Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Pimbi huyo, eti anataka aoneshwe Uthibitisho Kwa kuandika humu ndani.

Sayansi yake yenyewe inahitaji mchakato wa kimaabara kujithibitisha, yeye anataka kuona nini sijui.

Ni limbukeni fulani hivi wa kuokotaokota stori za vijiweni.
Mpumbavu tu huyo yaan anakera kinoma
 
Anakera sana huyu jamaa pamoja na wenzake,amejikita hapa kwa watu wenye imani potofu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]badala aende kwenye majukwaa ya sayansi huko wakajadiliane namna ya kufika mars,yeye kakaza fuvu mara uchawi haupo z z z z kwani kuna mtu kamlazimisha aamini uchawi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu hii kitu kwako haifit entoptic phenomena ILA hii ni hallucinations.
Mfano kusikia sauti ya mtu analia au anaongea lakini hakuna mtu huyo.
Au kuona mtu au vitu ambavyo hakuna mtu mwingine anayeviona kama vile kuona mtu amesimama karibu nawe lakini kiuhalisia hakuna huyo mtum

Hallucinations huwa inasababishwa na vtu vingi mojawapo ni magonjwa ya akili
Ila entoptic phenomena huwa inasababishwa na muundo wa ndani wa jicho lako.
Kitendo cha kuona kitu kinaamliwa na wanaokutazama au wewe unayetazama kitu husika?
 
Jamani kama huamini uchawi upo embu tulia basi usiharibu uzi.Kutwa kushupalia kila story ya kila mtu alf mtu mwenyew unakuta kazaliwa mjini na kakulia mjini ila unavyokomaza shingo utadhani unajua kila kitu.Huamini tulia hulazimishwi acha watu waandike story zao mnaharibu uzi!
Hao ndio wachawi wenyewe wanapoteza lengo la uzi ili tusiwatambue
 
Tarehe 10/07/2023 asubuhi ya saa moja na dakika kadaa watoto wangu wawili darasa la sita na mwingine la kwanza, walianza kupiga kelele kama kushangaa. Kitendo kilichokera mama yao na mimi pia. Kutoka wananionesha bundi aliye kuwa akidodoka kutokea juu ya bati/ paa ya nyumba yangu. Alipo fika chini alionekana amekufa miguu juu yaani alikufa akiwa chali. Hivyo nikaishia kushangaa tu. Nikawaelekeza watoto wasimwambie mtu yeyote tendo lile. Mwezi mmoja nyuma njiwa poli alikutwa amekufa upenyuni mwa nyumba yangu kubwa amabayo imebakia marumaru na baadhi ya vitu ikamilike. Nilichunguza nikagundua njiwa alijigonga kwenye alminium/ kioo cha dirisha akafa. Sikujali ila niliwaelekeza pia watoto wasiongelee lile tukio.

Sasa huyu bundi baada ya kuonekana amekufa nikarudi ndani kuoga na kujiandaa ili tuelekee kazini na watoto waelekee shule. Sasa mke wangu ana mtoto mwingine wa tatu mwaka mmoja na miezi miwili. Tumemuajiri binti wa jirani anakuja kumchukua na kushinda naye halafu mke wangu anamchukua anapotoka kazini mida ya saa tisa au kumi jioni.
Hivyo alikuja kumchukua mtoto kama ilivyo ada. Kwa kuwa niliwataka watu wasijue mke wangu alipo sikia kengele ina gonga akaniambia yule binti atakuwa ameijia mtoto kwa hiyo nikamtoe yule bundi ili asione ikajulikana kwa kuwa nimeamua iwe siri yetu.

Kweli nilitoka nikamtupe nje ya fensi. Cha kushangaza nilipo msogelea akainuka kama anataka kuruka. Nikachukua fimbo ya ufagio wa ndani nikampiga nayo kwa nguvu mara moja tu akaonekana amekufa. Nikashika bawa lake moja na kumrusha nje ya fensi. Nikaondoka kazini kama kawa.

Kilichofuata mida ya saa nne asubuhi kulitokea kutoelewana na mke wangu kwa kiasi kikubwa na kila nikielezea sababu ya ugonvi huo ndugu wananishangaa kuonesha eti mimi ndiyo mwenye makosa. Ila kiukweli toka hiyo siku sijisikii kumkubali wife hii hali napambana nayo kwa kiasi kikubwa na ninaona speed yangu ya kufanikisha malengo yangu inapungua sana na ninakosa ule umotomoto wa hamasa ya maendeleo kutokana na chuki kwa wife. Hata leo nimeamka na hali ya kutompenda wife, bila sababu ya msingi kwa kukelwa na kosa alilotenda siku hiyo nashindwa kusamehe, japo alikosea sharti langu la kumtaka asiwe anapakizwa na watumishi wenzie wa kiume sipendi na ndicho alifanya. Japo alieleza sababu ya kutenda vile nimekuwa mzito kusamehe.

Sasa wanajamii forum niwaulize sababu ni huyu bundi au ni nini? Hali yangu kwa sasa nimbaya kutokana na sonona takribani mwezi huu wote siko sawa kabisa. Najisikia kukata tamaa.
Bundi ni ndege wakawaida tu na ni ndege mzuri sana kama hutamuangalia kwa jicho la kishirikina.

Huu uzi mpaka unafika 1K replies ineonesha ni jinsi gani watu wamezama kwenye imani za ushirikiana.

Lakini nataka nikuambie kama utaendelea kutafuta suluhu ya mgogoro wa kimahusiano kati yako na mkeo kwa mawazo ya ushirikina basi utaenda kufeli.

