Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Ni wachache Sana ambao hawana elimu. That's the point..kwani point yangu ni kwamba hamna mzungu anayeamini ujinga. Wapo kibao ila ni wachache compared to us kwa sababu jamii zao zimeendelezwa kisayansi na kielimu
Ndio maana nikakwambia nikutajie vitabu vya wazungu vyenye kuelezea uchawi na mambo mengine ambayo wewe huyaamini kisha uniambie kuwa hao waliyoandika hivyo vitabu ni katika hao wazungu wachache wasio na elimu au wana elimu?
 
Naomba unipe reference ya kamusi gani inayoelezea hiyo maana ya uchawi?
Mimi nimejaribu ku compare watu wawili ambao wanakwenda wote kazini, wanalipwa Sawa na bado kuna mmoja anamzidi mwenzake.
Mmoja yupo radhi kumaliza mshahara wake kwenye pombe ILA mwingine yupo radhi ajibane akanunue kitu kitachomazilishia zaidi.

Naomba nipe maana ya uchawi uliyoitoa hapo umeipata KWenye kamusi ipi?
means ulikuwa unaona, ameshindwa kwa sababu ya ulevi na kukata taama. 😁 sisi tutakwambia yasikukute. Ukisema hapo uchawi upo wapi, unataka uone kama hesabu x+y=z
 
unajuwa hata baadhi ya hoja za kisayansi bado ipo kwenye imagination, means imeshindikana, mfano mtu kuzeeka

Kwani cellular damage na genetics mkuu zacc siumesema?
Mimi si mtaalamu sana wa hayo mambo lakini mbona yashaelezwa.

Au na wewe ndo wale wale pacific na antlatic maji hayamix mkahitimisha ile ni uwepo wa mungu? Wakati sababu za kisayansi zinaeleza.
Mkuu mbona hivyo vitu vinaelezwa vimejaa mitandaoni carolina TED TALK pale utakuta vijana toka mpaka africa wenye mawazo constructive
 
Ndio maana nikakwambia nikutajie vitabu vya wazungu vyenye kuelezea uchawi na mambo mengine ambayo wewe huyaamini kisha uniambie kuwa hao waliyoandika hivyo vitabu ni katika hao wazungu wachache wasio na elimu au wana elimu?
kwani sayansi yenyewe imetoka wapi, si wa wazungu, huyo jamaa anabishia asili
 
Ndio...sleep paralysis...jinamizi. imenitokea first hand na watu wengi husema sijui jini linakukaba mpaka umtaje Yesu sijui Allah. Ila in real sense ni concept ya biology inayohusisha brain, nervous system na muscles. Ndo maana nasema una mitandao vitabu watu wenye elimu mbalimbali, tafuta majibu yanayoeleweka sio kila kitu ambacho huelewi unasema tu ni uchawi...it's too easy
Hicho ndio ambacho pekee umeweza kuelezea kuhusu uchawi pamoja na kuishi kwako kwenye jamii yenye kuamini uchawi?
 
Kwani cellular damage na genetics mkuu zacc siumesema?
Mimi si mtaalamu sana wa hayo mambo lakini mbona yashaelezwa.

Au na wewe ndo wale wale pacific na antlatic maji hayamix mkahitimisha ile ni uwepo wa mungu? Wakati sababu za kisayansi zinaeleza.
Mkuu mbona hivyo vitu vinaelezwa vimejaa mitandaoni carolina TED TALK pale utakuta vijana toka mpaka africa wenye mawazo constructive
Sawa, science tells us a lot about cellular damage but has nothing to do with cellular damage, why? Means kuna higher power than science ambayo binadamu hajafika, unakubaliana na mimi!
 
means ulikuwa unaona, ameshindwa kwa sababu ya ulevi na kukata taama. 😁 sisi tutakwambia yasikukute. Ukisema hapo uchawi upo wapi, unataka uone kama hesabu x+y=z

