Kitendo walichonifanyia mwaka jana pale Cinemax. Kweli hawataenda Mbinguni mpaka leo nina jeraha kubwa sana

Kitendo walichonifanyia mwaka jana pale Cinemax. Kweli hawataenda Mbinguni mpaka leo nina jeraha kubwa sana

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Wale jamaa wahuni sana , nawachukia kiroho mbaya. Nliwahi fikiria hata kuwaroga. Basi tu ila nikiona hata jina lao tu napaliwa na chakula, pumzi inakata nahema kwa shida na macho yanakuwa mekundu.

Yaani wale jamaa wakunilisha mimi pop corn tsh 8,000? Pamoja na mademu 4 jumla 40,000 pop corn? Siwezi kusahau tukio hili la kifisadi, kitapeli, kijambazi, kinyonyaji na kinyanyasaji. Ipo siku tu watalipa.
Mwaka jana miezi flani imetoka movie moja nzuri (hata jina nimesahau. Na hata kwa kweli siku ile ile movie sikuweza ielewa. Nlikuwa na hasira sana)

Demu wangu aliomba nimtoe out tukaangalie movie ile ilikuwa very romantic. Nikasema haina shida. Akaniambia kama sitojali aje na mdogo wake yupo tu home anazaga zagaa amemaliza chuo.

Nikasema Hewallah Bibie uje naye tu hamna shida. Kweli tukakutana pale Mcity nje tukaanza na kula Ice Cream pale opp na duka la Nguo za Michezo. Tukiwa hapo wakapiga simu rafikize galfriend wangu. Wakamwambia wamemwona. Akawaambia waje wanisalimie.

Wakaja nisalimia. Nikawakaribisha wakakaa nao mmoja akaagiza ice cream mwingine kahawa Cappuccino sijui Kapuchino... Yaani shida tu hawa masister du. Watu tumezoea mademu wa uswazi wanaagiza chips kuku bei haizidi tsh 10,000.

Basi wakawa wanaongea galfriend naye kwa kutaka sifa akasema tunaelekea Cinemax kucheck movie. Wenzie nao wakaingia tamaa kuwa nao wanataman wangeiona. Ila ndo hivyo hawakujipanga. Shemu wenu akawaambia twendeni shem wenu atawalipia. Moyo ukashtuka mfukoni nilikuwa na 200,000.

Tumeenda kulipia tsh 10,000 kichwa, halafu miwani ya 3D 5,000 kwa watu watano. Tunaenda kwenye pop corn wakatupimia kila mmoja na mfuko wake wa kakhi. Nauliza tsh ngapi wananiambia 40,000. Moyoni nikasema Whaaaaaaaaat????? Nikashusha saut nikauliza why 40K?wakaanza stories za sijui sukari ya hizi pop corn sijui inatoka wapi.... Daah... Ye maumivu siwezi yasahau.

Wakati huo wale warembo wameshatangulia kwenda kuchukua na vinywaji. Wawili soda wawili juice za box. Wallah.... Nilitamani wale watu niwagegede pale pale....soda moja tu tsh 2000 sasa juice ya box ya 3000 mtaani pale 5,000. Wale jamaa nakwambia hawaendi Mbinguni. Piga ua hawaendi. Watakuwa Wamewaumiza watu wengi sana sidhani kama ni mimi peke yangu.

Mimi mpaka leo sitaki hata pita lile gate maana nikiona jina lao nachefukwa sana. Nawaza ukatili walionifanyia, nawaza jinsi ambavyo walibaka nafsi yangu siku ile.

Niliendelea kuwa natabasamu tu na mashemeji zangu ambao nao toka siku ile sitaki hata kuwasikia mbwa wale. Nlienda angalia movie ile hata sikuielewa. Yaani wale cinemax mwaka jana walinifanyia uhuni sana. Na receipt nilitunza ikaja tu ku fade. Nlisahau kuitoa copy.

Hawa jamaa mbingu watasikia tu kwa watu kama sisi. Hawaendi labda wabadilike na pia kuturudishia kiasi flani. Wametuumiza sana sisi wengine
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Demu wako ndo mwenye makosa 😀😀

Ila watu umetoka na mpenzi wako muda wa kuita mashost unapata wapi😀 au mi ndo mshamba au nna roho mbaya
Alitaka sifa za kijinga. Nlikuja mwambia alifanya uswahili sana.
 
Uzuri hukuitwa, wengine mbona wanalalamika gahalama ndogo Sana pale na wanampango wa kuongeza maana mpaka wapaka kucha wanaingia now. Kiingilio kitakua 15,000 na hizo corn zitauzwa elf Saba, soada elf Tano na juis elef 8 Kisha ualike mashemeji Tena .
 
Wale jamaa wahuni sana , nawachukia kiroho mbaya. Nliwahi fikiria hata kuwaroga. Basi tu ila nikiona hata jina lao tu napaliwa na chakula, pumzi inakata nahema kwa shida na macho yanakuwa mekundu.
ories za sijui sukari ya hizi pop corn sijui inatoka wapi.... Daah... Ye maumivu siwezi yasahau.

Wakati huo wale warembo wameshatangulia kwenda kuchukua na vinywaji. Wawili soda wawili juice za box. Wallah....

Hawa jamaa mbingu watasikia tu kwa watu kama sisi. Hawaendi labda wabadilike na pia kuturudishia kiasi flani. Wametuumiza sana sisi wengine
Baba wao ni wao mshauri kijana Gily
 
Wale jamaa wahuni sana , nawachukia kiroho mbaya. Nliwahi fikiria hata kuwaroga. Basi tu ila nikiona hata jina lao tu napaliwa na chakula, pumzi inakata nahema kwa shida na macho yanakuwa mekundu.

ale cinemax mwaka jana walinifanyia uhuni sana. Na receipt nilitunza ikaja tu ku fade. Nlisahau kuitoa copy.

Hawa jamaa mbingu watasikia tu kwa watu kama sisi. Hawaendi labda wabadilike na pia kuturudishia kiasi flani. Wametuumiza sana sisi wengine
Ha ha ha
Ysmetutokea wengi!
 
5A3D7F6D-1C08-4E3B-951F-864556FE7E6B.jpeg
 
Nakumbuka niliwahi nunua popcorn ya buku pale katiakoo nikaenda Zama nayo mkuki. Nafika mlangoni wakanizuia wakaniambia nawaharibia ati nembo ya mfuko sio Yao. Nikaanza ila palepale iishe dah wakaniambia apo ndio naharibu kabisa. Nikawapa wakanihifadhia mpaka muvu ilivyoisha nikatoka nikachukua nikasepa nayo.
 
Hovyo sana hawa jamaa... Wamekaa kiwizi wizi tu.
 
Back
Top Bottom