Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Mimi nilikua muoga wa sindano za "Kristapen"sijui zinaandikwa hivo, nikaenda na maza kuchomwa hosp. Ile nimeanza kuchomwa imeingia tu hivi nikaona maumivu ni balaa nikafanikiwa kukimbia nje ya chumba huku nalia balaa na sindano imening'inia kwenye Tako, daah nesi na maza wakanikimbiza na kunikamata hapo nje afu watu ni wengi hapo nje kwenye benchi la foleni wakamalizia kunichoma sindano hapo hapo kwenye benchi mbele za watu, daah nilisikia aibu balaa
 
Wakati unaiba ulikuwa unafikiria nn?
Utundu wa kitoto tu nilitaka kujua kwanini ile hirizi inapumua na nikagundua kuwa mle ndani anaweka vinyonga, sijui walikuwa wanakaa muda gani mpaka kufa
Nilichoshindwa kujua mpaka leo ni je alijuaje kama mimi ndio nilichukua hirizi yake
 
Nikiwa darasa la tatu nilikuwa na kijipu vile vidogo kwenye makalio. Sasa niliogopa kusema maana watu waliokuwa wananizunguka walikiwa wababe nilihisi watanikamua bila huruma, nikauchuna.

Asubuhi naenda shule sijapewa hela nikaamua kuiba, hela za mboga zilikuwa zinakaa juu ya vile vikabati vya zamani vyembamba virefu. Nikapanda stuli nikafikisha mkono kwenye hela bahati mbaya ikasogea mbele kidogo ikabidi nijirefushe zaidi kumbe nimeshaharibu stepu pale kwenye stuli ikateguka!!! Niliporomoka nikatulia tako lile lile lenye jipu, nilipata uchungu flani amaizing kabisa hadi wakubwa wakanikuta hapo na siri zote zikafichuka
Hahaaaa we bana umenichekesha sana, khaaa!
 
Nakumbuka nilikua na mchezo wa kudandia magali kwa nyuna bila dereva kujua..bas siku moja nilidandia trector nikashindwa kushuka trector lilikua linafata mawe polini mbali kidogo...nlivoona naji yamenizidi ilibidi nijisalimishe tu kwa dereva...dereva akanambie twende wore mpaka anakochukua mawe tutarudi wot,kufika kule alinigonga bakora za kutosha.
Mda wa kurudi trector likaalibika ijabidi tulale ukouko..uku home nako natafutwa sana Aaah keshi yake nilivorudi nlikura njiti za kutosha..
Mkuu 0713 ilibaki salama kweli?
 
Nilikuwa na tabia moja, kuwe na joto kuwe na baridi; me Ntalala bila kuvaa nguo kabisa na blanket langu juu.

Siku ya siku nimelala wee, kuja kushtuka saa 1 asubuhi, nimepanic hatari nimeshachelewa shule. Nilichofanya ni kukurupuka piga uniform ndrukiii shule (bahati nzuri home na shule hakukuwa mbali)

Kufika shule nikakuta ndo wanamalizia usafi, na uzuri friends zangu waliniwahia namba. Kuja kutahamaki sikumbuki kama nilinawa uso, ila mswaki sikupiga na tei te (chupi) pia sikuvaa. Nikaona isiwe kesi nikaenda bombani nikanawa, ile kurudi nikawa najishtukia ukute domo linanuka. Nikaanza kupretend kuwa jino linauma so tukawa tunawasiliana kwa vimemo, navyopenda kustorisha sasa khaa niliumiaje. Kufika muda wa break ndo nikatamani nilie kabisa, rede imekolea nashindwa kucheza nisije nikapiga chejo nikamwaga radhi. Sijawahi kuwa na siku mbaya shuleni kama ile. Kuanzia siku ile nikawa nikilala, tei tei naiweka juu ya bag nisije nikasahau kuvaa asubuhi[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hahaaaa kumbe we hupati shida na ule msema wa ukikubali kuolewa kubali na kulala bila pichu, teh
 
Mitaa ya kona ya Nairobi Arusha kulikuwa na wamama wauza Karanga na maandazi barabarani. Basi nikiwa na Binamu yangu tulikuwa na tabia ya kujifanya tunataka kununua karanga. Basi inabidi muuzaji atupe za kuonja. Tukishaonja tuu tunatoka nduki! Hiyo 1 ya nyingine baadae
 
Mimi nilikulia Ushuani geti kali kutoka na gari kurudi na gari na home after homework tunakaa na familia kwa utulivu hatukuwa kama nyie home kwenu nothing lazima muwe wajinga na vituko.mfano hapo juu kuna mchangiaji alikuwa haendi shule kazi kujificha.


swissme
Kweli hiki kilikua kituko chako cha utotoni.
 
kuna sku kulikuwa na harusi kwa mother mmoja hv sa sisi watoto tukapewa kazi ya kupanga viti ukumbini huku tukiaidiwa pilau,tulipomaliza tukaenda zetu kucheza ilipofika mida ya jioni tukajisogeza ili tupate ahadi yetu lkn hatukupata tuliendelea kusubiri mpk ikafka mida ya saa 1 kuelekea saa 2 usiku.
sasa ktk hilo kundi tuliokuwepo kulikuwa na dogo mmoja tulikuwa tunamzidi umri kidogo kwa wenge la kunyimwa pilau tukaanza kumlazimisha asepe skani lkn dogo akawa mbishi akala kipigo/mitama akaanza kulia huku akiwa chini kwa muda wa kama dk5 hv akuna aliemjali si tukaendelea na stor zetu...
ebhanaeee si kikanuka dogo akapandisha mlio kwa sauti ya kuunguruma akaamka kabeba stone 2 kubwa wacha weee tulianza kukontoza dogo nae nyuma yetu wachache wakauma kona wengine tukaendeleza sasa tulipokuwa tunaelekea ilikuwa ni skani kwetu lkn nlpofka me mwenyewe niliunga na wenzangu coz nliona mpk nkafungue mlango jiwe litakuwa limeshanipata hata la kichwa tukaenda kujificha dogo akala kona...
hili tukio sitalisahau...
 
