hii picha avatar yako ni bro wangu kabisa. Pls kwa heshima naomba usiitumie. Ni mpiga gitaa bendi ya KATAGKumpiga mtu na jiwe,bahati nzuri ndio mambo ya kijijn,maan alipasuka kweli kichwani
Hivi form two bado ni utotoni eehNikiwa form two siku moja sijui nini kiliniwasha ila nilijikuta nimewaropokea madem fulani wawili darasani kuwa break munione niwapeleke breakfast kantini ya shule wakaniambia poa. Mi baada ya dakika mbili nikasahau hiyo habari.
Break ya saa nne ilipofika mi nikatoka na mshkaji wangu tunatembea taratibu nikashangaa navutwa shati kwa nyuma!! kugeuka lahaula ni wale madem na hapo sina hata kumi mfukoni mi niliropoka tu.. nahisi nilitoa haja ndogo sikuile maana nilikosa hata cha kusema na hao ndo madem wakali wa class kwetu. Nilimgeukia mshkaji nikamuangalia kwa macho ya 'leo natamani nigeuke barafu niyeyuke'
Mshaji akatoa noti ya Sh.200/- mpyaa sijui aliiba wapi naye maana naye hana kawaida ya kuwa na mkwanja. Akanipitishia kisirisiri nikawapa wale madem wakasepa.
Jamaa alinipa kichambo cha haja ila niliona kawaida sana hata angekesha ananisema. Ni mshkaji wangu tunasaidiana kwenye shida na raha hadi leo na disemba mwaka jana nimechangia hela ya ng'ombe mzima wakati anatoa mahari
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]Nilichukua miba ya mtende huwa ni mikubwa hivi nikaichimbia nikiacha ncha kali kwa juu katika kinjia wanapita watu halafu nikajificha,akapita kaka mmoja akakanyaga nikacheka akaniona nilikimbizwa mpaka leo sikurudia japo hakunipata.
Mi nadhani hii ni 'deja vu' itakuwa juzi ukubwani ulipotumwa ndo ukafanya hivyo. Sasa ukadhani labda ulishafanyaga udogoni tena.nakumbuka nlivyokuwa naenda kutembea alafu baadaye giza narudi na majani ya ng'ombe siku moja hiyo nlitumwa kitu dukani badala nirudi nkaingia kwenye kibanda cha kuonyesha video kwanzia saa 1 usiku nilirudi saa 4 usiku na pesa nliyo tumwa nayo nilitumia kulipa movie na kunywea chai nilivyorudi nilipigwa fimbo za kufa pipo. Na kuanzia wakati huo sikurudia tena hadi juzi juzi ukubwani
Bend ipo wapi hiyoooMkuu
hii picha avatar yako ni bro wangu kabisa. Pls kwa heshima naomba usiitumie. Ni mpiga gitaa bendi ya KATAG
Good going Einstein. HahahaMimi nakumbuka nikiwa DOGO mbu walikuwa wanasumbua sana sasa kuna siku nikasema ngoja niwakomeshe nikachukua kiberiti na kuanza kuchoma neti ili niwateketeze...Nilichezea kipigo cha haja kutoka kwa dingi !!!!!
Mkuu bendi ipo Kasulu mkoa wa kigoma. Kasulu theatre Art Group chini ya kiongozi MnyikaBend ipo wapi hiyooo
Nimeshindwa kuatach video akiwa kwenye kazi jukwaani utamkubaliMkuu bendi ipo Kasulu mkoa wa kigoma. Kasulu theatre Art Group chini ya kiongozi Mnyika
Teh teh..Nilikuwa sijui maana yake broHahaaaaa no wonder unauza vifuniko vya asali aisee, hizi mambo kumbe unazo tangu utotoni, duuuh kubikiri sistaako!!
Teh teh..Mkuu ufukunyuku wa hayo mambo umeanza kitambo kumbeUtundu wa kitoto tu nilitaka kujua kwanini ile hirizi inapumua na nikagundua kuwa mle ndani anaweka vinyonga, sijui walikuwa wanakaa muda gani mpaka kufa
Nilichoshindwa kujua mpaka leo ni je alijuaje kama mimi ndio nilichukua hirizi yake
Hivi form two bado ni utotoni eeh
Kuna vingine siwezi kuvisimulia hapaTeh teh..Mkuu ufukunyuku wa hayo mambo umeanza kitambo kumbe
Utasimulia kesho asubuhi mkuu..Huu muda wa kulalaKuna vingine siwezi kuvisimulia hapa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Utasimulia kesho asubuhi mkuu..Huu muda wa kulala
Au andaa kitabu mkuu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
hahaha chamechaaNilikuwa na tabia moja, kuwe na joto kuwe na baridi; me Ntalala bila kuvaa nguo kabisa na blanket langu juu.
Siku ya siku nimelala wee, kuja kushtuka saa 1 asubuhi, nimepanic hatari nimeshachelewa shule. Nilichofanya ni kukurupuka piga uniform ndrukiii shule (bahati nzuri home na shule hakukuwa mbali)
Kufika shule nikakuta ndo wanamalizia usafi, na uzuri friends zangu waliniwahia namba. Kuja kutahamaki sikumbuki kama nilinawa uso, ila mswaki sikupiga na tei te (chupi) pia sikuvaa. Nikaona isiwe kesi nikaenda bombani nikanawa, ile kurudi nikawa najishtukia ukute domo linanuka. Nikaanza kupretend kuwa jino linauma so tukawa tunawasiliana kwa vimemo, navyopenda kustorisha sasa khaa niliumiaje. Kufika muda wa break ndo nikatamani nilie kabisa, rede imekolea nashindwa kucheza nisije nikapiga chejo nikamwaga radhi. Sijawahi kuwa na siku mbaya shuleni kama ile. Kuanzia siku ile nikawa nikilala, tei tei naiweka juu ya bag nisije nikasahau kuvaa asubuhi[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Chamechaa ndo nini Mkuu?hahaha chamechaa
Utakisoma?Au andaa kitabu mkuu