Kunguru wa Manzese
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 12,729
- 18,119
Mimi kukaa kwa ndugu hapana unakuwa huna uhuruNimesoma hizi, zinafurahisha lakini pia kuhuzunisha.
Nawashauri hasa vijana wa kiume ambao wamemaliza chuo au kurudisha mpira kwa kipa ni heri waende kwao kabisa au kwenda kwa mshikaji wako mkapambane pamoja kuliko kwenda kuishi kwa ndugu
Nakumbuka kipindi fulani miaka hiyo ya nyuma nilikuwa nimemaliza chuo, na nimepambana ila mambo magumu ikabidi nirudi mkoani huko kanda ya ziwa na kufikia manispaa kwa mama mdogo ambae anamfuatia mamaangu. Kiuchumi walikuwa poa sana na mme wake na walikuwa na mtoto wao mmoja darasa la 5 ambae anasoma hizi international school
Nimekaa pale mara zikaanza mambo za kuhakikisha kanakula, mara kuosha vyombo ingawa mfanyakazi yupo mara siku nyingine mpo wote na wazazi wake katoe taarifa ya Habari kanaweka katuni yaani vurugu tu.
Siku niliyoamua kutoenda kwa watu
Ni ile kamerudi shule kakaenda kucheza na nguo za shule halafu mamaake akanifokea kwanini nmekaacha kacheze na nguo hizo aiseee nilikakamata nikakapiga. Kakalia kanasema "uondoke uende kwenu sisi hatukutaki hapa, huku kanagalagala chini" na mzee wake akatoka huku anafoka anasema nani Kampiga mwanangu akamchukua akaenda nae town kukanunulia zawadi. Aiseee nilikaa siku mbili nikaondoka nikarudi dsm nikafikia kwa mshikaji tukapambana tukapata ajira na sikuwahi kurudi tena mpaka ingawa huwa tunawasiliana tu. Hata nikienda kikazi kanda ya ziwa sijawahi fikia kwa hao ndugu ingawa wamejenga sana. Mtoto wao huyo alifika six akazingua wakamfanyia mchakato akasoma chuo wakampa asimamie sehemu kapigisha hasara mpaka mzee wake ana sukari, starehe kwa sana kazi anazingua
Jamani malefic ndio kila kitu. Unajitahidi, unapambana unatoboa halafu wanao unawalea kimayai huwaonyeshi namna hela inapatikana ili wawe na nidhamu eti hutaki wateseke ona sasa unasema eti amepata mental health wakati ulimjengea entitlement ya kila kitu bila kumfanya atake responsibilities kwa kila maamuzi anayofanya.
Ni hayo tu tusijisahau kwenye malezi kisa uzungu
Bora kwenu hata kama njaa kali