Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Mwanzo nilikuambia Kuwa kwenye Hii Dunia huna unachojua ndo maana unapinga sana pasipokua na reason na inaonyesha kwa namna gani hufuaatili, Kuna baadhi ya Mambo hata Wana sayansi unao wamina wameshindwa kabisa kuyatatua wanabaki kunyamaza lakin ukweli Kuwa Haya Mambo yapo,, na kama wew na mtu ambaye huamini uchawi pengine nilitegemea uwe na sababu za kutosha kuthibitisha, na Kwa kulifanyia utafiti nenda hata huko vijijini ujionee mamb yanavyo endeshwa siyo kukurupuka hapa
Chukua link hii kaisomr hiyo ndege iliyopotea mpaka Leo Wana sayansi wanalifanyia utafiti bado hawajapata majibu The Mysterious Disappearance of Pan Am Flight 914 | Defensebridge
1. Defensebring sio credible source. Nataka BBC, Wikipedia, CNN, hivyo. Ndege tu ikianguka dunia nzima news. So niletee news source inayoeleweka hizi page hata wewe unaweza tengeneza.
2. 🤣Unajuaje sijaishi kijijini. Yaani we utaendelea kushift tu premise, Mara nikue, Mara niende Kijijini, Mara kiroho cjui. Mwishoni utasema nife ndo nitaona Kama watu wa dini wasemavyo.
3. Niambie kitu ambacho wanasayansi wameshindwa kuelewa na wakakaa kimya na kusema ni uchawi?
 
Hivi nikulize, Mfano mtu ambaye alikua masikini kabisa wa kutupwa na ni mtu ambaye unamfahamu kabisa let's say jirani maana jirani ni rahisi kufahamu life lake kwa sabab ya ule ukaribu mlionao, Sasa huyo mtu unajua kazi zake jinsi zilivyo anazo piga,,,,
Ghafura unashangaa huyo mtu anafanikiwa ananua magari anajenga majumba ya kifahari kazi anayo fanya haiendani na anacho ki project,, je hapo unaweza amini Kuwa uchawi au ni kazi??
Secondly unamini Uganga wa kenyeji?
Third unamini Kuwa Freemason ipo?
Naomba majibu yako
1. Kusema kwamba ni uchawi ni wivu wa maendeleo na uvivu wa kufikiria. Ili upate majibu mfate akuulize, maisha hayana formula. Wengine wanatumia miaka 10 wengine siku 2. Bado hujaprove uchawi.
2. Waganga wa kienyeji wapo kazi yao ni tiba asilia.... Sioni shida hapo
3. Freemason society ipo na majengo yake yapo, Ila wasemayo kuhusu freemason na makafara sijui shetani ni uwongo na Hamna ushahidi wa Hilo.
 
Kwanza toka mwanzo hoja yangu ni kwamba kwenye kufanikiwa wakati mwengine ni zaidi ya kufuata kanuni na kufanya kazi kwa juhudi, huo ndio msimamo wangu. Na wala sijasema kwamba kufanikiwa na kutofanikiwa basi lazima uchawi tu ndio unahusika.
Sawa ndo maana nimesema factors zipo nyingi ila none of them ni uchawi
 
Tuelezee hilo jambo kiscience chief,

Ilikuaje akawa kichaa
We jamani si umesoma ubongo au...si unajua psychology, mental problems na Nini. Sasa unauliza Nini, so ukichaa nao ni uchawi jamani. Si kusingekuwa na milembe. Au milembe Kuna waganga na wachungaji tu kule wanaombea.
 
Mkuu mbona matukio ya kutapeliwa na kuibiwa pia yapo, wewe umetaka yenye kuhusu uchawi ndio nimekutajia hilo la chuma ulete. Hata wanaoiba simu huku mtaani wanachomwa moto ila wanasiasa wanaoiba mabilioni hawaguswi.
🤣Ndo mtu akiibiwa anasema chuma ulete ni excuse. Siku hizi sio lazma ukabwe. Mjini watu Wana tactics nyingi Sana mpaka kuja kukuibia. Ndo maana nasema ni mchezo wa akili sio uchawi. We unasema uchawi kabla ya kuelewa. Ukielewa unacheka tu unakubali umepigwa bac ndo maisha, mi mwenyewe yashawahi nikuta so naelewa
 
Miaka fulani nikiwa chuo nilienda field kijiji fulani huko Dodoma. Sehemu niliyokuwa nafanya field ilikuwa nje kidogo na sehemu yalipo maduka. Sasa siku moja nilikuwa napita njiani nikasikia watu wanaambiana "huyu kijana anapitaje hiyo njia usiku huu". Sikuelewa sababu ya wao kutokupita ile njia usiku

Sasa siku moja tukiwa watatu na jamaa zangu ninaofanya nao field, mida ya saa moja jioni kigiza giza ndio kinaingia. Tunawa tunavuka kuna sehemu kulikuwa na mto kwenye hiyo njia ila hauna maji. Sasa kwa mbele tukaomuona mzee mmoja aliyeonekana umri umeenda sana anatembea polepole kwenye ukingo wa pili wa mto, tulitegemea tukija kuibuka tutampita. Lakini tulipokuja kutokea hatukuona chochote.

