Kitete cha Simba ugenini, nini shida?

Chambou255

Member
Joined
Feb 15, 2019
Posts
16
Reaction score
19
Simba kwa mara nyingine imeendelea kupata tabu ugenini kwa kupigwa 2-0 na JS Saoura.

Mechi ya mwanzo iliyopigwa taifa Simba walishinda 3-0 kupelekea Saoura kumtimua Nabil Neghiz aliyekuwa kocha mkuu.

Stori ileile ikajirudia kwa Al Ahly wakifungwa 5-0 Misri na kuondoka na ushindi wa 1-0 kwa Mchina.

Kwa matokeo hayo kundi limezidi kuwa ngumu kwa kila timu kuwa na nafasi ya kupita kutegemea kuteleza kwa wapinzani wenzao, kila timu ina mchezo mmoja Simba wakiwa na pointi 6, Al Ahly na vita wakiwa na 7 kila mmoja huku Saoura wakiwa na alama 8.

Swali la msingi, Kwa nini unadhani Simba wanakuwa na kitete ugenini na nini kifanyike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba inawachezaji wenye umri mkubwa, wakikutana na watu wanao kimbiza, simba wanapoteana vibaya sana. Soura walikua wana kaba kuanzia mbele kwa kasi, Soura wakipata mpira ni mbio nyingi, wame cheza kwa kasi karibu dakika 75 kweli wachezaji wetu wangeweza kucheza dk 75 kwa kasi ile? Wachezaji wa Soura karibu wote mpira unakaa mguuni, Tutawalaumu bure Wahenga wetu. Apa Nyumbani Simba uwa wanatumia Gharama kubwa sana kushinda mechi yaani mambo ya nje ya uwanja ni mengi mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endeleeeni kuweweseka.. Myama ndo tayari keshatinga robo. Kwenye kundi D kila timu inajilinda kwao. Huyo vita anaevaa jezi kama za vyura hachomoi taifa.
 
kilichonishangaza tobo zilikuwa nyingi, sijui sababu ni uhenga??!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba bado ni timu dhaifu sana,back pass za kijinga mno zimewacost penati.
Timu inapaniki sana.Nionavyo kwa Tanzania kisoka bado kama simba ndiyo wanacheza kichovu hivyo sijui waliobaki wakina yanga na azam itakuwa mdebwedo wa maana
 
Ukiwauliza hilo swali Mbabane wata kurushia mawe! nazani ata Vita, Mazembe, Esperance, Zamalek nao wana vitete ugenini! yale tuliyoyaona kwa Man U na Ajax, Africa ni ngumu sana kuyashuhudia. Ila Simba wajitahidi ugenini wasifungwe zaidi ya bao 1.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endeleeeni kuweweseka.. Myama ndo tayari keshatinga robo. Kwenye kundi D kila timu inajilinda kwao. Huyo vita anaevaa jezi kama za vyura hachomoi taifa.
sawa.

Sent from Nokia 7 Plus
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…