Kitendo cha wachezaji wa yanga kumpiga refa hakikubaliki

Kitendo cha wachezaji wa yanga kumpiga refa hakikubaliki

Kama ushahidi upo kwamba alipokea hela lazima naye atapata kipande chake, lakini kama ni tetesi tu zitabakia kuwa tetesi tu mpaka zitakapothibitishwa, jamani twende mbele turudi nyuma; kabla ya mechi ya jmosi Azam alishawafunga Yanga mechi tatu hizo nazo walitoa hela? Lawama zipelekeni kwa viongozi na wachezaji kwa kulishana sumu na kufanya matendo yasio kuwa ya kianamichezo, mie nlikuwepo uwanjani kadi zote hizo Niyonzima alistahili, nakumbuka kuna mechi ya Simba na Yanga Mrwanda alipata red mazingira kama yale ya aliyopata red Niyonzima, kwa hiyo mimi nasema bado Niyonzima alistahili alichopata ndo maana kwa kutambua hivyo kawaomba radhi wanachama, washabiki wa Yanga na wapenzi wa mpira kwa ujumla na kama ameonewa kwa nini aombe radhi?

red card aliyopewa mrwanda game ya simba+yanga ilikua halali coz ilikua dk ya 78 na alifanya makosa kibao,kwa haruna anamuonea sana na alijua haruna ndiyo injini ya yanga hakukua na fair
 
hivi kwa kosa hili kwa nini wasiifute yanga kwenye ligi kabisa ili iwe fundisho kwa timu zingine zenye tabia kama hii ya yanga
No. Adhabu ya fine inawatosha na hata ukiingalia sana adhabu hiyo sio ya haki kivile kwa sababu hakuna ushahidi wowote kuwa walipewa maelekezo na club kufanya makosa waliyoyafanya uwanjani. Yanga kama timu kiuhalisia haikuwa na namna ya kuzuia makosa waliyofanya wachezaji wake.
 
Kweli nawe unauonyesha ukilaza wako,kwa hyo Niyonzima kuomba msamaha kwako unadhani alifanya kosa? tulia wanaojua taratibu wachangie
Kama na wewe unaomba radhi bila kufanya kosa basi utakuwa umechanganyikiwa.
 
Hakuna mchezaji aliyeongezewa adhabu, ukweli ni kwamba adhabu ya Tegete ni miezi 6 tangu awali, hakuna kikao kingine kilichokaa kuhusu swala lile, hili ndio tatizo la waandishi makanjanja wa Tanzania badala ya kudeal na ofisa habari wa TFF wao wanaokoteza habari barabarani hili waonekane wako up to date kumbe makanjanja watupu, pumbavu kabisa.
Labda nikupe changamoto wewe mdau uliyeleta habari hii unaweza kutupa reliable source of news!!??

mdau nimepata information toka blog ya shaffih dauda
 
No. Adhabu ya fane inawatosha na hata ukiingalia sana adhabu hiyo sio ya haki kivile kwa sababu hakuna ushahidi wowote kuwa walipewa maelekezo na club kufanya makosa waliyoyafanya uwanjani. Yanga kama timu kiuhalisia haikuwa na namna ya kuzuia makosa waliyofanya wachezaji wake.
Huna sababu ya kumjibu mtu ambaye amefunikwa na kilemba cha ushabiki wa kijinga, yeye hajui kwamba Simba ilitaka kushuka daraja ilibidi FAT, YANGA na SIMBA waclose dill kwamba meChi ya mwisho ni lazima Yanga ifungwe ili kuinusuru Simba isishuke daraja, maana uchumi wa FAT unategemea klabu hizo.
Nadhani haya ni matatizo ya mashabiki waliokuja mjini na magari ya ziara.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
red card aliyopewa mrwanda game ya simba+yanga ilikua halali coz ilikua dk ya 78 na alifanya makosa kibao,kwa haruna anamuonea sana na alijua haruna ndiyo injini ya yanga hakukua na fair
Haitegemei ni dakika ya ngapi ya mchezo ndo mchezaji apate card, iwe ni dakika ya kwanza ya 45, ya 90 au ya 120 au hata baada ya mechi ili mradi tu mchezaji kafanya kosa basi anastahili adhabu.
 
mdau nimepata information toka blog ya shaffih dauda
Bloger anaweza kupost chochote hata akiwa Break Point Bar anakunywa pombe, TFF ina msemaje wake na wanahabari wote wanapaswa kupata habari za TFF kupitia kwa msemaji rasmi wa TFF na sio kupigiana simu na baadhi ya wajumbe wa kamati. huu ni uswahili na ukanjanja.
 
