Kitu gani kilikushangaza ulipofika Dar kwa mara ya kwanza.

Hongera mkuu wewe ulikuwa na lengo la kujifunza, kuna wengine walitaka kufika maisha club kwanza.
[emoji1] [emoji1] yaani nilikuwa na mzuka balaa na Bahari. Niliingia usiku kutokea Mkoani, Kesho yake nikadamkia kwenda baharini straight!!!
 
Mim nilishangaa sana kuona watu wananunua mihogo mibichi na kula na chumvi ilinibidi nikate mbavu mpaka watu wamenishangaa.
 
hahahahaaa
 
Hahaha
 
Mimi nilishangaa kuona wanaume wa dar wanavaa vinguo vya kubana makalio kama dada zao-pia kuona kaka wanakaba dada wanajiuza
 
Nilishangaa kuona mtu anakula hivi
1.ASUBUHI
-vitumbua viwili na chai ya rangi

2.MCHANA
-chips mayai na mishkaki

3.JIONI
-miogo ya jero na juice ya mua

4.USIKU
Burger au pizza
 
Dah nyie acheni wakuu Dar ya zamani ilikuwa na hadhi kwa watu wa mkoa. Nilikuwa nikirudi watu wanataka niwasimlie stori za akina Maxi na Zembwela halafu na kiswahili changu cha Kidaslamu haha nilikuwa nawakalisha.
Stori zipi za max na zembwela ?
 
Mtoto wa watu nimetoka Tanga nilikua siamini hivi vitu ila kukuta wadada wamejipanga Kama mishkaki na hawaogopi hata watu ilikua jambo LA kushangaza kweli kweli
Mimi nilishangazwa na watu kupanda daladala hata kama ni hatua 10 mbele..mtu anapanda daladala mwenge anashuka itv

Nilishangazwa sana wa watu wa dasilamu kwa hilo
 
Ukianzishwa uzi wa kitu gani kilikushangaza baada ya kufika ughaibuni kwa mara ya kwanza mnishtue[emoji3][emoji3]
 
Hii mambo ya kufunga mtaa na kusutana ilinishangaza sana.
Dar hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…