Kitimoto is overrated haina utofauti wala utamu kuliko nyama zingine..

Kitimoto is overrated haina utofauti wala utamu kuliko nyama zingine..

KITIMOTO KILA KTU KINAKAANGWA,nyie mlibugi ndo maana ilikuwa hivo
 
huyo mipishi ndo tatizo mkuu sio wewe, tafuta hotel moja wanao kaanga wa ku kaangie uone moto wake
 
Kwa miaka kadhaa toka nikiwa mtoto mdogo hadi leo hii nimekua sili Kitimoto Japo mimi ni Mkristo mkatoriki wa kuzaliwa. Hii ilitokana na sababu zangu binafsi na sheria kwenye biblia ya inayosema...
Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.

Mambo ya Walawi 11:7


Hivyo nikawa sigusi kitimoto hata nyumbani hakijawahi kupikwa (Mama alikua Muislim kabla, hatak ata kuiona japo mkatoriki)
Basi kwenye Pasaka hii ya Juzi juzi apa jirani yetu mchaga Noah yake aliipiga Breakdown akawa anauuza Kilo kwa buku Saba za lumumba tu. Tukachukua na sisi washkaji kilo 2 hivi. Nami nikasema ngoja nionje huyu mdudu ambao JF wanamsifia eti ni mtamu hasa ukishushia na Nyagi. Basi bwana ikaandaliwa vizuri sana hadi inaiitata nami nikasogea, nilijua nitakuta radha special kwenye pork (kulikua na supu, miskaki, iliyolostiwa, na ya pilau) asee mboga ya hovyo sana sijawah ona nilikula kidogo tu ikanishinda maana nilitema mate sana hafu nasikia imekaa rohoni. Ilibidi nile limao nzima ndo nikapata ahueni...

Nyama ya kuku itabaki kua nyama bora wakati wote kwangu hadi naacha hii dunia..

Da'Vinci: Young, Wild, Broke and Brainy.
Nyama tamu sana kwa Rank;-

1. Turkey(Classic Meat)(Wet frying)

2. Pork(Second Best)(Barberque ama Wet Frying). Ikiwa ni BBQ inalingana na Turkey kwa ranki.
3. Octopus
4. Duck(BBQ)
5. Chicken(BBQ)
6. Cattle/Goat.(kwa taste Hazina tofauti ya kupigiwa mstari)
7. Sheep
 
Acha kabisa hyo nyama mzee nan .... Ndio nyama tamu kati ya zote nilizowah kula ... Lakini supu yake sijawai kunywa ... Ila hyo nyama ukiichoma,ukiikaanga au ukipka roast yote ni balaa tupu
 
Dah, njoo Nakupeleka pale Madoto Kigogo, Yule Mzee anapika kwa order Yaani kama Hujaweka order yako usitie Mguu, order inatolewa week before...
Aisee watu mna maneno..
 
Nitakujulisha tu,i hope utakuja kufungulia uzi wa kuisifia nyama hii adimu hahahah
Unichinjie na hako kambuzi nyuma yako ili ikinishinda nipifie hako.. 🙁🙁 😀😀😀
 
Unichinjie na hako kambuzi nyuma yako ili ikinishinda nipifie hako.. 🙁🙁 😀😀😀
ha ha ha aisee we mgeni utakua mtata,eniwei nitajaribu kufikiria juu ya hilo!
 
Back
Top Bottom