wiki iliyopita nilienda kwenye harusi ya jamaa yangu basi mc akawa anaongea kwa madoido ni balaa, mara tukastukia anasema hii harusi ni kiboko ni wakati sasa wa msosi, nimeambiwa watu watakula mpaka wakimbie, subirini nikahakikishe. jamaa si akazungukia kwenye ma hot pot, mara akarudi na mbwe mbwe zimezidi aisee nikweli watu watakimbia msosi, akaenda kumbeba mtoto mdogo huku anaendelea na ku mc, katika kumrudisha kwa mama yake, wakati kainama amshushe hakuangalia kumbe mkono mmoja wa mtoto Upo kwenye mfuko wa koti lake la suti ile kamshusha tu, mkono wa mtoto ukatoka na paja la kuku wa kukaanga, jamaa akstuka na kuzuga : ayaaah... eheee na hiyo ndio zawadi yakoooo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. wakati mtoto mwenyewe hata meno hajaota.
Sent using
Jamii Forums mobile app