kitu cha kwanza, wanakula sana vyakula vinavyoboresha ubongo wakati wa ukuaji, sea food. pili, wanasisitiza sana watoto wao wasome na wanajali sana elimu. korea kusini kwa mfano, vifo vingi vya kujirusha gorofani vinatokana na wanafunzi ambao hawajafaulu mitihani. kitu kingine, ni kuzaa watoto wachache unaoweza kuwatunza na kuwapa mahitaji yote kuanzia chakula, shule za awali hadi vyuo vikuu, kingine ni mifumo yao ya elimu, mtu anasoma kile anachoenda kukifanya na miundombinu inawasapoti. pia, wanatumia sana suppliments. hata hapa kwetu tungekuwa hivyo watu wangetuona kuwa tuna akili nyingi.
tofauti na bongolala, tunakula ugali, viazi, magimbi, michapati, hatuli nyama ya kutosha, hatuli samaki za kutosha kwasababu hatuna pesa. familia za asia samaki kila siku wanaweza kuwepo, bongo kwa wiki unaweza kununua smaaki kidogo sana na mnagombania na watoto (badala ya kuwaaahca watoto wale). vyakula vyetu vingi havina madini ya kukuza ubongo wa watoto vizuri.