Mwanzoni nilidhani nimeona peke yangu nikakaa kimya. Baadae tukiwa tumeshafika yule mshikaji nae akaniuliza kama niliona lile tukio. Mshikaji wetu mmoja yeye hakuona alikuwa yuko bizzy kuchati na simu muda tukio linatokea.

Tulishangaa sana maana ile sehemu haikuwa na mti wala kichaka cha kujificha ni eneo plain tu. Na ilikuwa ni kitendo cha sekunde chache sana, yule mtu kutokomea kabisa asionekane, hata ingekuwa gari ni lazima tungeikuta.

Sasa uniambie ilikuwa ni hallucination uone kama sijakuzabua makofi.
 
baki hivo hivo

Ezekieli 21:21
[21]Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huko na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini.

sio lazima ujue uchawi wa kutazama maini ukoje.
 
Mm nakushauri nenda google andika hiyo ndege iliyopotea usome habari yake then uje hapa,,
Alfu Kingine kama hutaki kuamini unasema ni Fiction,, hivi mtu anakwambia vita ya kwanz ilipigana wewe unaminije Kuwa hiyo vita ilikuwepo na wakat wewe hukuwepo isipokua tu unaisoma na wew unamini why usiseme hiyo ni habari, acha kuonyesha kwa jinsi gan kichwa chako hakifanyi kazi,, tarifa huwa zinarekodiwa kwa ajili ya kizaz na kizazi kama kumbukumb ya vizaz vijavyo basi kama hiyo huamini
Pole sanaa
 
Attachments

  • Screenshot_20230804-184846_Firefox.jpg
    Screenshot_20230804-184846_Firefox.jpg
    157.9 KB · Views: 10
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.

MKATABA WA DP WORLD UCHAWI UPO
 
Miaka fulani nikiwa chuo nilienda field kijiji fulani huko Dodoma. Sehemu niliyokuwa nafanya field ilikuwa nje kidogo na sehemu yalipo maduka. Sasa siku moja nilikuwa napita njiani nikasikia watu wanaambiana "huyu kijana anapitaje hiyo njia usiku huu". Sikuelewa sababu ya wao kutokupita ile njia usiku

Sasa siku moja tukiwa watatu na jamaa zangu ninaofanya nao field, mida ya saa moja jioni kigiza giza ndio kinaingia. Tunawa tunavuka kuna sehemu kulikuwa na mto kwenye hiyo njia ila hauna maji. Sasa kwa mbele tukaomuona mzee mmoja aliyeonekana umri umeenda sana anatembea polepole kwenye ukingo wa pili wa mto, tulitegemea tukija kuibuka tutampita. Lakini tulipokuja kutokea hatukuona chochote.

Mwanzoni nilidhani nimeona peke yangu nikakaa kimya. Baadae tukiwa tumeshafika yule mshikaji nae akaniuliza kama niliona lile tukio. Mshikaji wetu mmoja yeye hakuona alikuwa yuko bizzy kuchati na simu muda tukio linatokea.

Tulishangaa sana maana ile sehemu haikuwa na mti wala kichaka cha kujificha ni eneo plain tu. Na ilikuwa ni kitendo cha sekunde chache sana, yule mtu kutokomea kabisa asionekane, hata ingekuwa gari ni lazima tungeikuta.

Sasa uniambie ilikuwa ni hallucination uone kama sijakuzabua makofi.
Hallucinations....🤣ungetaka kuaminika ungerecord
 
baki hivo hivo

Ezekieli 21:21
[21]Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huko na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini.

sio lazima ujue uchawi wa kutazama maini ukoje.
🤣🤣🤣🤣 Nimekuambiaje hiki kitabu kina makosa mengi kuliko gazeti la Jana. Soma post yangu ya #653 utaelewa. So this isn't evidence, ni kama story nyingine tu unanihadithia
 
Kwahyo kauli yako ya mwanzo kwamba wazungu hawaamini uchawi unaifuta???

Ni elimu ipi unayoiongelea ambayo unahisi watu wakiipata wataacha kuamini kuwa kuna uchawi?
Ya shule tu... kwani shuleni unafundishwa kitu chochote kuhusu uchawi. Unasoma biology, geography, physics, math, general studies, etc
 
Back
Top Bottom