Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Ulimwengu wa roho ni software huwezi kuuona kwa macho ya mwili wala kuushika kwa mikono yako...tusichanganye vinavyoonekana na visivyoonekana, tukafanya hiki ndio kile na kile ndio kile
-simu unayo na unafanya mawasiliano yote ninini kinafanyika mpaka umudu kufanya hayo yote?

Akili unayo na ukiulizwa hutabisha je ukiambiwa ionyeshe utaweza?
-Usingizi unao je kufumba macho ndio kulala usingizi?
Ni vema kuelewa kwama uchawi ni sehemu ya ulimwengu usioonekana, upo lakini hauna ithibati za kisayansi kwakuwa huwezi kuushika nk ....

Kuwepo kwa uchawi ni kitu cha kwanza lakini kuwepo na mtu akaweza kuutumia huo uchawi kwa muktadha fulani ni kitu kingine kabisa
Malumbano mengi pia yametokea kwenye kutaka ithibati za kuwepo kwa uchawi! Hizi ni fikra tengefu..

Kama ilivyo nguvu iliyopo kwenye mashine yoyote ana mwanga kwenye taa yoyote ama software kwenye kifaa chochote cha kielectronic...kama ulivyo uhai ndani ya mwili
Tafakari....
By Mshana Jr
Vitu vyote ulivyotaja vina mwanzo na mwisho, vinadhibitika, vinapimika, na vinaweza kuwa controlled. Simu usingizi akili, etc, akili ni activity za ubongo ukitoa ubongo we huna akili huna usingizi pia...na huna maisha. Kama unabisha toa ubongo. Software kama za Simu tunaziona na tunaweza tumia kuzifuta kuzitengeneza na kuziharibu. Uchawi is not provable in any form. Hata bacteria hawaonekani kwa macho mpaka watu wa dini walijua magonjwa yote ni mapepo tu Sayansi ikagundua microscope saa hivi tunaona Nini kinasababisha magonjwa. Hoja yako haina mashiko jaribu Tena. Na ulete proof ya uchawi vitu vyote ulivyotaja vina proof, watu Wana ubongo ndo maana Wana akili, ukiharibu ubongo wako umeharibu uwezo wa kufikiria...watu Wanalala na pia upepo upo na unapimika pressure as well as speed by science. Pamoja na uzito pia ndo maana tunaweza nunua gesi na kujaza matairi. Prove uchawi upo
 
Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).

Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.

Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.

Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.
Hii uliielezea kwenye story yako ile ambapo yule big wa mafinga alikua anaku search baada ya kutompa chake kwenye mbao ulizozulumiwa na yule mzee tapeli🤣.. Naikumbuka sana ile story yako mpaka mkaenda hadi makaburini.. unaskia vitu vinachoma choma tu🤣🙌
 
Mtu anakwambia kabisa kuwa huko wenzetu waliwauwa wachawi hivyo kiasi kikubwa wakatokomeza uchawi na kukaja kuzaliwa kizazi ambacho hakijihusishi sana na uchawi, sasa hapo wanataka tuone et wazungu hawaamini uchawi kwa sababu tu wana elimu. Watu wanarogana na kutibiana afrika halafu mtu anakuja anataka uwe na mitazamo kama ya wazungu na kupinga tu hakuna uchawi kisa wazungu hawaamini uchawi.
🤣🤣🤣Umeona upumbavu wako...huna ushahidi huwo... wenzetu nakuambia wamejenga hoja za logic na science hawawezi amini story story za hapa na pale bila uthibitisho..tofauti Yao na sisi..wewe mbongo ukiskia sijui jini kafanya Nini wapi..coz jamii yako ni ignorant na superstitious hutabisha..Ila wenzetu watafuatilia watakufa chanzo sio jini. Yaani wenzetu wanaenda kutafuta majibu bila kuwa na jibu kichwani, we unaenda na jibu la ushawi so ur conclusion tayari ushamake so ukiona kitu tofauti unakipotezea coz inakinzana na jibu lako, that's not science it's superstitious
 
Mkuu naomba nikuambie kitu

Kwangu uchawi naweza kukuambia ni miujiza/magic/maajabu/mazingaombwe yani sioni neno linalofit

Alafu niliona kama umesema wazungu hawaamini uchawi ushawahi kuangalia American Got talent?? Mtafute mdada anaitwa Riana

Kingine inawezekana cicre yako pia au hujatembea...

