Kitu gani kilichosababisha kuwepo na binadamu wenye rangi tofauti tofauti?

Kitu gani kilichosababisha kuwepo na binadamu wenye rangi tofauti tofauti?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Kuna waarabu, wahindi, wazungu, waafrika.

Na ukiangalia kitu kinacho watofautisha ni viwili tu; rangi ya ngozi na aina ya nywele, ila kimuundo wote wako sawa.

Sasa ni kitu gani kilicho sababisha kuwepo na huu utofauti?​
 
Kisayansi binadamu kiasili ni mweupe kama sokwe walivyo weupe. Alivyotoka porini na kwenda nyikani za Afrika Mashariki akapigwa na jua na kuwa mweusi. Alivyoanza kutawanyika kwenda mazingira mbalimbali akaanza kupata rangi mbalimbali. Kupitia natural selection watu wa rangi mbalimbali wakajigawa kimaeneo.

Kibiblia binadamu ni mweusi, wa kwanza kuwa mweupe ni Noah. Hadi baba yake alimshangaa na kwenda kwa babu yake kuuliza zaidi mbona nimezaa mtoto mweupe.
 
Enyi watu! Hakika sisi tumewaumba kutokana na mwanaume mmoja na mwanamke mmoja na tumewafanya kuwa ni mataifa na makabila ili mfahamiane, hakika aliye mtukufu wenu zaidi mbele za Allah ni aliye mchamungu zaidi katika nyinyi, hakika Allah ni mwenye elimu mwenye khabari {zote}.

Qu'ran 49:13
Aya ni maneno ya watu wa zamani walijiandikia kutokana na kutokuwa na jibu na mada tajwa.
 
Back
Top Bottom