Kitu gani uliwahi ona au kushuhudia ukacheka sana?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
hahaha mkuu nimejikuta nacheka
 
wiki iliyopita nilienda kwenye harusi ya jamaa yangu basi mc akawa anaongea kwa madoido ni balaa, mara tukastukia anasema hii harusi ni kiboko ni wakati sasa wa msosi, nimeambiwa watu watakula mpaka wakimbie, subirini nikahakikishe. jamaa si akazungukia kwenye ma hot pot, mara akarudi na mbwe mbwe zimezidi aisee nikweli watu watakimbia msosi, akaenda kumbeba mtoto mdogo huku anaendelea na ku mc, katika kumrudisha kwa mama yake, wakati kainama amshushe hakuangalia kumbe mkono mmoja wa mtoto Upo kwenye mfuko wa koti lake la suti ile kamshusha tu, mkono wa mtoto ukatoka na paja la kuku wa kukaanga, jamaa akstuka na kuzuga : ayaaah... eheee na hiyo ndio zawadi yakoooo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. wakati mtoto mwenyewe hata meno hajaota.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimkuta mtoto mdogo kama miaka mitano hivi ananunua chips mayai wakati analipia akatoa mfukoni Kama shilingi eflu nane na zaidi. Nikamwambia dah!! wewe bado mdogo unahela zote hizo ? Alinikazia macho kisha akaniambia " eeh, unashangaa sasa hivi, sasa we subiri niwe mkubwa kama babaangu.. [emoji851][emoji851]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa alipatwa na Tumbo la kuhara afu kwata imechanganya kwenye Guard alikuwa pembeni yangu .....
Basi afande akisema mbele tembea wengine tunarusha mikono yote Jamaa naona mkono mmoja anarusha mmoja amebana makalio pia tukiambiwa mbele tembea yeye anatembea nusu kulia (kiupande upande) yaani alikua kama mbogo kachanganyikiwa afande hatoi TANO aisee nilipiga kwata nacheka hadi machozi sitasahau....
822 Musoma Mara na unaa wa afande Kachila.[ NYUKI HAPIGWI BUSU]

via Huawei Social Phone
 
Haahhahahahahaua nakojoooaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hiyo inachekesha mno unashindwa jizuia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…