Nilikuwa na tabia moja, kuwe na joto kuwe na baridi; me Ntalala bila kuvaa nguo kabisa na blanket langu juu.
Siku ya siku nimelala wee, kuja kushtuka saa 1 asubuhi, nimepanic hatari nimeshachelewa shule. Nilichofanya ni kukurupuka piga uniform ndrukiii shule (bahati nzuri home na shule hakukuwa mbali)
Kufika shule nikakuta ndo wanamalizia usafi, na uzuri friends zangu waliniwahia namba. Kuja kutahamaki sikumbuki kama nilinawa uso, ila mswaki sikupiga na tei te (chupi) pia sikuvaa. Nikaona isiwe kesi nikaenda bombani nikanawa, ile kurudi nikawa najishtukia ukute domo linanuka. Nikaanza kupretend kuwa jino linauma so tukawa tunawasiliana kwa vimemo, navyopenda kustorisha sasa khaa niliumiaje. Kufika muda wa break ndo nikatamani nilie kabisa, rede imekolea nashindwa kucheza nisije nikapiga chejo nikamwaga radhi. Sijawahi kuwa na siku mbaya shuleni kama ile. Kuanzia siku ile nikawa nikilala, tei tei naiweka juu ya bag nisije nikasahau kuvaa asubuhi[emoji23] [emoji23] [emoji23]