaswa kutumia busara katika kumuadhibu Haruna Niyonzima......Sidhani kama kulikuwa na ulazima wa kumpa Niyonzima kadi nyekundu kutokana na aina ya kosa alilofanya....Kila mtu anaelewa kwamba kwa sasa Haruna Niyonzima na Juma Seif 'Kijiko' ndiyo injini ya Yanga.....Kumtoa mmojawapo kwa kadi nyekundu kama ile aliyopewa Haruna ni kuidhoofisha timu....Halii hii ndiyo iliwafanya wachezaji wa Yanga kumvamia muamuzi kwani hapa walithibitisha HISIA zao na TETESI zilizokuwapo mtaani kwamba muamuzi huyo amehongwa na Azam FC.......
Kuna haja sasa kwa TFF kuunda Kamati itakayoshughulillka na uchunguzi wa tuhuma za Rushwa dhidi ya waamuzi, wachezaji na viongozi wa soka,ikiwezekana wawashirikishe TAKUKURU katika kushughulikia tuhuma zote za rushwa zinazowahusu waamuzi,wachezaji na viongozi wa soka kama ilivyofanya kwa kesi ya ULIMBOKA MWAKINGWE na SHAABAN KADO......TFF wanapaswa kuwachunguza Azam maana kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikiwa/wakituhumiwa kujihusisha na Rushwa kwa waamuzi ili wawapendelee wanapokuwa uwanjani.......
Pia TFF waangalie mfumo wao wa kutoa adhabu kwa wachezaji na waamuzi.....Huu utaratibu wa kumfungia mchezaji ama muamuzi mwaka mmoja,miezi sita ama miezi mitatu si mzuri hata kidogo...Ni kweli wachezaji wanakosa nidhamu katika mchezo kiasi cha kufanya vitendo kama vile vilivyofanywa na wachezaji wa Yanga,lakini kuwafungia mwaka mmoja ama miezi sita si HAKI hata kidogo....Ni kuwaonea....Ikumbukwe mpira ndio AJIRA ya hawa vijana.......ni vema waweke hata utaratibu wa kuwafungia mechi kama inayofanyika katika ligi kubwa barani Ulaya,Amerika,Asia na Afrika(mfano unamfungia anakosa mechi moja, mechi mbili, mechi tatu,mechi tano au hata mechi nane kama ilivyokuwa kwa Louis Suarez)....Pia vilabu vipate nafasi ya kuwaadhibu wachezaji wao kwa kuwakata mishahara na ikiwezekana wachezaji wanaowapiga marefa wafunguliwe mashitaka ya jinai.....Kazi ya kuwahukumu wachezaji wanaowapiga marefa ifanywe na Mahakama na si TFF...TFF wao wawafungie mechi tu na si vinginevyo......
Kwa Azam na mtani wangu Ndetichia.......Kama ni kweli wana tabia hii ya kuwahonga waamuzi waiache mara moja kwani haitawafikisha popote.....Waangalie yasije yakawakuta kama yaliyowakuta Juventus kule Serie A......Kuwahonga waamuzi/wachezaji kwa lengo la kupanga matokeo ni SUMU kubwa na mbaya sana kwa maendeleo ya soka letu ambalo kadiri siku zinzvyosonga mbele limekuwa likiporomoka(kwa kiwango) kwa kasi ya ajabu sana.......Wabadilike
Pamoja na matokeo hayo ya juzi Yanga bado wana nafasi kubwa sana ya kuutwaa Ubingwa huu(maana hao Azam wana mechi 2 zaidi ya Yanga na Simba wana mechi 1 zaidi ya Yanga)........Ni matumani yangu kwamba kufungiwa kwa wachezaji hao kutatoa nafasi kwa Pius Kisambale, Oscar Joshua, Godfrey Bonny(Papic anambania sana mtaalamu wangu huyu), Bakari Mbegu, Chacha Marwa na wengine kuonesha uwzo/vipaji vyao.....
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo sasa.....
Bala.