passion_Amo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2023
- 378
- 542
Wewe unadai hakuna kabisa uchawi na chuma ulete ni katika aina za uchawi unaozungumziwa sana tu, sasa elezea hiko kinachoitwa chuma ulete kuwa si kweli kwamba ni uchawi kama inavyoaminika. Tumie hiyo elimu yako kunieleza mie nisiokuwa na elimu kwamba ni vp huko watu(wasio na elimu) kuona kupotea kwa hela na kuhusisha na uchawi kuwa si uchawi bali ni nini hasa.
Ok ngoja tukuulize swali rahisi maana unahangaika
Chuma ulete ni stori za kutungwa kwamba mtu anaichukua pesa kwa njia za maajabu
Ok, kwanini chuma ulete wasiende bank kuchukua pesa nyingi zilipo?
Unafikiri ingekuwepo mechanics hiyo wangapi wangekuwa matajiri?
Thibitisha hoja yako kwa kutuonyesha mtu aliyefanikiwa kwa chuma ulete au uchawi?