Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

1. Defensebring sio credible source. Nataka BBC, Wikipedia, CNN, hivyo. Ndege tu ikianguka dunia nzima news. So niletee news source inayoeleweka hizi page hata wewe unaweza tengeneza.
2. 🤣Unajuaje sijaishi kijijini. Yaani we utaendelea kushift tu premise, Mara nikue, Mara niende Kijijini, Mara kiroho cjui. Mwishoni utasema nife ndo nitaona Kama watu wa dini wasemavyo.
3. Niambie kitu ambacho wanasayansi wameshindwa kuelewa na wakakaa kimya na kusema ni uchawi?
 
1. Kusema kwamba ni uchawi ni wivu wa maendeleo na uvivu wa kufikiria. Ili upate majibu mfate akuulize, maisha hayana formula. Wengine wanatumia miaka 10 wengine siku 2. Bado hujaprove uchawi.
2. Waganga wa kienyeji wapo kazi yao ni tiba asilia.... Sioni shida hapo
3. Freemason society ipo na majengo yake yapo, Ila wasemayo kuhusu freemason na makafara sijui shetani ni uwongo na Hamna ushahidi wa Hilo.
 
Kwanza toka mwanzo hoja yangu ni kwamba kwenye kufanikiwa wakati mwengine ni zaidi ya kufuata kanuni na kufanya kazi kwa juhudi, huo ndio msimamo wangu. Na wala sijasema kwamba kufanikiwa na kutofanikiwa basi lazima uchawi tu ndio unahusika.
Sawa ndo maana nimesema factors zipo nyingi ila none of them ni uchawi
 
Tuelezee hilo jambo kiscience chief,

Ilikuaje akawa kichaa
We jamani si umesoma ubongo au...si unajua psychology, mental problems na Nini. Sasa unauliza Nini, so ukichaa nao ni uchawi jamani. Si kusingekuwa na milembe. Au milembe Kuna waganga na wachungaji tu kule wanaombea.
 
Mkuu mbona matukio ya kutapeliwa na kuibiwa pia yapo, wewe umetaka yenye kuhusu uchawi ndio nimekutajia hilo la chuma ulete. Hata wanaoiba simu huku mtaani wanachomwa moto ila wanasiasa wanaoiba mabilioni hawaguswi.
🤣Ndo mtu akiibiwa anasema chuma ulete ni excuse. Siku hizi sio lazma ukabwe. Mjini watu Wana tactics nyingi Sana mpaka kuja kukuibia. Ndo maana nasema ni mchezo wa akili sio uchawi. We unasema uchawi kabla ya kuelewa. Ukielewa unacheka tu unakubali umepigwa bac ndo maisha, mi mwenyewe yashawahi nikuta so naelewa
 
Miaka fulani nikiwa chuo nilienda field kijiji fulani huko Dodoma. Sehemu niliyokuwa nafanya field ilikuwa nje kidogo na sehemu yalipo maduka. Sasa siku moja nilikuwa napita njiani nikasikia watu wanaambiana "huyu kijana anapitaje hiyo njia usiku huu". Sikuelewa sababu ya wao kutokupita ile njia usiku

Sasa siku moja tukiwa watatu na jamaa zangu ninaofanya nao field, mida ya saa moja jioni kigiza giza ndio kinaingia. Tunawa tunavuka kuna sehemu kulikuwa na mto kwenye hiyo njia ila hauna maji. Sasa kwa mbele tukaomuona mzee mmoja aliyeonekana umri umeenda sana anatembea polepole kwenye ukingo wa pili wa mto, tulitegemea tukija kuibuka tutampita. Lakini tulipokuja kutokea hatukuona chochote.

Mwanzoni nilidhani nimeona peke yangu nikakaa kimya. Baadae tukiwa tumeshafika yule mshikaji nae akaniuliza kama niliona lile tukio. Mshikaji wetu mmoja yeye hakuona alikuwa yuko bizzy kuchati na simu muda tukio linatokea.

Tulishangaa sana maana ile sehemu haikuwa na mti wala kichaka cha kujificha ni eneo plain tu. Na ilikuwa ni kitendo cha sekunde chache sana, yule mtu kutokomea kabisa asionekane, hata ingekuwa gari ni lazima tungeikuta.

Sasa uniambie ilikuwa ni hallucination uone kama sijakuzabua makofi.
 
baki hivo hivo

Ezekieli 21:21
[21]Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huko na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini.

sio lazima ujue uchawi wa kutazama maini ukoje.
 
 

Attachments

  • Screenshot_20230804-184846_Firefox.jpg
    157.9 KB · Views: 10

MKATABA WA DP WORLD UCHAWI UPO
 
Hallucinations....🤣ungetaka kuaminika ungerecord
 
🤣🤣🤣🤣 Nimekuambiaje hiki kitabu kina makosa mengi kuliko gazeti la Jana. Soma post yangu ya #653 utaelewa. So this isn't evidence, ni kama story nyingine tu unanihadithia
 
Kwahyo kauli yako ya mwanzo kwamba wazungu hawaamini uchawi unaifuta???

Ni elimu ipi unayoiongelea ambayo unahisi watu wakiipata wataacha kuamini kuwa kuna uchawi?
Ya shule tu... kwani shuleni unafundishwa kitu chochote kuhusu uchawi. Unasoma biology, geography, physics, math, general studies, etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…