Hakuna mchezaji aliyeongezewa adhabu, ukweli ni kwamba adhabu ya Tegete ni miezi 6 tangu awali, hakuna kikao kingine kilichokaa kuhusu swala lile, hili ndio tatizo la waandishi makanjanja wa Tanzania badala ya kudeal na ofisa habari wa TFF wao wanaokoteza habari barabarani hili waonekane wako up to date kumbe makanjanja watupu, pumbavu kabisa.
Labda nikupe changamoto wewe mdau uliyeleta habari hii unaweza kutupa reliable source of news!!??

Wewe mwenyewe unaweza ukawa "Mkanjanja" ksbb Tegete hajafungiwa miezi 6,amefungiwa mechi 6 tu Kiongozi
 
Wewe mwenyewe unaweza ukawa "Mkanjanja" ksbb Tegete hajafungiwa miezi 6,amefungiwa mechi 6 tu Kiongozi
Kama wewe ni Yanga mwenzangu nakupa pole sana, soon utaupata ukweli tena leo hii na ni hapa hapa kupitia thread hii, its just a matter of time wait n see!......
 
Bloger anaweza kupost chochote hata akiwa Break Point Bar anakunywa pombe, TFF ina msemaje wake na wanahabari wote wanapaswa kupata habari za TFF kupitia kwa msemaji rasmi wa TFF na sio kupigiana simu na baadhi ya wajumbe wa kamati. huu ni uswahili na ukanjanja.

wao kama redio wamepata habari TFF leo asubui ndo jamaa aka2pia kwenye blog yake
 
Huna sababu ya kumjibu mtu ambaye amefunikwa na kilemba cha ushabiki wa kijinga, yeye hajui kwamba Simba ilitaka kushuka daraja ilibidi FAT, YANGA na SIMBA waclose dill kwamba meChi ya mwisho ni lazima Yanga ifungwe ili kuinusuru Simba isishuke daraja, maana uchumi wa FAT unategemea klabu hizo.
Nadhani haya ni matatizo ya mashabiki waliokuja mjini na magari ya ziara.

m2 kama huyo ambaye hajui historia ya yanga+simba+FAT Kuhusu simba kushuka daraja usibishane nae mkuu
 
Haitegemei ni dakika ya ngapi ya mchezo ndo mchezaji apate card, iwe ni dakika ya kwanza ya 45, ya 90 au ya 120 au hata baada ya mechi ili mradi tu mchezaji kafanya kosa basi anastahili adhabu.

cjasema muda flan ndo m2 apewe kad nilichokua nataka ujue kuwa na ushaid wa mrwanda na ile red kwamba ilikua halali lakini ya haruna ni magumashi alimtoa kwenye mood then akampiga red kad nyepesi kabisa duniani
 
Mimi ni shabiki mkubwa sana wa Yanga.....Pamoja na kuwa shabiki mkubwa wa Yanga sikupendezwa(hata kidogo) na hatua iliyochukuliwa na wachezaji wakubwa na wenye heshima katika soka la nchi hii kama Nadir Haroub, Nurudin Bakari, Jerry Tegete na Stephano Mwasyika cha kumpiga muamuzi Israel NKONGO...Hii ni aibu na fedheha kubwa sana kwa Yanga, TFF na Taifa kwa ujumla.....Katika hili naulalamikia zaidi uongozi wa Yanga kwa kuwaaminisha(tangu siku moja kabla ya mechi) wachezaji kwamba Azam wamemhonga muamuzi hivyo wategemee kushindwa katika mechi hiyo,hali hii iliwafanya wachezaji wa Yanga waingie uwanjani wakijua kwamba panga pangua siku hiyo lazima muamuzi awamalize kwa kuwapendelea Azam,na hili ndilo lilipelekea Haruna Niyonzima(mara kwa mara) kumlalamikia Refa kwa kumfokea kila wakati alipoonekana akifanya maamuzi ya kuikandamiza Yanga......Ningekuwa na uwezo ningewawajibisha viongozi hawa kwa kuanzia na Mwenyekiti Nchunga, Katibu Mwesigwa na Afisa Habari Sendeu kwani kauli zao ndizo zilipelekea mechi hiyo kuharibika kwani ziliwasukuma wachezaji kumpiga muamuzi.....

Lawama zangu pia namtupia muamuzi Israel NKONGO......Kwa hali ilivyokuwa kutokana na 'tension' ya mchezo na hali ya kisaikolojia ya wachezaji wa Yanga ambao tangu wakati wa 'pre match meeting' viongozi wao walionekana kutokuwa na imani na muamuzi huyo,alipaswa kutumia busara katika kumuadhibu Haruna Niyonzima......Sidhani kama kulikuwa na ulazima wa kumpa Niyonzima kadi nyekundu kutokana na aina ya kosa alilofanya....Kila mtu anaelewa kwamba kwa sasa Haruna Niyonzima na Juma Seif 'Kijiko' ndiyo injini ya Yanga.....Kumtoa mmojawapo kwa kadi nyekundu kama ile aliyopewa Haruna ni kuidhoofisha timu....Halii hii ndiyo iliwafanya wachezaji wa Yanga kumvamia muamuzi kwani hapa walithibitisha HISIA zao na TETESI zilizokuwapo mtaani kwamba muamuzi huyo amehongwa na Azam FC.......