Mimi siwezi sema moja kwa moja sababu ya ulevi maana huenda ikawa ni fundamental attribution theory.
Ila yeye ndani ya wiki mbili mshahara umeisha na anarudi kumkopa mwenzake. sasa kama pombe, wanawake na bado ana pikipiki anayoenda nayo kazini hizo stori za uchawi wata assume wengine kwangu ni matumizi makubwa zaidi ya anachoingiza.
 
mimi nilitongoza pisi kali TANGA barabara ya 11,nikaenda nae nyumba ya wageni,wakati namwingilia {tulikuwa tumezima taa} nikahisi harufu kali ya mbuzi na ikawa kama nimelalia sufi,nikachoma fasta kuwasha taa nikaona mbuzi kalala kitandani alaf nikasikia bonge la sonyo kutoka darin,nilivaa nguo suruali bila chupi nikatoka nduki kifua wazi!!.....kaunta alibaki kushangaa,mlinzi nae akabaki kunsema,,,hii ndo tanga bhana lazima "jamaa kakutana na kioja"
😂😂😂
 
Sawa, science tells us a lot about cellular damage but has nothing to do with cellular damage, why? Means kuna higher power than science ambayo binadamu hajafika, unakubaliana na mimi!
Something which science yet to investigate it doesn't mean we fix that gap is witchcraft or god.

Je ushawahi soma Enmenkar and the lord of arrata?
Hawakuamini kwamba tujenge mnara unaofika juu mawinguni tukamuone mungu wakiamini mungu yupo juu mawinguni? Hilo gap la knowledge walilokuwa nalo linathibitisha mpaka sasa mungu wa kutungwa yupo mbinguni?
Sijui unaelewa lakini mkuu?
 
Rekebisha hakuna mafanikio yenye uchawi kwa namna yoyote ile as long as huyo mtu tayari anafanya kazi
Ondoa "hakuna sehemu niliposema mafanikio ni uchawi tu"
sababu neno uchawi ni stori za kufikirika za miujiza.
Wanaofanya kazi ni wengi sasa usitake kutuaminisha kwamba kufanya kazi tu ndio kufanikiwa wakati kiuhalisia haipo hivyo, wewe jamaa ndio unataka tungelee vitu nje ya uhalisia.

Hakuna mafanikio yenye uchawi as long as huyo mtu anafanya kazi, ila asiyefanikiwa pamoja na kufanya kazi ndio unataka tufikirie sababu za zaidi ya kufanya kazi tu ndio hufanya asifanikiwe.
 
2017

Nimetoka hasubuhi naelekea miangaiko k/koo njiani kuelekea kituoni kupanda gari, nasimamishwa na dogo mmoja ambaye najuana naye palipokuwa mtaani tulipokuwa tunaishi

Dogo akaanza kunilalamikia kuhusu dogo mwenzake ambaye aliweka nae share kwenye biashara fulani, na biashara ilikubali sanaa , hiyo biashara waliyokuwa wanafanya.. walikuwa wanatoa matunda baadhi ya vijiji vilivyokuwepo karibu na dar na kuya supply katika supermarkt walisajili kabsa kampuni yao, aisee walikuwa wanakimbiza hatari

Dogo akawa ananiomba nikaongee na huyo mwenzake ambaye wameshare biashara, malalamiko yake kuwa huyo jamaa anamroga Kwa kigezo cha kutaka kumdhurumu pesa na biashara kiujumla, nikamuhoji sanaa dogo licha yakuwa nilikuwa nachelewa miangaiko,nilimuhoji kuwa kajuaje kama anarogwa akanielezea kuwa mama yake ana ostaz wake kuwa kila mwezi anakuja kumuombea dua mama yake na nyumba yao kiujumla kuwa yeye ndio kawaambia, nikamuuliza umechukua hatua zozote

Akanambia kuwa mama yake alijaribu kumtafuta jamaa akakataa kwenda, wakaamua kumpigia sim na kumwambia akakataa kuwa hafanyi hivyo

