Kitu gani unachokumbuka ambacho mama yako alikuonya ukiwa mtoto na mpaka leo hukisahau?

Mama aliniambia Mwanamke ni Nyoka mwenye sumu Mwanangu!....Baba akanambia ikitokea ukampa mimba Mwanamke, huyo ndo Mke wako, isipokua kama huyo Mwanamke amelelewa Na Mama tu bila Baba, na Kama Baba na Mama yake waliachana, USIOE MWANAMKE HUYO!......UTAKUJA KULIA PEKE YAKO!
 
Mi alinipiga baada ya kunikuta nashikia nguo wakati napika alifoka sana akisema wenzenu wanazihitaji na hawajui watazipata wapi..nilihisi kanionea lakini nilipoanza chuo Dodoma ndo nikajionea.Wallah MUNGU awaongoze mama zetu waliohai na walitangulia.
 

Usidhulumu/usirushe pesa/mali ya mtu.
Mke wa mtu muogope kama jela
Wakatae marafiki/company mbaya
Penda wengi lakini AMINI wachache
 
mama aliniambia mengi ila ambalo sitalisahau na nalishuhudia kila kukicha ni hili.. "mwanaume siyo ndugu yako ni rafiki tu aweza kuwepo ama kuondoka usiache kumthamini ndugu kwa sababu ya rafiki"
live long mama.
Safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…