Kitu gani kinasababisha wanaume kuwafanyia wanawake matukio ya kikatili?

Wewe ukizingua nani anakupiga?
 
Well said
 
Mwanaume dhaifu hukimbilia nguvu na ukatili. Akikuchoka au umemchoka muache aende zake maisha hayatakuwa mwisho. Ila pia tungekuwa na uwezo wa kuongea au kupima miili ya wanaume wengi waliolala makaburini, pengine nao wamekufa kwa mateso makubwa sana.
 
Umeeleza Vizuri sana mkuu
 
Ndani ya ndoa na mahusiano kunamambo mengi sana ya Siri. Wahehe wanamsemo usemao "Munyumba na kugati kulimafunikisi" au "Mugati munamafunikisi" hivyo kupeleka lawama Moja Kwa Moja Kwa mwanaume ni kosa kubwa sana. Yafaa zikafanyika tafiti Ili kubaini ukweli wa ndani na wakina, ndipo tutoe lawama Kwa mwanaume. Maana hata dawati la jinsia au ustawi wa jamii wameegemea upande mmoja wa kumtetea mwanamke mwishowe wanasababisha umasikini mkubwa katika familia.

Kuna siku nilikutana na askari mmoja wa kike mkoani Iringa, yupo kwenye dawati la jinsia, nikamuuliza jambo linalohusiana na ukatili wa kijinsia, maana kulikuwa na jamaa yangu anamgogoro wa ndoa. Askari huyo alifunguka akasema jinsi mambo yanavyoenda ya ukatili. Wao baada ya shtaka kuletwa la ukatili huwa wanaanza uchunguzi wa kina kujua Nini chanzo na je jambo linaukweli kiasi Gani? Ndio maana walikuja kubaini kuwa mkoani Iringa wanaume wanafanyiwa ukatili sana na wake zao. Na ndoa nyingi za wasomi Kwa sasa zinasumbua kiasi kwamba wanapokuja kuleta malalamiko unaona kabisa kuwa kunakaujuwaji Fulani Kwa mwanamke.

Akaendelea kusema kuwa, siku hizi wanawake wamekuwa wakishawishiwa na ndugu, jamaa na marafiki Ili kumshtaki mwenza wake kuwa kafanyiwa ukatili wakiwa na lengo la kugawana Mali na hao marafiki wanakuwa karibu sana wakimpa msaada wa danganya toto na mwisho wa siku pesa ikipatikana ya mgawo Mali wanapata chochote, mwisho wa siku mwanamke aliyevunja ndoa yake anabaki hohehae. Na mengine mengi sana aliniambia.

Ushauri wangu Kwa dawati la jinsia na ustawi wa jamii, mkiletewa jambo lolote linalo husu ukatili tafadhari msikimbilie kutoa majibu ya Moja Kwa Moja, yafaa mfanye uchunguzi wa kutosha, ikiwezekana muende mpaka anapoishi, majirani na ikiwezekana anakofanyia kazi muhusika mwaweza pata taarifa muhimu pasipokuwa na shaka lolote na mkatenda haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…