Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Kufumwa tunatiana wakati wa komborera.
 
ha haaha nimejikuta nacheka walivyodondoka
 
ha haaha utoto raha sana .. iala mama zetu walikuwa wanapiga sana aisee
 
Nilichukua miba ya mtende huwa ni mikubwa hivi nikaichimbia nikiacha ncha kali kwa juu katika kinjia wanapita watu halafu nikajificha,akapita kaka mmoja akakanyaga nikacheka akaniona nilikimbizwa mpaka leo sikurudia japo hakunipata.
ha ha ha ha ha ha ha ha wewe umenifanya nicheke mpaka watu wananishangaa hapa!!!!
 
OMG !! Nilisababisha Ajali ya zaidi ya gari 15 katika ROUND ABOUT nilipo katiza kwa miguu !!
 
Nskumbuka ndugu yangu miaka ya hivi karibuni alivizia mama yake na baba yake awapo akatupia kitu hicho,da umeme zii,jamaa kachanganyikiwa,sasa anajua kwamba mama yake jion humuagizia kwenye mambo ya vikoba,sasa jamaa kafikilia hapa wazee wakirud wakiniagiza harafu umeme ukarud itakuwaje,jamaa katulia tutweeeeeee,walivyorud jamaaa akaongopea km anaharisha kweli wazaz wake walivyorudi wakawa na lengo lilelile la kumuagiza,sasa baada ya kuona kwamba jamaa anaendesha basi wakasema atampelekea asubuhi,jmaaa huku akipiga misele ya ndani chooni,ndani chooon,sasa wakati ile nakwenda chooni anafungua mlango "anasikia uwoooooooooo",jamaaa badala ya kuingia choooni mbio ndan mpka wakamshangaaa,alivyofanikiwa akasema mwanzo na mwisho
 
Nilikuwa na tabia moja, kuwe na joto kuwe na baridi; me Ntalala bila kuvaa nguo kabisa na blanket langu juu.

Siku ya siku nimelala wee, kuja kushtuka saa 1 asubuhi, nimepanic hatari nimeshachelewa shule. Nilichofanya ni kukurupuka piga uniform ndrukiii shule (bahati nzuri home na shule hakukuwa mbali)

Kufika shule nikakuta ndo wanamalizia usafi, na uzuri friends zangu waliniwahia namba. Kuja kutahamaki sikumbuki kama nilinawa uso, ila mswaki sikupiga na tei te (chupi) pia sikuvaa. Nikaona isiwe kesi nikaenda bombani nikanawa, ile kurudi nikawa najishtukia ukute domo linanuka. Nikaanza kupretend kuwa jino linauma so tukawa tunawasiliana kwa vimemo, navyopenda kustorisha sasa khaa niliumiaje. Kufika muda wa break ndo nikatamani nilie kabisa, rede imekolea nashindwa kucheza nisije nikapiga chejo nikamwaga radhi. Sijawahi kuwa na siku mbaya shuleni kama ile. Kuanzia siku ile nikawa nikilala, tei tei naiweka juu ya bag nisije nikasahau kuvaa asubuhi[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Tei tei ndio nini??!!!
 
Nakumbuka nilikuwa na rafiki yangu, siku moja akawa ana hela, kumuuliza alkozipata akaniambia alipewa na anti yake, kumbe aliiba! Basi tukatumia kila tulichokipata kinachofaa kula ananunua, sasa chenji zilizobaki akaniambia nimuifadhie then tuwe tunatumia wote, kumbe alikuwa anaogopa kwenda nazo kwake, mimi nikaenda kuzichimbia chini karibu na home lakin kuna mtu aliniona nkichimbia yeye akavunga nlipoondoka akaenda kufukua akasepa nazo,yamkini hadi leo sijamgundua! Kesho yake asubuh ndo nlkuja kukuta zimefukuliiwa, nlipoenda shule yule jamaa akaniambiia nimpe hela, nikamwambia nimesahau, tulipotoka shule nkamwambia hela zimepotea baada ya kuzichimbia, daah ghafla nkalamba box, na mimi nkarudisha konde, tukapigana mpka watu wakatuamua ikabidi tupelekwe kwa wazazi wetu ndipo ikabainika aliiba, tukalambwa wote bakora za kutosha...nlikuwa std two wakati huo...
 
Mimi nakumbuka nikiwa DOGO mbu walikuwa wanasumbua sana sasa kuna siku nikasema ngoja niwakomeshe nikachukua kiberiti na kuanza kuchoma neti ili niwateketeze...Nilichezea kipigo cha haja kutoka kwa dingi !!!!!
 
Wakati unaiba ulikuwa unafikiria nn?
 
Kijana kumbe we ni bro wangu kwenye hizo vitu..Nakumbuka mi first time kuangalia nilikuwa form one..Basi baada ya kutoka kuangalia kila msichana ninayekutana naye namuona kama yupo uchi vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…