Akanambia ameona kuwa mimi vijana wengi wananiheshimu na kunifata kwa ushauri na nimewazidi kidogo tu umri ingekuwa rahisi kuyamaliza matatizo yao

Nikamuuliza kuwa yeye anatakaje, akasema anataka kama apewe share yake na amuache aendelee na biashara, kwa maelezo yake dogo walikuwa na kama m12 kwenye account yao ya biashara

Kiukweli nilijaribu kumtafuta yule dogo mwenzake na alikataa kuwa hajaweka share na mwenzake huyo aliyokuja kuniomba nikaongee naye, nikamtafuta dogo na kumuelezea alibaki kulia tu na kunambia bro jamaa ataniua

Sasa ni 2023, roho inaniuma sanaa nilipata kwenda hapo mtaani mwanzoni wa mwaka huu, nimemkuta yule dogo aliyekuja kunilalamikia kuwa anarogwa ni chiz kabsa wallah nililia machozi kama mtoto mdogo nilihisi nna tuhuma Kwa Mwenyezi Mungu

Kibaya zaidi kanikumbuka na akiwa akinikuta njian ananisimamisha tunaongea vizur tu na tukimaliza maongezi ananiomba pesa, huwa nampa niliyokuwa nayo

Hakika Mungu atatulipa kwa chochote tutachowafanyie wengine
Sasa uyo ostaz aliemwambia anarogwa kwanini hakumtibu?
 
Kwanza nimeomba maana ya uchawi uliyosema umeitoa wapi hujaniambia.

Pili mekuonyesha watu na mifano wote wanafanya kazi.
Halafu In a simple way kama kila mtu anaweza kuya term mafanikio kwa namna yake point itabaki pale pale kufanya KAZI tu.

Nipe mfano wa mtu mmoja ambaye ana utajiri kutokana na uchawi?
Halafu nipe reference ya kamusi inayotoa maana ya uchawi uliyoitoa wewe?
 
Sasa uyo ostaz aliemwambia anarogwa kwanini hakumtibu?

Mambo ya kifamilia mkuu, mimi nimemkuta mtu kapagawa tu na sikuwa na msaada

Na hayo mambo yanazidiana nguvu chief ndio maana akawa anaomba msaada wa kimaongezi na jamaa

Jua kuna wataalamu wa sehemu tofauti tofauti so wengine wanaweza kutibu tu wengine wanaweza kuroga yaani ni fani tu na uwezo unakuaga tofauti
 
Pale mwanza lilipo jengo la NSSF kwa sasa kulikua na bibi anamiliki eneo hilo yule bibi alikataa kutoka eneo hilo kupisha ujenzi pamoja jitihada zote za kumubembeleza zilishimdikaana ikabidi watumie nguvu huwezi amini bulldozer, excavator, wheel loader zote zilishishindwa kuvuja nyumba ya yule bibi inakitoka huko ikiwa nzima ikifika pale inapata breakdown kufupisha story yule bibi walimkalisha chini na kumsihi sana ndio akakubali nnacho kwambia sio story ya kusikia nlikua Mwanza miaka hio kaulize hio story

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hii habari niliisikia hapo mwanza
 
Naomba unipe reference ya kamusi gani inayoelezea hiyo maana ya uchawi?
Mimi nimejaribu ku compare watu wawili ambao wanakwenda wote kazini, wanalipwa Sawa na bado kuna mmoja anamzidi mwenzake.
Mmoja yupo radhi kumaliza mshahara wake kwenye pombe ILA mwingine yupo radhi ajibane akanunue kitu kitachomazilishia zaidi.

Naomba nipe maana ya uchawi uliyoitoa hapo umeipata KWenye kamusi ipi?
Kwani maneno yote tunayotumia humu tumetoa tafsiri zake kwenye kamusi? Unataka kuniambia jinsi ulivyoeleza wewe uchawi umetoa kwenye kamusi? Mimi nimeeleza uchawi kwa jinsi navyojua unavyofanyika.

Kamusi niliyo nayo hapa inaeleza hivi kuhusu uchawi:ni ufundi wa kutumia dawa mitishamba au vitabu maalumu vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe.