Mi nakumbuka kuna demu alimzingua jamaa mmoja kitaa..Basi yule jamaa kwa asira akamwambia "ujue ntakubikiri"..Basi mi nikalipenda hilo neno bila hata kujua maana yake..Nikihisi kuwa litakuwa linamaanisha ntakupiga....Siku tumekaa sitting room na wazee pamoja na wagen tunacheki Tv tukaanza kugombania rimoti na sista..yeye akiwa anataka kubadili chanel..Ndo kumwambia "ujue ntakubikiri,we endelea tu"...

Nilipelekwa chemba nikapewa stiki za kutoha..Zen baadae darsa ndo likafwata..Ndo ikawa chanzo cha kupunguza kuokotaokota maneno kitaa
Hahaaaaa no wonder unauza vifuniko vya asali aisee, hizi mambo kumbe unazo tangu utotoni, duuuh kubikiri sistaako!!
 
Nikiwa form two siku moja sijui nini kiliniwasha ila nilijikuta nimewaropokea madem fulani wawili darasani kuwa break munione niwapeleke breakfast kantini ya shule wakaniambia poa. Mi baada ya dakika mbili nikasahau hiyo habari.

Break ya saa nne ilipofika mi nikatoka na mshkaji wangu tunatembea taratibu nikashangaa navutwa shati kwa nyuma!! kugeuka lahaula ni wale madem na hapo sina hata kumi mfukoni mi niliropoka tu.. nahisi nilitoa haja ndogo sikuile maana nilikosa hata cha kusema na hao ndo madem wakali wa class kwetu. Nilimgeukia mshkaji nikamuangalia kwa macho ya 'leo natamani nigeuke barafu niyeyuke'

Mshaji akatoa noti ya Sh.200/- mpyaa sijui aliiba wapi naye maana naye hana kawaida ya kuwa na mkwanja. Akanipitishia kisirisiri nikawapa wale madem wakasepa.

Jamaa alinipa kichambo cha haja ila niliona kawaida sana hata angekesha ananisema. Ni mshkaji wangu tunasaidiana kwenye shida na raha hadi leo na disemba mwaka jana nimechangia hela ya ng'ombe mzima wakati anatoa mahari
 
Nikiwa form two siku moja sijui nini kiliniwasha ila nilijikuta nimewaropokea madem fulani wawili darasani kuwa break munione niwapeleke breakfast kantini ya shule wakaniambia poa. Mi baada ya dakika mbili nikasahau hiyo habari.

Break ya saa nne ilipofika mi nikatoka na mshkaji wangu tunatembea taratibu nikashangaa navutwa shati kwa nyuma!! kugeuka lahaula ni wale madem na hapo sina hata kumi mfukoni mi niliropoka tu.. nahisi nilitoa haja ndogo sikuile maana nilikosa hata cha kusema na hao ndo madem wakali wa class kwetu. Nilimgeukia mshkaji nikamuangalia kwa macho ya 'leo natamani nigeuke barafu niyeyuke'

Mshaji akatoa noti ya Sh.200/- mpyaa sijui aliiba wapi naye maana naye hana kawaida ya kuwa na mkwanja. Akanipitishia kisirisiri nikawapa wale madem wakasepa.

Jamaa alinipa kichambo cha haja ila niliona kawaida sana hata angekesha ananisema. Ni mshkaji wangu tunasaidiana kwenye shida na raha hadi leo na disemba mwaka jana nimechangia hela ya ng'ombe mzima wakati anatoa mahari
 
nakumbuka nlivyokuwa naenda kutembea alafu baadaye giza narudi na majani ya ng'ombe siku moja hiyo nlitumwa kitu dukani badala nirudi nkaingia kwenye kibanda cha kuonyesha video kwanzia saa 1 usiku nilirudi saa 4 usiku na pesa nliyo tumwa nayo nilitumia kulipa movie na kunywea chai nilivyorudi nilipigwa fimbo za kufa pipo. Na kuanzia wakati huo sikurudia tena hadi juzi juzi ukubwani
 
Nikiwa mdogo niliwahi kuiba hirizi iliyokuwa inapumua ya mzee mmoja mchawi aliyekuwa anaogopeka sana pale kijijini. .kwenda kuipasua nilikuta kinyonga aliyekatwa mkia alitweta kwa kukosa pumzi vizuri
Lile tukio lilikuwa kubwa na baya pale kijijini mpaka ikibidi nihamishwe
Basi toka siku ile ukawa uko very interested na kupiga watu fix mtaani ili na wewe uogopwe.
 
Back
Top Bottom