Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Kufumwa tunatiana wakati wa komborera.
 
Dahh.....
Hii ilinitokea ukubwani aiseeee....
Tukiwa chuo flani Jijini Dar, tulikua tukilala kwa room yetu na usiku tuliamka kujisomea.
Pembeni ya room yetu alikua jamaa na mpenziwake wapo kwa room moja na room mate wengine.
Kumbe jamaa walikua wakianza kufanya mambo yao, hawa too mate wangu walikua wakienda wanapanga viti then wanaanza kula chabo kwa kubadilishana (kwazam).
Sikuhiyo katika kula chabo, jamaa mmoja alianguka kutoka juu viti walivyo vipanga na ule mshtuko ulifanya kelele ambayo ilipelekea jamaa wote kukimbia na kujificha sehem tofauti na room kwetu.
Jamaa mwenye mpenzi alitoka kwa hasira na kuja moja kwa moja room kwetu na alinikuta pekeangu nikiwa najisomea Dahh......[emoji134], jamaa alini maindi sana na aliamini kwamba mimi ndie nilikua nikimla chabo na nika dondoka na kiti.
Kuanzia skuhiyo jamaa alinichukia sanaaaa..... hapo ilikua mwaka 1999.
Cha ajabu nilikuja kuitwa kwenye usahili wa kazi sehemu mwaka 2008, nilimkuta na yeye akiwa kati ya walio ni sahili. Jamaa alini recommend vizuri na nilipata kazi na Hakuwahi kuniuliza tukio lile
ha haaha nimejikuta nacheka walivyodondoka
 
mbavu sina mumie!!!!!!!!!!!
mie sitasahau nilikuwa mgonjwa nikapelekwa hosp na mama. enzi hizo sindano ni zile za ppf tena zinachemshwa kwenye stove ndo unadungwa, manake zilikuwa za kushea.
sasa nikiwa na maza nilicho fresh japo iliuma balaa afu si unajua vituo vya afya vya msing vilivyokuwa? manake havikuwaga na vitanda vya kuchomea sindano kama siku hizi so unasimama kisha unatupiwa mkuki wako.

kesho yake nikaambiwa niende alone kuchoma sindano manake dozi ilikuwaga ni sindano 5 miaka iyo. nilipofika njian nikajionea tabu si nikautana na rafiki zangu tukaenda kubembea? mbembea zenyewe si hizi za siku izi, kijijini ilikuwa karibu na mto kuna mti, na huo mti umeotea mti wa kutambaa ule ambao huwaga unaota kwa kupata sapoti ya mti mwingine sasa miziz yake ule unaotambaa ndio unaushika kwa mikono miwili unabembea nao. wenzako ndo wanakusukuma. asa mie kule kuumwa, mwili uko weak si nikajishika ili nibembee, ile nasukumwa tu nikenda mara ya kwanza ile narudi mara ya pili nguvu zikaisha nikadondoka kwenye jiwe. Jmani niliumwa acha tu. ikabidi sasa nijipeleke mwenyewe hosp manake nilijua nikifika home maza asingejali mkono umevunjia ama nini ningelemba mboko afu ndo nipelekwe hosp.
ha haaha utoto raha sana .. iala mama zetu walikuwa wanapiga sana aisee
 
Nilichukua miba ya mtende huwa ni mikubwa hivi nikaichimbia nikiacha ncha kali kwa juu katika kinjia wanapita watu halafu nikajificha,akapita kaka mmoja akakanyaga nikacheka akaniona nilikimbizwa mpaka leo sikurudia japo hakunipata.
ha ha ha ha ha ha ha ha wewe umenifanya nicheke mpaka watu wananishangaa hapa!!!!
 
Nikiwa natoka shamba huku nimebeba mihogo kichwani na uchovu na njaa, niliamua kufumba macho ili nisione ninakokwenda na nistukie nimefika au kukaribia

kitu fulani kikaniambaia nifumbue macho nikajikuta katikati ya barabara ila bahati hakukua na magari yanayokua au kwenda
http://www.google.com.sa/url?url=ht...4ILzAN&usg=AFQjCNEMMQVrkeg6_Pub0oqDCxGFFBPxsg
hili tukioa limekua likinirudia sana kichwani kwangu



Je, wewe unakumbuka kituko gani cha hatari au kukufurahisha ambacho hutokisahau maishani
OMG !! Nilisababisha Ajali ya zaidi ya gari 15 katika ROUND ABOUT nilipo katiza kwa miguu !!
 
Dingi si aliwahi kunidaka na mikanda ya X pornograph darasa la tano kipindi hicho VHS nikala kichapo cha kolabo mama baba na broo na mikanda yote ikavunjwa vunjwa

Balaa sasa yule jamaa niliyemuomba mikanda alinidai karibu mwaka mzima na kila akinidaka nlikua nakula makonzi tu sina pakushtaki
Nskumbuka ndugu yangu miaka ya hivi karibuni alivizia mama yake na baba yake awapo akatupia kitu hicho,da umeme zii,jamaa kachanganyikiwa,sasa anajua kwamba mama yake jion humuagizia kwenye mambo ya vikoba,sasa jamaa kafikilia hapa wazee wakirud wakiniagiza harafu umeme ukarud itakuwaje,jamaa katulia tutweeeeeee,walivyorud jamaaa akaongopea km anaharisha kweli wazaz wake walivyorudi wakawa na lengo lilelile la kumuagiza,sasa baada ya kuona kwamba jamaa anaendesha basi wakasema atampelekea asubuhi,jmaaa huku akipiga misele ya ndani chooni,ndani chooon,sasa wakati ile nakwenda chooni anafungua mlango "anasikia uwoooooooooo",jamaaa badala ya kuingia choooni mbio ndan mpka wakamshangaaa,alivyofanikiwa akasema mwanzo na mwisho
 
Nilikuwa na tabia moja, kuwe na joto kuwe na baridi; me Ntalala bila kuvaa nguo kabisa na blanket langu juu.

