Kitila Mkumbo awakosoa CHADEMA juu ya kuwafukuza wabunge wa viti maalum

Huyu professor kipindi yupo wizarani aliulizwa idadi ya viwanda 100 kila mkoa walivyokua wanasema wamejenga ,akaweka link ya document nikaifungua ni aibu tupu .

Yaani hakuna cha maanw maana kule nilikuta machine za kusaga nafaka , cherehani , uhunzi n.k

Kama ndio professors wa Tanzania ndio wa aina hii sio ajabu hata watu wanaowafundisha ni bomu.

Kuna siku nimekuta mtu mmoja mtandaoni mwenye degree yake ila barua anayoandika ni upuuzi mtupu.
 
Kuna tatizo katika kufikiria kwetu na wala si kura.

Siasa inaondoa uwezo wa kufikiri kwa nyakati. Nafikiria anayeongea ni Kitila Mkumbo

1. Yupo Bungeni, atueleze lin kura ya siri ilipigwa ! je amewahi kzungumzia hilo?

2. Kilichovuruga mchakato wa katiba ni kura ya wazi ya CCM leo analiona CDM kwa mara ya kwanza! Prof

3. Kura za mkutano mkuu wa CCM zilipigwa kwa ''siri' kwa mikoa. Kitila alikuwepo,je hiyo ni kura ya siri? Tena zilikuwa na namba.

JokaKuu
 
Mbunge wa Ubungo Kitila Mkumbo amekosoa hatua ya CHADEMA ya kuwafukuza wabunge 19 wa viti maalumu walioteuliwa kwa tiketi ya chama hiko.

Amesema "Inaogopesha kuona njia pekee ya CHADEMA kutatua migogoro ya ndani ni kufukuzana. Duniani kote vyama vya upinzani vinaongoza kuwa na utamaduni wa kuvumiliana,kama Chadema wanatumia mabavu kiasi hiki kwa akina Halima Mdee wakiwa hawana dola, siku wakipewa dola itakuwaje"

Kuhusu kura ya wazi, Kitila amesema "Kura ya wazi/hadharani kwenye Demokrasia sio nzuri, na sio sahihi kwa chama kinachopigania Demokrasia hasa chama cha upinzani kama CHADEMA, ni kura inayokulazimisha mtu ufanye maamuzi ya "Group Thinking" Prof. Kitila Mkumbo
Huyu anatafuta uteuzi kelele sana saiv
 
..wangepiga kura ya siri wangesema imechakachuliwa.

..Naibu Katibu Mkuu Kigaila ametolea ufafanuzi kura ya wazi.

..amesema kunapokuwa na suala la uchaguzi, unamchagua Jpm au Ssh, ndipo inapigwa kura ya siri.

..kunapokuwa na suala la uamuzi, kwa mfano unaunga mkono bajeti au la, inapigwa kura ya wazi.

..hivyo ndivyo Naibu Katibu Mkuu Kigaila alivyofafanua.
 
Ndivyo ilivyo. Wabunge pia wanatakiwa kupimwa kwa rekodi ya upigaji kura wao kwenye miswada na maazimio ya bunge. Rekodi hiyo inatakiwa kuwa wazi ili msimamo wa kila mbunge ujulikane. Uchaguzi wa viongozi na wawakilishi ni suala lingine.
 
Mbunge wa Ubungo Kitila Mkumbo amekosoa hatua ya CHADEMA ya kuwafukuza wabunge 19 wa viti maalumu walioteuliwa kwa tiketi ya chama hiko.

Amesema "Inaogopesha kuona njia pekee ya CHADEMA kutatua migogoro ya ndani ni kufukuzana. Duniani kote vyama vya upinzani vinaongoza kuwa na utamaduni wa kuvumiliana,kama Chadema wanatumia mabavu kiasi hiki kwa akina Halima Mdee wakiwa hawana dola, siku wakipewa dola itakuwaje"

Kuhusu kura ya wazi, Kitila amesema "Kura ya wazi/hadharani kwenye Demokrasia sio nzuri, na sio sahihi kwa chama kinachopigania Demokrasia hasa chama cha upinzani kama CHADEMA, ni kura inayokulazimisha mtu ufanye maamuzi ya "Group Thinking" Prof. Kitila Mkumbo
Kule bungeni huwa wanapiga kura za namna gani, pale wanapoitwa jina la mbunge mmoja mmoja?
 
