Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Jamani kama huamini uchawi upo embu tulia basi usiharibu uzi.Kutwa kushupalia kila story ya kila mtu alf mtu mwenyew unakuta kazaliwa mjini na kakulia mjini ila unavyokomaza shingo utadhani unajua kila kitu.Huamini tulia hulazimishwi acha watu waandike story zao mnaharibu uzi!
Yeyote asiyeamini uchawi upoo ujue Hana Mungu...
Vitabu vya dini zote mbili kubwa zimetaja uchawi Sasa kama Mtu haamini ujue huyo Sio Muislam Wala Christian
Kubisshana nao ni kupoteza muda tu
 
Natoa my own expirience , siuiti uchawi Ila the practise of dark and white magic mbona ipo tu.
Nina muda wa miaka takriban 10 nikideal na goetic demons ,using goetic magic.
Na ndio spirit anaitwa vizuri tu ndani ya duara (pentagram) ,kufuata nyiradi fulani na anakuja vizuri .
And no sio freemasonry, wala sio illuminati ,wala sio hallucinations . Unatumia majina takatifu ya mungu kuwashurutisha forcefully and they perform some but not all you require ,Kuna kanuni nyingi siwezi zungumzia.
Wanao itisha dhibitisho mambo haya wanaofanya wengi hadharani hawawezi including myself zungumzia Ila yapo ,much of these things watu wakiona ukifanya wanaweza kukuita shetani n.k
Ila the magical system can be manipulated kufanya uchawi .
Na ndio yanafaida kulingana na matumizi.
 
Nimekutumia video dr richard sambaiga, cristine noe palanjo BADO wanaogea umebisha nimekutumia article toka daily news wakiwa quoted walichoongea BADO unabisha


Nilikwambia wewe ni scammer kubali.

Tutatoa elimu msiendelee kuwaibia watu.
Article na daily news wapi na wapi?. Haya hiyo article ethnography imefanywa muda Gani na methodology ilikuwa ipi wakati wanaenda kuifanyia tafiti?
 
We jamaa unakua mgumu sana sabab hujajiandaa kuelewa. Uchawi upo... Ukikaa umaskinin ndo utauona mana maskini Wana vita za wenyewe Kwa wenyew. We ukitaka uaminif nenda umakondeni huko ndo utakuja hapa kusema neno.
Mana hujawahi kukutana nao ndo mana huamini. Ni kama mungu tu
🤣🤣🤣 Nijibu swali...why uchawi unachagua watu ambao ni maskini na wajinga? Yaani me mpaka niwe maskini na mjinga ndo nitaona uchawi..it shows clearly haupo ni imagination
 
Hata Yesu kutembea juu ya maji fizikia inakataa, Musa kugawa bahari sayans inagoma pia. Kufunga siku 40 bila kula kunywa chochote sayans inagoma. Yesu kupazwa angani inakataa pia. Aloo

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
😂😂😂😂Una uhakika alifanya hivi vitu...mbona hamna ushahidi nje ya Biblia kwamba hivi vitu vimetokea.. nikikuambia na Krishna alizaliwa kwa bikra na alifufuka je. Na Krishna kaja kabla ya Yesu Sasa...zote ni story tu za mababu
 
🤣🤣🤣 Nijibu swali...why uchawi unachagua watu ambao ni maskini na wajinga? Yaani me mpaka niwe maskini na mjinga ndo nitaona uchawi..it shows clearly haupo ni imagination
That's not manticized in such way. Maskini sio wajinga. Uchawi unaendana na husda yan wivu wa kimaisha na kupinga maendeleo. Class la matajiri hawana muda wa kukuonea husda sabb Wana vyao. Wew ukitaka kujua upo au haupo.... Kaishi MTWARA NA WAMAKONDE
 
Watu waliofanyia research uchawi wapo.. chuo kikuu Cha Daresalaam kimefanya tafiti hzo. Na uchawi upo wa aina KUU mbili. Upo unaohusisha object za mtu husika kama Uzi wa nguo anazovaa, nyayo nk. Kuna mwingine wanakutengezea object yenye kiumbo Cha mtu na kukitaa jina lako. Wakikivunja mguu na wewe unavunjika.
Yupo lekcha Udsm aliwahi kuanguka na ungo shinyanga akifanya study za kiethnografia na wachawi
😂😂😂Sawa naomba unitumie research Yake hapa wote tuisome... until then ni story za mtaani tu
 
Uchawi unazuaga taharuki mana unaonekana kikwazo Cha maendeleo ngazi ya mtu mmoja mmoja. Mbona hata ulaya witchfinder walikuwepo. Watu waliuana sana na wachawi walisakwa kama njegele... Uchawi upo wakuu
Ndio...ulaya walikuwa wanachoma wabibi wanaohisi ni wachawi...😂ila waliacha, why, coz wameelimika hamna uchawi...😂😂😂Sasa wewe sema tu walikuwa, ni zamani 1600s 1700s, now wameendelea kifikra ndo maana hawaamini uchawi
 
Mara kibao nasema kuwa wazungu(jamii ya waliyoelimika) wana vitabu vingi vyenye kufundisha na kuelezea uchawi na wana elimu tofauti na sisi.

Unalijua hilo?
😂😂😂Hata wewe unaweza kuandika kitabu Cha mashoga ila haimaanishi bongo inasapoti bongo..kule Kuna uhuru ukitaka uwe atheist sawa satanist sawa mlokole sawa mshirikina. Ila majority of them hawaamini uchawi, na research zimefanyika. Except america coz america Kuna watu wengi wa background tofauti Asia, Africa, Europe, south America etc so hivyo.. lakini countries Kama Sweden France wanaoamini uchawi ni wachache Sana..we umepata vitabu coz of course vipo Ila haimaanishi ndo majority view ya jamii Yao...😂elewa bac
 
Huyu utabishana nae tu. Wazungu wenyewe wanaomuaminisha huyu kuhusu uwepo wa sayansi uchawi wanaujua na uliwasimbua sana miaka hiyo.
Wafalme waliajiri watu wasake wachawi mitaani na kuwaua. Mana uchawi na maendeleo haukai sehem moja
😂😂😂😂😂Acha kurudi nyuma...hata wewe ulikuwa hujui mvua inasababishwaje, hujui dunia inazunguka jua, hujui radi inasababishwaje, so for a tym ulijua ni miujiza, Mungu au wachawi ila now si una elimu...Sasa mi nimeongolea mwaka 1200 au 2023...😂Acha kujikosha bac
 
Sikulazimishi uamini au usiamini ila nacho weza kusema tu ni hv achana na post zangu coz kubishana naww siwez na kila mtu anaiman yake
😂Ndo usitupangie Sasa...wewe Kama huelewi nature.. huelewi biology..usitutishe kwamba ni uchawi..ni ukosefu wa maarifa
 
Back
Top Bottom