Hakuna uchawi, hakuna, majini, hakuna mizimu wala hakuna kurogana.

Nakuambia ukiendekeza fikra hizo utajikuta unajitengenezea maadui wengi ukiwadhania ni wachawi wanaokutakia mabaya wakati sio.

Huu uzi mi nautumia kama entertainment tu ila nime quote post yako baada ya kuona umeweka ombi la kutaka ushauri.

Ushauri wangu kwako ndio huo whether you like it or not lakini hakuna chemistry yeyote kati ya bundi na mafarakano yenu na mkeo.

Bundi ni ndege tu
 
Jamani kama huamini uchawi upo embu tulia basi usiharibu uzi.Kutwa kushupalia kila story ya kila mtu alf mtu mwenyew unakuta kazaliwa mjini na kakulia mjini ila unavyokomaza shingo utadhani unajua kila kitu.Huamini tulia hulazimishwi acha watu waandike story zao mnaharibu uzi!
Acheni kupotosha watu washindwe kuangalia namna sahihi ya kudili na changamoto zao wajikite kutafuta ufumbuzi kwenye maswala ya kufikirika.

Ongelea uchawi kama stori kufurahisha watu ila sio opt ya kumshauri mtu kwenye utatuzi wa shida zake.
 
Acheni kupotosha watu washindwe kuangalia namna sahihi ya kudili na changamoto zao wajikite kutafuta ufumbuzi kwenye maswala ya kufikirika.

Ongelea uchawi kama stori kufurahisha watu ila sio opt ya kumshauri mtu kwenye utatuzi wa shida zake.
Ila hayo mambo ya kufikirika kama kweli yanatoa ufumbuzi wa matatizo yao basi bora uache watu watatue shida zao kwa hayo mambo.
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Nitafute kwa wakati wako ili nipate kumtibia apate kupona huyo dogo uchawi upo .
 
Hapana mkuu sijatazama hapo tu.

Ungemalizia na huko chini kabisa, unaweza kuwa ecstatic na BADO hali hii ya hallucinations ikakupata.

Mimi binafsi huwa sina shida na imani za watu ILA kwenye swala la kuthibisha ndo huwa kuna matatizo. Naheshimu imani YAKO.
Kama huna shida na imani za watu kwa nini unataka wakuthibitishie?
 
Kama huna shida na imani za watu kwa nini unataka wakuthibitishie?
Huwa wanadhani kwa wengine kushindwa kuthibitisha imani zao ndio moja kwa moja kunawafanya wao kuwa sahihi kwa wanayoyaamini wao. Kama utafuatilia vizuri utaona wanakimbilia kudai uthibitisho na wanatumia muda mwingi kudai huo uthibitisho(hata kama hicho kitu hawakifahamu vizuri) kuliko hata kueleza zaidi hayo wanayoyajua wao.

Kung'ang'ania kudai uthibitisho ni kama kinga na silaha kwao katika kushambulia imani za wengine.
 
Ujuaji mwingi katika huu Uzi kama kitu huamini wewe why ulazimishe wengine wakuamini wewe Bora mkaa kimya
🤣Hivi wewe...what's wrong with educating ppo..hizi Imani hazina faida kwa mtu yoyote zaidi yakuendeleza ujinga na umaskini. Sawa amini unachoamini...amini bac Mungu yupo mawinguni, ila ukianza kuamini kwamba Kuna watu wanafanikiwa kwa uchawi, wewe unafeli kwa uchawi, unakuwa hausolve tatizo lako..Bali kutafuta visingizio tu
 
Pimbi huyo, eti anataka aoneshwe Uthibitisho Kwa kuandika humu ndani.

Sayansi yake yenyewe inahitaji mchakato wa kimaabara kujithibitisha, yeye anataka kuona nini sijui.

Ni limbukeni fulani hivi wa kuokotaokota stori za vijiweni.
🤣Unahitaji maabara ulione jua...🤣Kuna many forms of research bana experimentation is just one of them.. Rudi form 4 geography
 
Huwa wanadhani kwa wengine kushindwa kuthibitisha imani zao ndio moja kwa moja kunawafanya wao kuwa sahihi kwa wanayoyaamini wao. Kama utafuatilia vizuri utaona wanakimbilia kudai uthibitisho na wanatumia muda mwingi kudai huo uthibitisho(hata kama hicho kitu hawakifahamu vizuri) kuliko hata kueleza zaidi hayo wanayoyajua wao.

Kung'ang'ania kudai uthibitisho ni kama kinga na silaha kwao katika kushambulia imani za wengine.
🤣🤣🤣🤣Ndio...kwa Nini utudanganye Sasa...yaani we uje uje tu na story zako mbele ya watu wazima wenzako afu si tukuamini tu kisa we unaamini. Dunia haipo hivyo, Kama huna uthibitisho huna maana, hata sheria inafanya kazi hivyo. Sayansi same thing. Bac Kama huna uthibitisho tofautisha situations ambazo uchawi unahusika na hauhusiki..🤣bado huwezi..Sasa unakuta situation moja mwingine asie na elimu anasema ni uchawi mwingine anaona ni natural coincidence au hallucinations. So ili tuweke kitu clear lazma wote tuone...🤣🤣tuna attack Imani kwa sababu Imani itself it's an excuse. Mtu anaweza abudu jua mbwa it's just imani, wote wakiomba wanapewa..the question comes ni kweli jua linajibu maombi au ni we mwenyewe..same applied to uchawi na Imani nyingine
 
Back
Top Bottom