Anazungumziaje swala la kushutumiwa kufoji majina kuyapeleka NEC? mnaohoji hawa watu mnawaogopa?
Kufoji na kupeleka nec kivipi?Vp na saini ya mnyika nayo ilipatikaje?

Nafikiri ungesema anatuhumiwa kupeleka majina nec bila ruhusa.
Na kama majina yalipaswa kupelekwa nec,tatizo lao hasa lipi?

Mdee analalamika mwenyekiti alikuwa anampango wakukiuka utaratibu kwakupeleka majina yake mfukoni,hili linatazamwaje?
 
Hawezi kuzungumzia forgery iliyofanywa na wanaccm/waliotumwa na CCM,akifanya hivyo kwa uwazi/ukweli naye lazima afukuzwe huko CCM.Mkuki kwa nguruwe...
Msingi Wa issue ya Mdee na wenzake ni uchafu uliofanywa na CCM, Mdee na wenzake walilazimishwa kuwa wabunge ili CCM ipate kuhalalisha uchafuzi kuonekana ulikuwa uchaguzi.Walikwiba kura zote bila kufikiria consequences za uendeshaji wa Bunge pasina wapinzani.Ndipo mchakato wa Mdee na wenzake ukafanyika,Professor anajifanya anafahamu mambo kuliko CDM ama Watanzania?
Tangu lini CCM na wanachama wake wakawa watetezi wa wana CDM au wapinzani?
 
Mbunge wa Ubungo Kitila Mkumbo amekosoa hatua ya CHADEMA ya kuwafukuza wabunge 19 wa viti maalumu walioteuliwa kwa tiketi ya chama hiko.

Amesema "Inaogopesha kuona njia pekee ya CHADEMA kutatua migogoro ya ndani ni kufukuzana. Duniani kote vyama vya upinzani vinaongoza kuwa na utamaduni wa kuvumiliana,kama Chadema wanatumia mabavu kiasi hiki kwa akina Halima Mdee wakiwa hawana dola, siku wakipewa dola itakuwaje"

Kuhusu kura ya wazi, Kitila amesema "Kura ya wazi/hadharani kwenye Demokrasia sio nzuri, na sio sahihi kwa chama kinachopigania Demokrasia hasa chama cha upinzani kama CHADEMA, ni kura inayokulazimisha mtu ufanye maamuzi ya "Group Thinking" Prof. Kitila Mkumbo
Kitila Mkumbo hana moral authority ya kuikosoa Chadema Mbona alikaa kimya bwana wake alipowafukuza wakina Membe?

Kitila Mkumbo ni mchumia tumbo aliyekatwa mkia!! Kutaka kwake Chadema wawasamehe wale mamluki ni Sawa na kuwashauri Chadema “Waonje Sumu”; akijua wazi kuwa SUMU haionjwi!
 
Kufoji na kupeleka nec kivipi?Vp na saini ya mnyika nayo ilipatikaje?

Nafikiri ungesema anatuhumiwa kupeleka majina nec bila ruhusa.
Na kama majina yalipaswa kupelekwa nec,tatizo lao hasa lipi?

Mdee analalamika mwenyekiti alikuwa anampango wakukiuka utaratibu kwakupeleka majina yake mfukoni,hili linatazamwaje?
Unaamini kwa dhati kuwa ndivyo ilivyokuwa?Shauri limepelekwa mahakamani na maamuzi ya huko yatazingatia uhalisia na hivyo in vema kusubiri.Japokuwa inawezekana wakakawia lakini tutayafahamu.Hofu yangu in gharama,muda,na mwisho wanaweza kuweka mpira kwapani kama ilivyokuwa kwenye shauri la Mwenyekiti Mbowe.
Tunafahamu ukweli lakini bado tunapotezeana muda wa kujadili uhalifu wa watawala na kuacha hoja ya upatikanaji Wa Katiba mpya ili kukomesha impunity inayoendelea!
 
Angeanza na zile kura za wazi bungeni,wanaoafiki waseme Ndiyoooo!
Hivi kumbe wanasemaga WANAOAFIKI?
Mi nlijua wanasema WANAFIKI waseme NDIO kisha Wenyewe wanaitikia
 
Back
Top Bottom