Kitu gani unachokumbuka ambacho mama yako alikuonya ukiwa mtoto na mpaka leo hukisahau?

Kitu gani unachokumbuka ambacho mama yako alikuonya ukiwa mtoto na mpaka leo hukisahau?

Mama aliniambia Mwanamke ni Nyoka mwenye sumu Mwanangu!....Baba akanambia ikitokea ukampa mimba Mwanamke, huyo ndo Mke wako, isipokua kama huyo Mwanamke amelelewa Na Mama tu bila Baba, na Kama Baba na Mama yake waliachana, USIOE MWANAMKE HUYO!......UTAKUJA KULIA PEKE YAKO!
 
Mi alinipiga baada ya kunikuta nashikia nguo wakati napika alifoka sana akisema wenzenu wanazihitaji na hawajui watazipata wapi..nilihisi kanionea lakini nilipoanza chuo Dodoma ndo nikajionea.Wallah MUNGU awaongoze mama zetu waliohai na walitangulia.
 
Poleni na kazi za wiki nzima Wakuu!

Ni weekend ya kurelaxxx

Nimeona leo tujikumbushe enzi zileeeee

Nikiwa mdogo nilikuwa sipendi kula chakula kingi ila nilikuwa napenda mboga kama nyama au samaki, wasiponiangalia wakati wa kupakua wanaumia! Nilikuwa najijazia mboga kiukwelii...nilikuwa na umri kama wa miaka 6-8 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mama akanidhibiti kwa kunieleza kuwa, kila wakati ninapopakua mboga niwe nawakumbuka wenzangu ambao hawajapakua.

Tokea kipindi hicho mpaka leo huwa kila nikitaka kupakua lazima nikumbuke ambao bado hawajapakua. Hivyo mama alinifundisha nidhamu wakati wa kula tokea enzi zile mpaka leo nakumbuka.

Vipi wewe unakumbuka lipi ambalo mama alikurudisha kwenye reli?

Usidhulumu/usirushe pesa/mali ya mtu.
Mke wa mtu muogope kama jela
Wakatae marafiki/company mbaya
Penda wengi lakini AMINI wachache
 
mama aliniambia mengi ila ambalo sitalisahau na nalishuhudia kila kukicha ni hili.. "mwanaume siyo ndugu yako ni rafiki tu aweza kuwepo ama kuondoka usiache kumthamini ndugu kwa sababu ya rafiki"
live long mama.
Safi
 
Back
Top Bottom