Kituko gani alikufanyia mtoto wa mwenyeji wako ulipokuwa ugenini huwezi kukisahau hadi leo hii?


Akiolewa ndio utasikia ooh mume wangu nataka nimdhibiti kwa mganga kumbe yeye ndio mchawi
 
Kwangu angekufa njaa huyu, au la mama ake ndo amtumie hizo hela za chips.
 
Duuuh malezi hayo,
 
Dogo aling'ang'ania miwani Hadi akaivunja hakurizika akatoka nje viatu nilivulia mlangoni akavichukua akavikojolea dada wa kazi akampiga mama mtu akaja juu eti kwanini usingemwambia kwaustarabu maana mtoto hajui chochote niliaga hapo hapo na sijawahi Tena kukanyaga Ile familia
 
Tupo Sebuleni tunatizama Habari ITV namsikia kabisa kuwa Kajamba Yeye ila kwakuwa yuko Kwao akanisingizia Mimi na Mimi kwa Hasira sasa nikaamua Kuwajambia Mubashara ambapo Harufu ya Mjambo wangu ikaonekana ni tofauti na yake ndipo Baba yake akamkamata na Kumchapa sana Viboko na baadae Kuniomba Radhi pia.
 
Nimevua viatu vyangu natoka havionekani kuzunguka nyuma wamejaza michanga na mawe wanaendesha gali.
Nikajisemea moyoni nitawafuraisha Hawa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]khaa!
 
Unakosea sana kumpa pesa,
Anatakiwa asosi kinachokuwepo,hataki alale njaa ama arudi kwao.
 
Siku ondokeni wote mapema mumuachie nyumba na vyakula vibich msimpe Hela mtakuta kapika pilau njaa sio mchezo
 
Niliendaga kwa anko

Mwanae wa miaka minne,nimekaazangu nachart si aKaanza kulia,mama yake akamuuliza unataka nini??,,,,,,,,,kakasema kanataka simu yangu kaangalie vichekesho,

Mama yake akaniambia warda mpe mtoto simu achezee maana amezoea kuchezea simu yangu sasa ni mbovu

Nikamwambia sinaga hayo mambo kwenye simu yangu na ata kama zingekuwepo nisingempa katu,atafute cha kuchezea,,,auntie alinuna,,Mtoto wanamlelea kwapani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…