Kiteto: Wanawake wawili wakamatwa na Nyara za serikali

Kiteto: Wanawake wawili wakamatwa na Nyara za serikali

Kwenda zako huko. Digidigi ni ishu?
Sidhani kama watamshikilia , wanapiga biti tu hapo ili kutoa elimu.

Ila mwisho wa siku wasipopigisha mikwara kwa namna hiyo raia wakishajua utamu wa nyama ya porini wakaanza kuleta mazoea ya kuwinda kuwala then expect kuanzishwa tabia ya wawindaji haramu kuweka mitego bila utaratibu ambayo hunasa hadi wanyama wasiohusika kama twiga, tembo, simba, chui, etc ambayo huwapa majeraha,na vilema vya kudumu ambavyo huwatesa.
 
Wapewe tu onyo au adhabu ndogo na kuachiwa. Ni kitu kidogo sana. Hawa ni watu maskini wanaohangaikia tu maisha.

Hakuna mwenye uwezo atakayehangaika na digidigi.

Hizo nyara pia siyo za Serikali. Ni nyara za umma, na Serikali ni mlinzi tu. Kwenye umma, na hao akina mama wamo.
Ni sawa, ukawa na watoto 10, umewatengea shamba la mahindi linalosuburi yakomae, yavunwe ili hao watoto 10 wafaidi kwa pamoja, lakini mmojawao, kabla hayajakauka, akavunja mahindi matano akaenda kuchoma ale. Kwa mzazi mwenye huruma, utampa onyo, na kumwachia.

Lakini onyo ni muhimu. La sivyo kila mmoja ataona kuwa unaweza kuwinda wanyama pori, na hutafanywa chochote. Baadaye watatoka kwenye digidigi wataebda kwa nyumvu, baadaye kwa tembo.
 
hadi huruma wangechukua nyama hizo wakale na kurudishwa mtoto swala porini yaishe....... Tunapakia twiga na hatushikwi
 
Watu wanauza wanyama na kusafrisha ulaya wanajipatia mabilioni mama wa watu kakamata digi digi ajipatie kitoweo, imekuwa nyara, na polisi kakaza fuvu kabisa


Nchi hii bado sana, tuko nyuma mno.
 
Wanawake wawili wa Kijiji cha Kimana wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kiteto kwa kukutwa na nyara za Serikali, ambazo ni Swala na mtoto wa mnyama aina ya Digidigi ambaye yuko hai.

Wanawake hao ni Veronica Paulo (24) na Witnes Paulo (20) ambapo Machi 20.2023 wakiwa nyumbani kwao wamedaiwa kukutwa nya nyara hizo za Serikali wakiwa eneo la Njutaa kata ya Partimbo.

Frz8OzVXwAAm0mp


Eti nyara ya serikali !!, Serikali hiyo nyara kaipata kutoka wapi??.
 
Na wanavojua kuzitumia Intellectual intelligence walizosoema kwenye vijitukio vidovdgo utazani kwel tuna polisi.

Ije ishu ya jangiri utaona wanafanya upelelezi Hadi mnasahau.

Toka lini nyma ikawa nyara za serikali, Kuna KAZI ni laana hapa Tanzania ikiwemo Police
 
Ni uonevu.
Mtu yupo pembezoni mwa hifadhi mwacheni ale vya hifadhini mdogomdogo.
Wanyama wako wengi , vitu vingine muvipotezee
 
UOnevu mtupuuu, kwahiyo wanataka watu wafe njaa??
Police sijui wakojee, wanakera mnooo.
Mxxxieeeew
 
Na wanavojua kuzitumia Intellectual intelligence walizosoema kwenye vijitukio vidovdgo utazani kwel tuna polisi.

Ije ishu ya jangiri utaona wanafanya upelelezi Hadi mnasahau.

Toka lini nyma ikawa nyara za serikali, Kuna KAZI ni laana hapa Tanzania ikiwemo Police
Gharama walizotumia tu kwenda kuwakamata hao wanawake na kuita waandishi inazidi bei ya hiyo nyama,, polisi wapuuzi sana
 
Wakati nipo mdogo nimekula nyama za hao digidigi sana,ni tamu kwa kweli,si ndio wazaramo wanaita Mnokela?
 
  • Naamini dada za watu waneingia kwenye mikono ya 'wanyonya damu'.I
  • li wapate kupona hao askari watawananii ... watakavyo na watatoa rushwa ya hela
 
Malkin wa Tembo kaua mamia ya Tembo yupo kitaani! Hao wadaa kwa kukutwa na finyango tu za Swala watapotezwa.
 
Back
Top Bottom