Kitunguu swaumu na upara

Kitunguu swaumu na upara

Kijana kijana

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2018
Posts
2,546
Reaction score
2,621
Nimepata taarifa kutoka kwa bwana mmoja aniambia nitumie kitunguu swaumu kwa kukiponda ponda kisha nisugue kwenye nywele zangu ambazo zimeanza kufifia kama upara kisha zitaanza kurudi.

Nipo kwenye dozi hapa na kweli nikipaka nasikia hasa inaingia nahisi ndo inapenya zake ndani kwenda kurekebisha maoto.

Kama kuna mtu ashawahi tumia tofauti na hii tushare maujanja au kama kuna mtu naye nywele zake zinapotea basi namkaribisha tutumie.

Feedback muhimu
 
unachanganya na nini mkuu?

1. Olive oil vijiko 2 vya chakula
2. Asali kijiko 1 cha chakula
3. Mdalasini kijiko 1 cha chai
Pasha moto olive oil kisha changanya vyote kwa pamoja paka kwenye nywele acha kwa muda wa dakika 20 kisha osha nywele zako na upakae mafuta zikishakauka...

si chai hii, yanasaidia sana
 
unachanganya na nini mkuu?

1. Yanasaidia kufanya mzunguko wa damu kufanya kazi vizuri kwenye ngozi ya kichwa na kupenyeza hadi kwenye shina ya nywele kisha kuifanya nywele inayoota kuwa imara
2. Yansaidia kupambana na mba kwenye ngozi ya kichwa
3. Yanasaidia uzalishwaji wa mzizi au shina ya nywele
4. Yanasaidia uzalishwaji wa melanin ambayo inafanya kazi ya kutoa rangi ya nywele inayotakiwa.
5. Yanasaidia kuifanya nywele isiwe kavu sana.
 
1. Olive oil vijiko 2 vya chakula
2. Asali kijiko 1 cha chakula
3. Mdalasini kijiko 1 cha chai
Pasha moto olive oil kisha changanya vyote kwa pamoja paka kwenye nywele acha kwa muda wa dakika 20 kisha osha nywele zako na upakae mafuta zikishakauka...

si chai hii, yanasaidia sana
huu ni mchanganyiko wa kuupaka kila siku au inatosha kuutengezena ukatumia wiki nzima
 
Nikajua unazungumzia Mzee Machache (mmiliki wa TV pendwa) na Bakayoko
 
huu ni mchanganyiko wa kuupaka kila siku au inatosha kuutengezena ukatumia wiki nzima

kwa kuwa asali na mdalasiri ukivichanganya haviwezi kukaa muda mrefu ni vema ukachanganya kidogo tuu, chini ya vipino nilivyokueleza hao juu, ili utumie kwa siku itapendeza
 
Naona unatengeneza new species.
Pass that trait to your offsprings then tupate kikazi kipya chenye aina flani ya nywele Amazing sana
 
kwani kipara ni ugonjwa? mbona watu wanapambana na kipara kiasi hicho? au ndo tuseme wanapambana na uzee!

duuh! kweli ujana raha.
 
Madhali cha kwangu hakiumi wala hakiwashi na kiwepo tu .,. Ila mpaka uje ugundue Nina airport labda niwe chaka.
 
Back
Top Bottom