Tuliosoma shule za bweni wengi Tushaona/Kusikia vitu vingi vya kutisha miss corridor,Mtu mrefu ambae mwisho humuoni,Vimbilikimo... binafsi sitapenda kuviongelea kwa upande wangu maana hata nikikuambia hutaamini na najua hutaamini kwasababu haukuona wewe
Miss corridor hata ukimgoogle utamkuta na inajulikana ni story za kichawi za shule za kiafrika. Ni kitu kinajulikana to be just horror stories. Jiulize why kitu uone mwenyewe. Hamna mtu atakubishia unaona jua. Ila ukisema unaona jua limekuwa pink, wakati wote tunaona njano obviously u r crazy
 
Shule za kusomea ujinga hizo.
Kuna tofauti ya jamii yenye watu wenye elimu na yenye watu duni. Dar na rukwa, Kilimanjaro na shinyanga, kagera na lindi. Niambie mikoa gani inaongoza kwa watu wenye elimu na uchumi mzuri na niambie mikoa gani Inaongoza watu wenye Imani za kishirikina. Umeona pattern hio. Ndo hivyo the higher ur education the less unaweza amini ujinga.
 
Hawa wanaojiita wanasayansi waliosoma haya mashule ya kata ya KIKWETE ni watu WAJINGA kuliko mtu yeyote.
Nimesoma shule kubwa maisha yangu yote sio kila mtu maskini Kama wewe jiheshimu...watu wengine sio lazma wataje historia zao kwa sababu huu ni mtandao huru, ni maamuzi yangu kutaka au la
 
Mimi Iko hivi ila mpaka Leo sijui ni mauchawi au Nini huko Moshi vijijini!

Kipindi Niko around 12 Mimi na machalii zangu tulikua na tabia ya kuiba parachichi nyakati za usiku kwa lengo la kuuza siku ya soko kujipatia shilingi mia Tano au buku mbili!

Lengo lilikua kupata pesa ya daftari,kalamu,soksi wali nyumbani na extra pro max mandazi!

Tulikua watatu tunaamka usiku saa mbovu (tulipendelea nyakati za mbalamwezi tuone vizuri) mmoja kazi yake ni Kuokota parachichi, mwingine kujaza kwenye kiroba alafu mwingine ni Mimi msoma gepu(anayeangalia usalama)

Iyo siku sitasahau tulivuna parachichi za kuzidi,nakumbuka kulikuwa na mbalamwezi (full moon) kutizama kwenye Ile nyumba tunayoiba parachichi niliona kitu kirefu cheupe kimechongoka juu kama mshale kinatufuata huku kikiyumba na kilikua kama kinabadilika rangi za bluu!

Nilichofanya Sasa nilikimbia na wale machalii wote walikimbia kivyao!

Tulikutana uwanja wetu asubuhi hio hio,Kuna alie umia na miba mwingine kapoteza ndala!

Mpaka Leo hii sisi ni madingi tukiwa tunakula bia nikiwakumbusha wanacheka tunajikuta tunaagiza bia zingine
Hallucinations
 
Watakwambia hiyo kama movie tu zinatengenezwa.
Angalia kitu kinaitwa breaking the magician code. Afu utaelewa hizi magic tricks zinafanywaje. Ingekuwa uchawi unadhani wangebaki pale. Ile ni entertainment ni Sanaa kama nyingine, sio wajinga wale Kama wewe.
 
Binafsi siwakatalii...Kuna vitu kama hujavishuhudia ni vigumu kuamini

Ila tatizo lao ni kujihisi wanajua pale ambapo hawajui kama hawajui

Maana halisi ya watu wa dizaini hii tunawaita wajinga
🤣🤣🤣we ndo mjinga, ukiona kitu Cha uwongo afu we peke yako we ndo chizi sio sisi. Nenda kagale gale kwa mwamposa kabisa mwambie una mapepo
 
Kama Kuna mtu haamini uchawi..simply inbox me ,kwa nauli yangu ntakutoa huko ulipo ili twende nikakuoneshe uchawi
Sina mda. Kama una evidence of it tuonyeshe... Usalama wangu na mda wangu it's more important
 
