Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Mi nakumbuka kuna demu alimzingua jamaa mmoja kitaa..Basi yule jamaa kwa asira akamwambia "ujue ntakubikiri"..Basi mi nikalipenda hilo neno bila hata kujua maana yake..Nikihisi kuwa litakuwa linamaanisha ntakupiga....Siku tumekaa sitting room na wazee pamoja na wagen tunacheki Tv tukaanza kugombania rimoti na sista..yeye akiwa anataka kubadili chanel..Ndo kumwambia "ujue ntakubikiri,we endelea tu"...

Nilipelekwa chemba nikapewa stiki za kutoha..Zen baadae darsa ndo likafwata..Ndo ikawa chanzo cha kupunguza kuokotaokota maneno kitaa


Hahaha....maza atakua alikua anakufuatilia sana kuanzia siku hiyo kumbikiri sister noma haha
 
Wakati niko form 1 shule fulani Arusha(bweni),nilitumiwa pesa ya matumizi kwa TMO,sh2,000. Zilkuwa za kutosha enzi hizo,wakati natoka kuzichukua posta,njiani nikakuta jamaa wanachezesha kamari ya karata,kikundu-keusi. Nikavutika,tamaa ikanijia,nikajaribu. Walikula zote,kasoro 200. Mama moja mpita njia aliniokoa,walitaka kuninyang'anya 200 iliyobaki. Toka siku hiyo sitaki kabisa michezo ya kubahatisha.
 
Hahaha....maza atakua alikua anakufuatilia sana kuanzia siku hiyo kumbikiri sister noma haha
Teh teh..Hawakuwa na wasiwasi kwa hilo..Walijua tu kijana hajui anachoongea..Sema waliamua kunipa kichapo ili niace kuokota maneno mtaani
 
mimi tukio ninalo kumbuka tuliona gari inakuja tukasema tulale barabarani tuone nini kitatokea nakumbuka nilikuwa na age kama 5 or 4 years na gari kuiona kijijini ni kama mara moja kwa mwezi kilicho tokea yule dereva alisimamisha gari akachukua fimbo akanichapa wenzangu wakakimbia baada ya kuchwapa akili ndio ikaja nini kingetokea baada ya dereva kutukanyaga

Nyie kweli mlikuwa na akili za kitaahira
 
Nikiwa mdogo niliwahi kuiba hirizi iliyokuwa inapumua ya mzee mmoja mchawi aliyekuwa anaogopeka sana pale kijijini. .kwenda kuipasua nilikuta kinyonga aliyekatwa mkia alitweta kwa kukosa pumzi vizuri
Lile tukio lilikuwa kubwa na baya pale kijijini mpaka ikibidi nihamishwe

Ahaaaaaa,ndio maana mkuu stori zako ni za kuwangawanga kwa sana,kumbe tokea kitambk mtunduuu
 
Mi nilivyokuwa darasa la nne ripoti iitoka nimefeli kinyama,mwalimu akanipa kwwnye bahasha niipeleke home,mwanaume nikasema ngoja niifungue niicheki,kufungua tu daaaah,kitu nimekuwa wa 67 kati ya wanafunzi 77,nikaona huu ni msala nyumbani,basi nikaifuta ile sita kiustadi sana nikaonekana nimekuwa wa saba,home wakastukia mchezo kwani maksi zilikuwa mbovu halafu eti nimefaulu,weee,nilikula mbata,siwezi kuzisahau kamwe
 
Teh teh..Hawakuwa na wasiwasi kwa hilo..Walijua tu kijana hajui anachoongea..Sema waliamua kunipa kichapo ili niace kuokota maneno mtaani


Hahahah...na ilibidi uache tu hayo maneno mkuu!
 
Baada ya kuona sinema ya "Super Man" mimi na wenzangu tukaiba khanga za Mama zetu na kupanda juu ya paa la nyumba ili turuke twende Zanzibar tukaibe vitu na kurudi usiku ule ule. Bahati nzuri alitangulia kuruka rafiki yangu, akavunjika mkono na mbavu vibaya sana. Kwa uwoga wa kupoteza maisha nikakataa kushuka kule juu ya paa, nikaokolewa na jamaa wa faya. Utoto ni maji ya moto kweli.
Hey superman. Ukaogopa kwenda Zenj...ha ha ha
 
Mmmmh.... mie nilikua napenda sana kucheza mpira wa rede na mumy alikua hapendi, siku hiyo kuna wageni mamaa yupo busy nikakusanya soksi zangu nikatengeneza mpira wangu nikacheze nje.... kimbembe kikawa nitatokaje na mpira mama asijue...nikaweka tumboni tumbo linatuna ikanibidi niufiche kwenye chuppi nitoke nao....nikatoka kwa kujiamini sasa tembea yangu kama nimebakuliwa wananishangaa wewe unamatatizo gani mie kimyaaaa mwishowe mpira ukachoropoka papuchini puuu chin!! Nikikumbukaga nacheka sana
 
