Kitendo cha wachezaji wa yanga kumpiga refa hakikubaliki

Kitendo cha wachezaji wa yanga kumpiga refa hakikubaliki

Bala,waambie hao kuwa msimu uliopita tulichukua kombe siku ya mwisho,wameshangilia Yanga kufungwa na Azam halafu wameshindwa kumfunga Toto

shauri yao na hawajui wametuzid game 1 na huyo azam wanayemsifia ka2zid game 2?
 
Ni kweli kwamba wachezaji wa Yanga wanastahili kufungiwa kwa makosa waliyofanya,cha ajabu yule refa alipigwa na Mwasika lakini hakumpa kadi,kwa nini refa naye hajapewa adhabu?

makosa ya kiutendaji tu,hata canavaro anastail red coz alianzisha vurugu
 
Acha ushabiki mkuu......Yanga tayari wana timu ya ngumi kama ilivyo kwa Simba......

Kumbuka kwamba unawazungumzia mabingwa hapa... Yanga ndio mabingwa wa Tanzania na Afrika Mashariki na kati.....Simba mna kombe gani?......

Msimamo wa Ligi unaonesha kwamba Yanga wanshika nafasi ya 3 na wakishinda mechi ya kesho watapanda hadi nafasi ya pili.....Azam wanawazidi Yanga mechi mbili na Simba wanawazi Yanga mechi moja.....Yanga bado wana nafasi kubwa sana ya kutwaa Ubingwa wa Tanzania.......Kubali kataa.......Hutaki Unaacha......

Bala.

umesahau bingwa wa tusker 2liomfunga sofapaka
 
I see...umenikumbusha karibuni niliambiwa hivo...'no publicity is bad publicity'

But I am still wondering hw can this help 'Yanga'
 
kwa hii adhabu nahisi JOSHUA KAMPIGA MSUMARI MWASIKA KAMA KADO ALIVYOMTWANGA MWENZIE BERKO KILA HOSPITAL AWAONI TATIZO ...NA SRC YA BERKO NI UPUUZI WA JUMA KASEJA NDIE ALIMWEKEZAA KADO JINSI YA KUMSHUGULIKIA BERKOMASKINI ANATAMANI AOMBE LIKIZO LOH MTAPIGANA MSUMARI MPAKA MWISHO BONGO YETU

imani tu
 
Mtani.........

Najua haupo serious......

Yaani Yanga ishindwe kuchukua ubingwa wala kushika nafasi ya 3 kwa wachezaji wa 5 kufungiwa/kusimamishwa?.......

Kumbuka Yanga ina wachezaji 30 na wengi ni wazuri na wamekosa namba......

Mbona muda mrefu Stephano Mwasyika aliumia na kufanyiwa operesheni nafasi yake ikazibwa vema na kijana Oscar Joshua(Kwangu mimi huyu mtotot ni mzuri kuliko hata Mwasyika).....

Mbona Yanga ilichukua ubingwa wa Kagame bila ya kuwepo kwa mtaalamu Haruna Niyonzima(alikuwa anachezea APR) na kiungo kilikuwa kikichezwa vema na wataalamu Geofrey Bonny na Rashid Gumbo 'Fundi'(Huyu ndio alitoa krosi tamu iliymkuta Kenneth Asamoah akatupia kichwa kilichompeleka Kaseja Marikiti na kuipa Yanga goli la ushindi)....

Vilevile Nadir Haroub kwa kipindi kirefu aliumia na nafasi yake ilikuwa ikizibwa vema na Chacha Marwa pamoja na Bakari Mbegu bila kumsahau bwana mdogo Ibrahim Job....

Jerry Tegete hayupo kwenye 1st eleven,muda mrefu hajaanzishwa.....ina washambuliaji lukuki wa kati ambao hata wasipokuwepo Davies Mwape na Kenneth Asamoah bado watafanya vizuri....Tunao Shamte Ally, Pius Kisambale, Omega Seme, Hamis Kiiza 'Diego' na wengine wengi ambao ni wazuri tofauti na unavyofikiri....

