Nawasalimu wanabodi.
Mwaka 2015 Mwanadiplomasia mahiri na kachero mbobezi Bernard Membe alijaribu kuusaka Urais kupitia CCM lakini akakatwa jina lake hatua za mwisho.
Macho na masikio ya wengi yalikuwa ni kwa Edward Lowassa na Membe lakini ngekewa ikamdondokea John Magufuli ambaye sasa ni Rais.
Mwaka 2016 mwezi Machi Jumuiya ya Madola (CommonWealth) ilitoa nafasi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ambapo ilikuwa ni zamu ya Afrika Mashariki kumtoa mtu. Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki ilipendekeza mtu huyo atoke Tanzania huku wakipendekeza awe ni Membe. Utarayibu wa Jumuiya hiyo ni kwamba anayependekezwa lazima apate kibali na ruhusa ya mkuu wa nchi yake.
Kinachosikitisha, Rais Magufuli akamwekea "bambi" Membe na nafasi hiyo ikaenda nchi nyingine. Membe akakosa nafasi hiyo.
Kama angefanikiwa kwanza angeenda kuishi jijini London. Angelipwa mshahara wa $50,000 kwa mwezi. Marupurupu $23,000, angesafiri na ujumbe wa watu 25 kila safari ya kikazi. Hizo ni faida binafsi.
Faida za kinchi ni pamoja na kupaa kidiplomasia duniani tofauti na sasa ambapo diplomasia yetu inaishia Buguruni. Tanzania ingezidi kusifika kwa kutoa viongozi hodari katika ngazi ya kidunia baada ya kina Dk. Salim Ahmed Salim, Dk. Asha-Rose Migiro, Balozi Mahiga (marehemu) nakadhalika. Unajiuliza ni kwa nini Magufuli alimkatili Bernard Membe?
Namshauri Magufuli, vichwa vya watu kama Membe si wa kuacha kuzurura nje ya utawala. Ni watu wa kuwa nao karibu. Mchukue Membe awe mshauri wako wa masuala ya diplomasia na usalama.
Nawasilisha!