'Havipo kimwili'. Kwa phrase yako hii ndio sasa usimkatalie mtu aliyeona kitu ila si kimwili, wewe utasema hallucinations (psychology), mtu wa faith atasema maoni ( vision). Tofauti ni kuwa kuna watu vitu hivyo huwavuta katika hatari inayoonekana kimwili ila sababu haionekani kimwili (ndo wengine husema uchawi). Hallucinations unasikia, unaona au unasikia harufu ya vitu ambavyo havipo kabisa na huingii hatarini mpaka ufahamu wako urudi.
Wasemao juu ya uchawi ni pale hali hiyo (isiyoeleweka kwa nje) inakutia kwenye kiwewe mpaka hatari ( dereva anasema yupo speed ktk eneo analolifahamu siku zote hakunaga watu, ila ghafla mtu anakatiza barabara, kumkwepa ni kutengeneza sababu ya nje ya ajali na vifo. Wenye uzoefu wanasema amua kugonga tu). Na kwa kuwa hallucinations hazipimiki kwa nje, inawezekana kabisa kuwa hata hallucinations ni uchawi pia maana vyote sio ktk ulimwengu huu wa mwili.
Ulimwengu wa mwili kivipi...Kuna ulimwengu mwingine kwani?
 
Sijakukatalia na ni kweli sayansi inakupa sababu ya wewe kuwa ktk hali hiyo ( msongo wa mawazo, hofu isiyodhitika/ anxiety, sonona, upweke nk) ndio maana mtu anaweza kusikia sauti ikimsemesha na akajibu, mtu anaweza kuona picha ambayo haipo na akaduwaa au kuifata lakini ghafla hali hiyo hupotea ( like sleep walkers), japo cerebral malaria nayo huleta hali hii ila uchawi unapitiliza haya, mfano wa ndugu wa mwenge (watu huku nje wanaona anakaribia hatari ila yeye anahangaika ni mtu ambaye wengine hawamuoni).
Mimi nina rafiki alinisimulia kuwa wakati anaendesha bike ghafla sauti yenye nguvu ikwamwamuru rukaa! Pasi kujiuliza akaruka upande wa nje ya barabara harafu akaona ni kama kuna mtu amemdaka. Ile kutua chini bike yake imeharibika kwa kugongwa ila watu wakasema ni gari imekutupa nje. Sasa anajiuliza gari ilikuwa nyuma haioni, nani alimwambia ruka? Nani alimdaka nk, maswali haya sayansi itaishia kusema ni hallucination ila watu wa faith watavuka mpaka na kusema is about God or devil.
Why is faith good?
 
Nilikuuliza wote wasiofanikiwa na wanafanya kazi ni kwa sababu ya kutojinyima na kutumia hovyo mishahara yao kama hao uliyowatolea mifano? Ili tujue kwamba wote tukifanya kazi halafu tukafuata kanuni ya kujinyima basi wote tufanikiwe kama hao polisi.

Huko nyuma niligusia kitu kuhusu nyota kung'aa au tuseme mvuto kwa maana unaweza ukawa ni msanii mzuri unaimba vizuri ila hauna mvuto haukubaliki kwa watu au ni mwanasiasa ila hauna mvuto kwa watu, hivyo ni vitu ambavyo vipo na vikikosekana kwa hao watu wawili vinaweza kufanya kushindwa kufikia mafanikio kwa hao watu aina mbili. Kwahiyo uchawi unaweza ukatumika katika mazingira kama hayo ili kupatikana huo mvuto ambao utasaidia katika kazi zao.

Uchawi pia hutumika kwenye biashara katika hali ya kuvuta wingi wa wateja, haya mambo yapo tunaishi nayo kwahiyo hivyo ndivyo uchawi unavyotumika nimeona nikuelezee kwanza.
How do u know that? How do u prove that? Mbona it seems lyk uchawi is just an excuse. Mtu hajafanikiwa wenzake wamefanikiwa..hoo ni uchawi. It's a dumb excuse ndo maana hatuendelei wenzetu washakua kifikra
 
Tatizo hawa jamaa wao wanaangalia mambo kwa upande mmoja tu na wamejifunga hawataki kabisa kusikia nje ya wanachoamini, wapo radhi wakwambie hilo hatujui ila sio uchawi,jini au Mungu.
How do u know we haujajifunga katika kuamini uchawi? Mbona unanikamia Mimi wakati u doing the same? Je nimebisha kwamba hamna jua? Coz I see it. Nimebisha kwamba joe Biden exists? No, coz hata Kama sijawahi kumuona ila Kuna extraordinary evidence that he does exist. Why niamini kitu ambacho hakina uthibitisho wowote independent zaidi ya story tu za mtu kutokana na kutoelewa kwake
 
Back
Top Bottom