Nurudin Bakari karudi juzi tu wakati wa 2nd leg na Zamalek.....Hakucheza kwa karibu wiki 3 na Yanga bado ilikuwa ikifanya vizuri tu........

Yanga ni zaidi ya uijuavyo mkuu.........

Yanga Afrika.......Mabingwa wa Tanzania na Afrika Mashariki na kati.......Hivi Simba mna kikombe gani vile?,la Mapinduzi?....La hasha......

pale key players ni wawili 2 canavaro,nurdin.TEGETE HANA NAMBA,MWASKA YUPO OSCAR JOSHUA
 
yanga ni vilaza wote
[video=youtube_share;TMY4QVjIsvM]http://youtu.be/TMY4QVjIsvM[/video]
 
we unaushahidi,au umeskia clouds a.k.a tawi la simba.nani asiyejua jopo lawatangazaji wa michezo woote 11 kasoro,ibrahim mohamed pale clouds ni wanachama nawengine ni viongozi wa simba ?hii ni police case sio unaropoka .:shut-mouth:

wale wote simba hawawez kuisema vzuri yanga shame on them
 
sisi ni vichwa vya wendawazimu,bila nidhamu hakuna kitu chochote kinaweza kufanyika,soka atujui,nidhamu hatuna pia
 
Nimeshangazwa sana na baadhi ya watu wazima, wanaoheshimika kuinuka bila hata ya aibu na kusapoti huu utumbo uliofanywa na wachezaji wa Yanga.
Ni kitendo cha aibu sana kwa wachezaji wakubwa hivi kufanya hayo mambo. Haya mambo tumezoea kuyaona mchangani huko mchafukoge na magereza lakini kwa Yanga ilikua ni jambo la kufedhehesha sana.
Nadhani ule utaratibu wa kuwapima hawa wachezaji kabla ya kuingia uwanjani ufanyike kwani wengi wao wanavuta mabangi yanayowalipua vichwa.
 
Tunataka kuanzisha klabu ya ndondi sasa tulikuwa tunatesti zari...lol... Yanga mmetuangusha....
 
Mkuu Massai!

Mchezaji tena wa kulipwa kufungiwa kutocheza soka mwaka mzima (au hata miezi sita) unasema ni adhabu ndogo wakati mpira ndiyo ajira yake?

Au mkuu ulitaka kusikia Yanga imefutwa kabisa ndiyo ufurahi

Ni kweli lile vurumai hata mimi sikulipenda lakini umesikia malalamiko ya wachezaji Yanga kuhusu comments refa wakati mechi ilpokuwa inaendelea?
 
mkuu massai!

Mchezaji tena wa kulipwa kufungiwa kutocheza soka mwaka mzima (au hata miezi sita) unasema ni adhabu ndogo wakati mpira ndiyo ajira yake?

Au mkuu ulitaka kusikia yanga imefutwa kabisa ndiyo ufurahi

ni kweli lile vurumai hata mimi sikulipenda lakini umesikia malalamiko ya wachezaji yanga kuhusu comments refa wakati mechi ilpokuwa inaendelea?
soka lenye nidhamu duniani lipo ulaya,hususan uingereza nidhamu ya mashabiki na wachezaji ni vitu muhimu sana hasa uwapo uwanjani.sasa kama kwenye pitch wana behave namnahile nje ya uwanja wanakuaje?tuache ushabiki kama ni kwawenyetu walioendelea kisoka unadhani pale adhabu gani ingestahili kwa kitendo cha refa kupigwa ngumi na mchezaji?nakama si kuzuiliwa na wenzake unadhani hatima ya yule refa ingekua nini?nasisitiza nidhamu na uwajibikaji ndio nguzo ya muhimu katika kufanikiwa katika hili chandimu letu siwezi liita soka kamwe.naomba nipe adhabu iliyokua inastahili katika soka la kimataifa.
 
Mimi ni Yanga damu. Lakini timu yetu hii imekuwa ni upuuzi mtupu na hii ni kutokana usajiri wa hovyo hovyo kila mwaka.
 
Back
Top Bottom