NILISHAKUJIBU HAPA ;
Mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa ni pamoja na eneo la mji wa arusha, mji wa arusha ulikuja kutengwa na kugawanywa na baba wa taifa mwl Julius nyerere akaunda mkoa mpya wa arusha pamoja na wilaya za monduli na manyara ya sasa.
Kiasili wameru ni wachagga, na ilikuwa sehemu ya mkoa wa Kilimanjaro, wameru na wachagga wa machame wanasikilizana, nenda kajifunze historian kuhusu kumegwa kwa mji wa arusha.
Kuhusu uhaba wa ardhi, wachagga walivamia Kilimanjaro na kuteka eneo LENYE RUTUBA KUZUNGUKA MLIMA KILIMANJARO. hawakuwa na haja na maeneo mengine makame kama ya upareni, wao walitaka maeneo yenye RUTUBA TU kwaajili ya kilimo na ufugaji, na eneo hili lenye rutuba ni kuzunguka mlima Kilimanjaro tu, waliishi hapo kwakufanya shughuli za kilimo na ufugaji.
Kwa wakati ule idadi yao na mashamba yao yaliwatosha sana, mpaka serikali ilipokuja na kuanzishahifadhi ya wanyama ya mlima kilimanjaro (Kilimanjaro national park) KINAPA ambayo ilizuia wachagga kuendelea kufyeka msitu unaozunguka mlima Kilimanjaro ili kujipatia mashamba na adhi yenye rutuba.
For Your Information;
Kinachotakiwa na wachagga sio ardhi tu, bali ni ardhi yenye rutuba! Kilimanjaro kuna ardhi tele ya kuishi lakini wanachotaka wao ni ardhi yenye rutuba! Na kuomba ardhi sio dhambi.kumbuka pia wako wachagga wengi tu wenye mashamba makubwa morogoro, mbeya, iringa,tanga na pwani, sasa sio wrote wenye access ya kujua wapi ilipo ardhi bora ndio maana wakatoa maombi yao na sio kosa kisheria.