Kuna haja sasa kwa TFF kuunda Kamati itakayoshughulillka na uchunguzi wa tuhuma za Rushwa dhidi ya waamuzi, wachezaji na viongozi wa soka,ikiwezekana wawashirikishe TAKUKURU katika kushughulikia tuhuma zote za rushwa zinazowahusu waamuzi,wachezaji na viongozi wa soka kama ilivyofanya kwa kesi ya ULIMBOKA MWAKINGWE na SHAABAN KADO......TFF wanapaswa kuwachunguza Azam maana kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikiwa/wakituhumiwa kujihusisha na Rushwa kwa waamuzi ili wawapendelee wanapokuwa uwanjani.......

Pia TFF waangalie mfumo wao wa kutoa adhabu kwa wachezaji na waamuzi.....Huu utaratibu wa kumfungia mchezaji ama muamuzi mwaka mmoja,miezi sita ama miezi mitatu si mzuri hata kidogo...Ni kweli wachezaji wanakosa nidhamu katika mchezo kiasi cha kufanya vitendo kama vile vilivyofanywa na wachezaji wa Yanga,lakini kuwafungia mwaka mmoja ama miezi sita si HAKI hata kidogo....Ni kuwaonea....Ikumbukwe mpira ndio AJIRA ya hawa vijana.......ni vema waweke hata utaratibu wa kuwafungia mechi kama inayofanyika katika ligi kubwa barani Ulaya,Amerika,Asia na Afrika(mfano unamfungia anakosa mechi moja, mechi mbili, mechi tatu,mechi tano au hata mechi nane kama ilivyokuwa kwa Louis Suarez)....Pia vilabu vipate nafasi ya kuwaadhibu wachezaji wao kwa kuwakata mishahara na ikiwezekana wachezaji wanaowapiga marefa wafunguliwe mashitaka ya jinai.....Kazi ya kuwahukumu wachezaji wanaowapiga marefa ifanywe na Mahakama na si TFF...TFF wao wawafungie mechi tu na si vinginevyo......

Kwa Azam na mtani wangu Ndetichia.......Kama ni kweli wana tabia hii ya kuwahonga waamuzi waiache mara moja kwani haitawafikisha popote.....Waangalie yasije yakawakuta kama yaliyowakuta Juventus kule Serie A......Kuwahonga waamuzi/wachezaji kwa lengo la kupanga matokeo ni SUMU kubwa na mbaya sana kwa maendeleo ya soka letu ambalo kadiri siku zinzvyosonga mbele limekuwa likiporomoka(kwa kiwango) kwa kasi ya ajabu sana.......Wabadilike

Pamoja na matokeo hayo ya juzi Yanga bado wana nafasi kubwa sana ya kuutwaa Ubingwa huu(maana hao Azam wana mechi 2 zaidi ya Yanga na Simba wana mechi 1 zaidi ya Yanga)........Ni matumani yangu kwamba kufungiwa kwa wachezaji hao kutatoa nafasi kwa Pius Kisambale, Oscar Joshua, Godfrey Bonny(Papic anambania sana mtaalamu wangu huyu), Bakari Mbegu, Chacha Marwa na wengine kuonesha uwzo/vipaji vyao.....

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo sasa.....

Bala.
 
Masikini Nsajigwa kamshika Canavarro huku wengine wanashambulia!

Kwakweli timu yetu ya yanga imetufedhehesha sana, hata refa akiwa vipi hutakiwi kwenda kumpa kichapo.
 
Balantanda,

Kule nje wanawafungia wachezaji mechi chache kwa makosa ya kawaida ya kimchezo. Lakini ukimvamia refa ukamtandika ngumi au kumkwida aisee unaweza kula ban ya life!
 
Balantanda,

Kule nje wanawafungia wachezaji mechi chache kwa makosa ya kawaida ya kimchezo. Lakini ukimvamia refa ukamtandika ngumi au kumkwida aisee unaweza kula ban ya life!
Hebu nipe mfano wa mchezaji aliyepata life ban kuwa kumdunda muamuzi/mchezaji mwenzake....
 
Hebu nipe mfano wa mchezaji aliyepata life ban kuwa kumdunda muamuzi/mchezaji mwenzake....

Mtani pole........hakuna life ban bana.....lengthy bans sawa.....kama huyu

article-1388957-0012022000000258-420_306x423.jpg

plgoldfunny2.jpg
 
Back
Top Bottom