Siku moja nakumbuka nimeingia kwenye mgahawa mmoja hivi , aseeeh nilikutana na bomba la kunawia ambalo sijui hata linafunguliwaje. Nilihangaika sana bila mafanikio na nikawa naona aibu kuuliza , niliganda pale pale nikawa najifanya nakunja shati huku nikisubiri mtu aje ili nione wanavyofungua. Basi, ikapita kama dakika moja hivi mdada akaja kunawa.
mdada: Kaka za sahizi?
Mimi: salama Dada
Mdada: vip kaka,maji yameisha nn mana nimekuona upo umesimama hapa muda mrefu?
Mimi: maji yapo, ila kuna mtu tu namsubir hapa[emoji4]
Mdada: anhaa, si ungeket tu kweny kiti kaka angu?
Mimi: kimoyo kimoyo nikawa najisemea huyu Dada katumwa nn[emoji1] ?
Basi alivyomaliza tu kunawa na mimi nikaenda kunawa, kumbe ili maji yatoke unatakiwa ubonyeze kibatan ambacho kipo pale pale juu ya bomba then ukimaliza we unasepa zako, bomba linajifunga lenyewe bila kuguswa[emoji1] [emoji1] [emoji1] , mi nilikuwa nahangaika kuzungusha Tu. Dah huwa nacheka sana nikiifikiria hii siku
Sent using
Jamii Forums mobile app