Sasa kutoka kwenye hiyo mifano yako ndio unataka kuhitimisha kwamba wasiofanikiwa ni kwa sababu hawajinyimi na hutumia hovyo pesa zao? Na kumbuka sio kila mafanikio yanahusu mali kwamba upate pesa.
 
2017

Nimetoka hasubuhi naelekea miangaiko k/koo njiani kuelekea kituoni kupanda gari, nasimamishwa na dogo mmoja ambaye najuana naye palipokuwa mtaani tulipokuwa tunaishi

Dogo akaanza kunilalamikia kuhusu dogo mwenzake ambaye aliweka nae share kwenye biashara fulani, na biashara ilikubali sanaa , hiyo biashara waliyokuwa wanafanya.. walikuwa wanatoa matunda baadhi ya vijiji vilivyokuwepo karibu na dar na kuya supply katika supermarkt walisajili kabsa kampuni yao, aisee walikuwa wanakimbiza hatari

Dogo akawa ananiomba nikaongee na huyo mwenzake ambaye wameshare biashara, malalamiko yake kuwa huyo jamaa anamroga Kwa kigezo cha kutaka kumdhurumu pesa na biashara kiujumla, nikamuhoji sanaa dogo licha yakuwa nilikuwa nachelewa miangaiko,nilimuhoji kuwa kajuaje kama anarogwa akanielezea kuwa mama yake ana ostaz wake kuwa kila mwezi anakuja kumuombea dua mama yake na nyumba yao kiujumla kuwa yeye ndio kawaambia, nikamuuliza umechukua hatua zozote

Akanambia kuwa mama yake alijaribu kumtafuta jamaa akakataa kwenda, wakaamua kumpigia sim na kumwambia akakataa kuwa hafanyi hivyo

Akanambia ameona kuwa mimi vijana wengi wananiheshimu na kunifata kwa ushauri na nimewazidi kidogo tu umri ingekuwa rahisi kuyamaliza matatizo yao

Nikamuuliza kuwa yeye anatakaje, akasema anataka kama apewe share yake na amuache aendelee na biashara, kwa maelezo yake dogo walikuwa na kama m12 kwenye account yao ya biashara

Kiukweli nilijaribu kumtafuta yule dogo mwenzake na alikataa kuwa hajaweka share na mwenzake huyo aliyokuja kuniomba nikaongee naye, nikamtafuta dogo na kumuelezea alibaki kulia tu na kunambia bro jamaa ataniua

Sasa ni 2023, roho inaniuma sanaa nilipata kwenda hapo mtaani mwanzoni wa mwaka huu, nimemkuta yule dogo aliyekuja kunilalamikia kuwa anarogwa ni chiz kabsa wallah nililia machozi kama mtoto mdogo nilihisi nna tuhuma Kwa Mwenyezi Mungu

Kibaya zaidi kanikumbuka na akiwa akinikuta njian ananisimamisha tunaongea vizur tu na tukimaliza maongezi ananiomba pesa, huwa nampa niliyokuwa nayo

Hakika Mungu atatulipa kwa chochote tutachowafanyie wengine
Hili ni fundisho kwenu kwamba mtu akikueleza matatizo yake uache kujifanya MWANASAYANSI, na badala yake umsikilize kwa MAKINI na umpe msaada STAHIKI.
 
mimi niliona uchawi upo shule.. kulikua na mchupi mkubwa sana unaanikwa ijumaa kila tukitegea tuone anaeuanua tunamkosa

Siku moja bweni zima la SAMORA MACHEL tukasema hatulali mpaka tumuone anaeanua
Hauwezi amini sote tulipigwa na usingizi mzito wa pono
Mpaka namaliza shule pale Ile chup hatukujua ya nani
Ukiitazama sana mwili unasisimka
SIJUI LILIKUA CHUPI LA JINI SIZE YENYEWE TU HAIKUA YA KIBINADAM
Mwaka gani hii
😂😂😂🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom