NGOJA NIKUSAIDIE KIDOGO KWASABABU KUNA MAMBO HUJAYAJUA NA KWA FAIDA YA WENGINE:-
• Kifupi ukiona Mtu yeyote anajiita Muarusha hata kama anazungumza kimasai still hana asili yoyote ya Umasai ila ubantu ambao ni wa kichagga au kimeru, kwasababu, kiasili na tangu enzi Wamasai hawafanyi vifuatavyo :-
* HAWALIMI, wakati Waarusha / Wameru tangu karne nyingi zilizopita wanalima migomba, mahindi, maharage,mbogamboga na nafaka zilezile kwa 100% zinazolimwa Kilimanjaro
*ASILI YA CHAKULA, Unaposikia LOSHORO au kitalolo ni vyakula vinavyotokana na mahindi, maziwa na ndizi. Kitalolo kina hadi mbogamboga, Vyakula hivyo havijawahi kuwepo Umasaini kwasababu Wamasai hawalimi mahindi wana ndizi, ila Wamasai chakula chao ni Nyama na Maziwa TU.
* AINA YA UFUGAJI : Wameru, Waarusha, Wachaga wana ufugaji wa ndani (Sedentary Livestock keeping) na wanafuga mpaka Kuku, wakati Wamasai kamwe hawafungii mifugo ndani isipokuwa wanatafuta malisho popote katika mkoa wowote hawana makazi ya kudumu.
* AINA YA MAKAZI : Kwa karne nyingi zilizopita Wameru/Waarusha/Wachaga wana makazi ya kudumu (Permanent settlement) ila Wamasai hawana makazi ya kudumu, hawana makaburi ya kudumu wala maboma yanayokaa mahala pamoja permanently.
WAKIBOSHO KUINGIA ARUSHA MIAKA YA 1800 :
ARUSHA ni neno linalotokana na ''LARUSA'' ambalo ni Ukoo uliopo Kibosho na uliohamia Arusha kabla hata Wamasai hawajafika Arusha ya leo.
Hawa wakibosho walifanya shughuli ya kuuza nyama mabuchani TU. Hakuna Mmasai aliyekuwa anauza nyama buchani isipokuwa wao wamasai walikuwa wanawauzia ng'ombe wakibosho na wakibosho wakiuza buchani kuwauzia wasomali walioishi kaloleni na waswahili wachache pamoja na wahindi waliokuwepo wakati ule Arusha mjini.
KIFUPI, Ukisikia Mtu anajiita Muarusha hata kama anakuambia ni Mollel, Laizer, Kivuyo, Siara au Sirikwa halafu amezaliwa Arusha mjini na Babu, baba yake kazaliwa Arusha mjini huyo ni Mkibosho ama Mmachame TU.
Baadhi ya Maboma ya kiarusha yenye asili ya kibosho ni kama Kirindo au Kirindoi ipo sanawari, Kishili ipo Sekei, Boma la Siara wapo Kijenge, Lesiando ipo Ilboru, Ndoivo - Ilboru, Kirusha ipo Ngaramtoni n.k, n.k ILA watakuambia wao ni Mollel au Laizer au Kivuyo.
NI KWELI, kuwa Wamasai waliwakuta Wakibosho wa ukoo wa ''LARUSA'' pale Arusha mjini hasa pale ATC na Levolosi, na wao wakawaita LARUSAI na mpaka leo hii na kesho Wamasai wa Simanjiro, Longido, Loliondo n.k wanawaita Waarusha ''LARUSAI''
WAMERU ni Wamachame kabisa wale lakini utasikia Mbise, Kitomari, Kaaya n.k lakini kiasili ni Wamachame na wana share like everything, wao walitengana kipindi cha uanzishwaji wa Dayosisi za Lutheran (hii ni historia nyingine tuiache)
Mengine uliyoyaandika ni Kweli.
Nakaribisha Maswali.
Loyalist