Daaah sema imani ni kitu cha ajabu sana ukiishaamini tu huwezi tena kutoamini.
Mimi sio mwandishi mzuri ila nina kisa cha kushea nanyi.
Mwaka X niko zangu shule ya bweni(wavulana tupu)sasa kulikuako na mwenyekiti wa casfeta (Nothing personal) alikua kila jumapili baada ya kutoka kanisani lazima apite kila bweni kutoa mahubiri watu wampokee yesu na vitu kadha wa kadha kuhusu kumjua Mungu.
Na jamaa ni moja ya wale watu wanaonena kwa lugha yaani kifupi alikuwa wa moto sana, na sio mtu wa mambo mengi.
Sasa wapuuzi huwa hawakosekani wakasema tutajuaje kama jamaa ana nguvu kweli za kiroho? Kuna mpuuzi mmoja akasema ni rahisi tutamjaribu, wengine tukauliza kivipi jamaa akasema walokole si wanakemea mapepo na kila kitu basi tutamletea pepo au jini watu wakacheka sana.
Basi jamaa kuona watu wanacheka akasema jumamosi ya wiki ijayo kazi ndo itafanyika, na jamaa alikua ni mkazi wa kule shule ilipo so kila weekend anaweza kwenda nyumbani, basi bana Ijumaa ikafika akaenda nyumbani kwao akarudi jumamosi jioni na miguu ya mbuzi sijui alitoa wapi, basi mipango ikapangwa kwamba ile miguu ndo jaribu lenyewe kwa yule bwana mwenyekiti wa casfeta.
Hapa niseme kidogo yule bwana mwenyekiti alikua na kawaida ya kwenda maombi ya usiku ila kabla hajatoka huwa mara nyingi huenda kuoga chooni ule usiku kabla hajaenda maombi.
Sasa huyu muhuni aliyeleta hii miguu miwili ya mbuzi akasema hii miguu tutaweka kwa kuegemeza mlangoni kama inaangalia mbele yaani kuingia chooni, choo ambacho mwenyekiti ataingia halafu tutagonga mlango na kuondoka.
Hapa pia nieleze kidogo vile vyoo vyetu mtu akiwa ndani awe amesimama au amechuchumaa akiwa anajisaidia huwa anaona miguu ya aliyesimama kwa nje kama amesimama kwenye mlango wa choo.
Basi bwana wahuni wakasubiria mda ambao mwenyekiti ataamka kwenda kuoga hili aende kwenye maombi, na hapa ni yeye tu(mwenyekiti) alikua hajui ila bweni zima tulikua tunajua huu mpango.
Mda ukafika ilikua kama saa 8 usiku hivi kumetulia, dogo wa form nyoya akaja kutushtua kwamba mwenyekiti ameenda chooni, basi yule muhuni akasubiri dakika kadhaa akaenda na miguu mbuzi hadi chooni akaweka mlangoni kama alivyosema halafu akagonga mlango halafu akasepa.
Sasa wakati huo kumbe mwenyekiti alikua anakata gogo(anakunya), hivyo alikua anaona vizuri kwa chini ya mlango, kusikia mlango wa choo unagongwa akaangalia chini ya mlango, kuangalia chini akaona kwato na miguu ya mnyama.
Yule bwana alitoka na mlango kama ulivyo tukasikia tu puuuuuuh aliamsha bweni zima, damu zinamvuja kwa kujikata na mlango ni ile milango ya bati yenye frame ya chuma. Akasema ameona jini😅😅
Yule bwana aliyeweka miguu baada ya mwenyekiti kuingia bweni huku akitweta na damu zinatoka akenda chooni kimya kimya kutoa ile miguu kuficha msala kwa sababu mwenyekiti aliumia sana ilibidi tumepeleke zahanati ya shule.
Baada ya kupata nafuu watu wakawa wanamhoji sasa kwanini hukukemea na akaanza kukimbia? Jamaa hakuwahi kutupa majibu na hadi anamaliza form six alijua amekutana na jini😅
NB: Hakuwahi kulala tena bweni zaidi ya ofisi ya dini, shule yetu ilikua na ofisi za viongozi wa dini na sehemu za kuabudu pia.