Mmmmh.... mie nilikua napenda sana kucheza mpira wa rede na mumy alikua hapendi, siku hiyo kuna wageni mamaa yupo busy nikakusanya soksi zangu nikatengeneza mpira wangu nikacheze nje.... kimbembe kikawa nitatokaje na mpira mama asijue...nikaweka tumboni tumbo linatuna ikanibidi niufiche kwenye chuppi nitoke nao....nikatoka kwa kujiamini sasa tembea yangu kama nimebakuliwa wananishangaa wewe unamatatizo gani mie kimyaaaa mwishowe mpira ukachoropoka papuchini puuu chin!! Nikikumbukaga nacheka sana
Ungemwambia mother nimezaa..!
 
Hahaaaa hii imefanana na yangu
Tulikuwa tunafuata mikate ya shule, enzi hizo form one. Katikati ya safari tunaingia kichakani tunachokonoa mikate tunakula minofu ya ndani. Kesho yake wanakati wa breakfast watakaopewa hiyo iliyoliwa ndani shauri yao na hawalalamiki coz na wao ikifika zamu yao wanafanya hivyo hivyo, teh
ha ha haha ha utoto raha sana
 
Nikiwa chekechea Moja iliitwa Neema pale kikuyu Dodoma, Enzi hizo habari za chuna ngozi zilitapakaa sana kwamba wanadanganya watoto Kwa pipi au wanateka Kwa nguvu, mama akaniambia nikitoka shule nisiwe napitia popote niende nyumbani straight.. Sasa kukawa na kasichana kanaitwa Ashura alikuwa rafiki sana na tulipendana... Yeye kwao ilikuwa karibu na kamlima Hivi, umbali kiasi na njia yao ina mapori.. Kwa mapenzi nliyokuwa nayo nikawa napuuza amri ya mama namsindikiza Ashura hadi karibu na kwao naiona nyumba ileee, halafu narudi mwenyewe spidi 120 mbio....
Mnh...
Ujasiri pendoni nmekua nao masikini mini!! .. Sijui yuko wapi siku hizi Ashura dah.!
kaolewana anagongwa na wengine ha ha ahhaha
 
Mwalimu kaingia darasani:

Wanafunzi wote tukasimama, na kutoka salam. Sasa sijui ilikuaje tu likaja wazo, nikaenda kutoa kiti cha mmoja wa jamaa alikua anajiona mjanja sana. Wakati mwalimu anasema 'Okay sit down' jamaa anakaa tu akaenda chini...dah class nzima wakaona na toka siku hiyo alikua mpole...utoto una raha yake
 
Nakumbuka nilikuwa na rafiki yangu, siku moja akawa ana hela, kumuuliza alkozipata akaniambia alipewa na anti yake, kumbe aliiba! Basi tukatumia kila tulichokipata kinachofaa kula ananunua, sasa chenji zilizobaki akaniambia nimuifadhie then tuwe tunatumia wote, kumbe alikuwa anaogopa kwenda nazo kwake, mimi nikaenda kuzichimbia chini karibu na home lakin kuna mtu aliniona nkichimbia yeye akavunga nlipoondoka akaenda kufukua akasepa nazo,yamkini hadi leo sijamgundua! Kesho yake asubuh ndo nlkuja kukuta zimefukuliiwa, nlipoenda shule yule jamaa akaniambiia nimpe hela, nikamwambia nimesahau, tulipotoka shule nkamwambia hela zimepotea baada ya kuzichimbia, daah ghafla nkalamba box, na mimi nkarudisha konde, tukapigana mpka watu wakatuamua ikabidi tupelekwe kwa wazazi wetu ndipo ikabainika aliiba, tukalambwa wote bakora za kutosha...nlikuwa std two wakati huo...
ha ha ha
 
Utoto raha.

Nakumbuka tulikuwa tunalinda ndege shambani sasa tukawa tunapewa chakula tunaenda nayo..

Siku moja tukashiba na kutupa ugali ulobaki.

Baada ya miaka kama miwili ikaja njaa kubwa kijijini watu wakawa wanashinda njaa ikitokea mara moja moja mnapikiwa uji siku inapita.

Si nikakumbuka tuliwahi kutupa ugali kipindi cha nyuma , ikabidi niwaambie wenzangu twende kutafuta ugali tulotupa miaka ilopita ili tule.

Kufika tuliambulia patupu
ha ha aakili ya utoto bwana
 
Back
Top Bottom