Siku ya siku nimelala wee, kuja kushtuka saa 1 asubuhi, nimepanic hatari nimeshachelewa shule. Nilichofanya ni kukurupuka piga uniform ndrukiii shule (bahati nzuri home na shule hakukuwa mbali)

Kufika shule nikakuta ndo wanamalizia usafi, na uzuri friends zangu waliniwahia namba. Kuja kutahamaki sikumbuki kama nilinawa uso, ila mswaki sikupiga na tei te (chupi) pia sikuvaa. Nikaona isiwe kesi nikaenda bombani nikanawa, ile kurudi nikawa najishtukia ukute domo linanuka. Nikaanza kupretend kuwa jino linauma so tukawa tunawasiliana kwa vimemo, navyopenda kustorisha sasa khaa niliumiaje. Kufika muda wa break ndo nikatamani nilie kabisa, rede imekolea nashindwa kucheza nisije nikapiga chejo nikamwaga radhi. Sijawahi kuwa na siku mbaya shuleni kama ile. Kuanzia siku ile nikawa nikilala, tei tei naiweka juu ya bag nisije nikasahau kuvaa asubuhi[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nilikuwa na tabia moja, kuwe na joto kuwe na baridi; me Ntalala bila kuvaa nguo kabisa na blanket langu juu.

Siku ya siku nimelala wee, kuja kushtuka saa 1 asubuhi, nimepanic hatari nimeshachelewa shule. Nilichofanya ni kukurupuka piga uniform ndrukiii shule (bahati nzuri home na shule hakukuwa mbali)

Kufika shule nikakuta ndo wanamalizia usafi, na uzuri friends zangu waliniwahia namba. Kuja kutahamaki sikumbuki kama nilinawa uso, ila mswaki sikupiga na tei te pia sikuvaa. Nikaona isiwe kesi nikaenda bombani nikanawa, ile kurudi nikawa najishtukia ukute domo linanuka. Nikaanza kupretend kuwa jino linauma so tukawa tunawasiliana kwa vimemo, navyopenda kustorisha sasa khaa niliumiaje. Kufika muda wa break ndo nikatamani nilie kabisa, rede imekolea nashindwa kucheza nisije nikapiga chejo nikamwaga radhi. Sijawahi kuwa na siku mbaya shuleni kama ile. Kuanzia siku ile nikawa nikilala, tei tei naiweka juu ya bag nisije nikasahau kuvaa asubuhi[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Tei tei ndio nini??!!!
 
Nakumbuka nilikuwa na rafiki yangu, siku moja akawa ana hela, kumuuliza alkozipata akaniambia alipewa na anti yake, kumbe aliiba! Basi tukatumia kila tulichokipata kinachofaa kula ananunua, sasa chenji zilizobaki akaniambia nimuifadhie then tuwe tunatumia wote, kumbe alikuwa anaogopa kwenda nazo kwake, mimi nikaenda kuzichimbia chini karibu na home lakin kuna mtu aliniona nkichimbia yeye akavunga nlipoondoka akaenda kufukua akasepa nazo,yamkini hadi leo sijamgundua! Kesho yake asubuh ndo nlkuja kukuta zimefukuliiwa, nlipoenda shule yule jamaa akaniambiia nimpe hela, nikamwambia nimesahau, tulipotoka shule nkamwambia hela zimepotea baada ya kuzichimbia, daah ghafla nkalamba box, na mimi nkarudisha konde, tukapigana mpka watu wakatuamua ikabidi tupelekwe kwa wazazi wetu ndipo ikabainika aliiba, tukalambwa wote bakora za kutosha...nlikuwa std two wakati huo...
 
Mimi nakumbuka nikiwa DOGO mbu walikuwa wanasumbua sana sasa kuna siku nikasema ngoja niwakomeshe nikachukua kiberiti na kuanza kuchoma neti ili niwateketeze...Nilichezea kipigo cha haja kutoka kwa dingi !!!!!
 
Nikiwa mdogo niliwahi kuiba hirizi iliyokupenda inapumua ya mzee mmoja mchawi aliyekuwa anaogopeka sana pale kijijini. .kwenda kuipasua nilikuta kinyonga aliyekatwa mkia alitweta kwa kukosa pumzi vizuri
Lile tukio lilikuwa kubwa na baya pale kijijini mpaka ikibidi nihamishwe
Wakati unaiba ulikuwa unafikiria nn?
 
Dingi si aliwahi kunidaka na mikanda ya X pornograph darasa la tano kipindi hicho VHS nikala kichapo cha kolabo mama baba na broo na mikanda yote ikavunjwa vunjwa

Balaa sasa yule jamaa niliyemuomba mikanda alinidai karibu mwaka mzima na kila akinidaka nlikua nakula makonzi tu sina pakushtaki
Kijana kumbe we ni bro wangu kwenye hizo vitu..Nakumbuka mi first time kuangalia nilikuwa form one..Basi baada ya kutoka kuangalia kila msichana ninayekutana naye namuona kama yupo uchi vile
 
Back
Top Bottom