2017
Nimetoka hasubuhi naelekea miangaiko k/koo njiani kuelekea kituoni kupanda gari, nasimamishwa na dogo mmoja ambaye najuana naye palipokuwa mtaani tulipokuwa tunaishi
Dogo akaanza kunilalamikia kuhusu dogo mwenzake ambaye aliweka nae share kwenye biashara fulani, na biashara ilikubali sanaa , hiyo biashara waliyokuwa wanafanya.. walikuwa wanatoa matunda baadhi ya vijiji vilivyokuwepo karibu na dar na kuya supply katika supermarkt walisajili kabsa kampuni yao, aisee walikuwa wanakimbiza hatari
Dogo akawa ananiomba nikaongee na huyo mwenzake ambaye wameshare biashara, malalamiko yake kuwa huyo jamaa anamroga Kwa kigezo cha kutaka kumdhurumu pesa na biashara kiujumla, nikamuhoji sanaa dogo licha yakuwa nilikuwa nachelewa miangaiko,nilimuhoji kuwa kajuaje kama anarogwa akanielezea kuwa mama yake ana ostaz wake kuwa kila mwezi anakuja kumuombea dua mama yake na nyumba yao kiujumla kuwa yeye ndio kawaambia, nikamuuliza umechukua hatua zozote
Akanambia kuwa mama yake alijaribu kumtafuta jamaa akakataa kwenda, wakaamua kumpigia sim na kumwambia akakataa kuwa hafanyi hivyo
Akanambia ameona kuwa mimi vijana wengi wananiheshimu na kunifata kwa ushauri na nimewazidi kidogo tu umri ingekuwa rahisi kuyamaliza matatizo yao
Nikamuuliza kuwa yeye anatakaje, akasema anataka kama apewe share yake na amuache aendelee na biashara, kwa maelezo yake dogo walikuwa na kama m12 kwenye account yao ya biashara
Kiukweli nilijaribu kumtafuta yule dogo mwenzake na alikataa kuwa hajaweka share na mwenzake huyo aliyokuja kuniomba nikaongee naye, nikamtafuta dogo na kumuelezea alibaki kulia tu na kunambia bro jamaa ataniua
Sasa ni 2023, roho inaniuma sanaa nilipata kwenda hapo mtaani mwanzoni wa mwaka huu, nimemkuta yule dogo aliyekuja kunilalamikia kuwa anarogwa ni chiz kabsa wallah nililia machozi kama mtoto mdogo nilihisi nna tuhuma Kwa Mwenyezi Mungu
Kibaya zaidi kanikumbuka na akiwa akinikuta njian ananisimamisha tunaongea vizur tu na tukimaliza maongezi ananiomba pesa, huwa nampa niliyokuwa nayo
Hakika Mungu atatulipa kwa chochote tutachowafanyie wengine